My Blog List

Friday, December 22, 2006

MASLAHI YA NCHI NI ZAIDI YA SIASA NA HISIA ZA WATU

Unaposikia tofauti kati ya siasa na maslahi ya nchi mfano mzuri uko hapa kwenye maziwa makuu.
Pia kuna hili la kalenda ya uendeshaji wa ligi ya soka.
Pia huko Kenya rais Kibaki atakuwa Mombasa kama kawa.

Thursday, December 21, 2006

HAKUNA HAJA YA MIKOPO ELIMU YA JUU-PROF: MAAMDANI

Wakati wabongo tunalia na JK kuhusu mikopo ya elimu ya juu, yule profesa maaarufu, Maamdani kachapisha kitabu akisema eti serikali isilipie ila wote tulipie elimu

Tuesday, December 19, 2006

JK NA JINAMIZI LA CCM NDANI YA MWAKA MMOJA IKULU

JK sasa anaanza kuona ukweli halisi wa bongo kuwa tatizo liko kwenye CCM. Hili ni jinamizi ambalo JK ana kazi ngumu kuliondoa manake ncchi imeoza na itagharimu Taifa sana kuweza kuondoa hayo ambayo JK kakemea jana.

SALAM ZA CHRISTMAS

Tunasherehekia Krismas soma jinsi makasisi wa dini mbalimbali(mapadiri na wachungaji na mashehe pia) walivyobadilika siku hizi na tunakkumbushwa je Yesu wa wakristu angezaliwa leo ingekuwaje Afrika?Alafu nataka uone ni jinsi gani wabunge wa Afrika hasa Uganda walivyo na ulafi na mapenzi na MABENZI na si wananchi, yaani wanatishia serikali pale inapotaka kuwakata usawa.
Mwisho, ona jinsi Jaji Kiongozi Uganda hisia zake juu ya utawala bora.Alafu mkuu wa Jeshi la polisi Uganda naye anaamua kumjibu na kumkosoa ikibidi Jaji Kiongozi, patamu hapa.
Alafu wajue watu kumi waliotingisha Uganda mwaka huu.

Friday, December 15, 2006

MKE WA MUSEVENI KATIKA UGOMVI KUMTETEA MUMEWE

Mke wa rais Museveni ambaye ni mbunge jana inasemekana karushiana maneno makali na mwanamama mmoja wa shoka wa chama cha upinzani katika kile kinachoonekana kutetea rekodi mbovu ya mumewe ndani ya bunge.
Alafu unajua kwanini maprofesa wa Makerere wamegoma? Soma haya.

Wednesday, December 13, 2006

UDIKTETA-SIRI YA KUISHI MUDA MREFU

Eti madikteta hawafi mapema, tunahimizwa tuwe majitu korofi na dhalimu ili tuishi muda mrefu.

Thursday, December 07, 2006

JK AIGE KUTOKA KWA CALDERON WA MEXICO

Kama kweli Tanzania inapenda maendeleo tunahitaji kiongozi kama huyu aliyechaguliwa huko Mexico majuzi. JK angekuwa namna hii na akatekeleza basi tunaweza kufanikisha "Maisha bora kwa kila Mtanzania".
Vinginevyo JK anatania tu.

UHURU BONGO--BONGE LA PATI SAWA AU DHIHAKA?

Kama mtanzania sina budi kujumuika na watanzania wenzangu kuadhimisha siku hii ya miaka 45 ya uhuru wa Tanzania bara(Tanganyika).Huu ni wajibu wa mzalendo yeyote kutathmini je uhuru wetu umeleta tija kwa watanzania wote au kwa kukundi fulani ndani ya jamii tu?Sisherehekei manake kwa hali ilivyo si muafaka kwa hili bali ni wakati wa kujiuliza kwa nini tunaendelea kuharibu uchumi wetu namna hii?Sherehe tuwaachie wanaoona matunda ya uhuru kama akina JK na Ngoyai: hawa kwao hakuna tatizo la umeme, maji wala usafiri au barabara mbovu. Kwao wanazo njia mbadala kutatua haya.
Nimefuatilia sherehe za uhuru leo kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam(RTD) kwani wakati ndio sherehe inaanza hawa jamaa wa Tanesco wakakata umeme alafu ikaw ndio mwisho wa kuangalia Runinga yangu.Matanzgazo ya RTD hayasikiki vizuri nashangaa kwanini RTD wasiweke mtambo wa FM manake hizi FM radio nyingi ni muziki kwa kwenda mbele utadhani siku ya leo ni sawa na zingine. Ni Radio Free Afrika ya Mwanza na Sauti ya Injili ya Moshi angalau leo wamekuwa na vipindi kuwahoji watu ambao walihusika na uhuru wetu wakati ule na wametoa mawazo murua kweli. Nakwambia tukio hili hapa Moshi si la muhimu kama siku ya jumapili au sikukuu ya Idd El Fitri kwani siku hizo umeme ni bwerere.Hasira imenishika kwani baada ya sherehe kumalizika hawa jamaa wanawasha umeme, nakwambia Tanesco hapa Moshi hawajui uhuru kabisa. Hayo tuyaache, ila JK hotuba yake ilikuwa nzuri nampongeza sana. Ila aliangalia tu mafanikio nchi iliyojipatia tu tangu 1961, ameacha kuzungumzia matatizo kama haya ya Umeme.

Nami naona nieleze kwa ufupi japo ninafikiri nini siku hii:

Mtizamo wangu unatia wasiwasi sana kama kweli tumefikia mafanikio ya dhati kulingana na kipindi cha miaka 45. Naanza na sekta ya barabara tumefeli kabisa. Bado hatujaweza kuunganisha nchi yetu kwani tunalazimika kupitia Kenya kusafiri kutoka Arusha kwenda Mwanza, Bukoba au hata Kampala.

Pili bado tunakumbwa na njaa kila mwaka ilihali tuna ardhi, mito kibao kuwezesha kilimo cha umwagiliaji. Ukija kwenye maji ndio usiseme kabisa. Hakuna maji kunywa ya kutosha hata katika miji kama Dar es salaam, Arusha na hata Mwanza.
Huwezi kuamini nchi yenye umri wa miaka 45, haina umeme wa kuaminika na kutosha angalau mautmizi ya majumbani achilia mbali viwandani. Viongozi, yaani wanasiasa hawana utashi wowote kwa maendeleo ya jumla ya nchi. Maslahi binafsi yamewekwa mbele kuliko uzalendo: kwa mfano, nchi inagenishwa kwa kubadilishana/bei poa kati ya watu fulani ndani ya tabaka tawala(elites) na si kwa maslahi ya mtu.
Ukija kwa watunga sheria(Wabunge) ndio basi tena. Bunge limekuwa jamvi la kila mtu siku hizi hata wendawazimu au kwa maana nyingine mbumbumbu kielimu nionavyo kutokana na matendo yao.Elimu si tija kwa mtu kuwa mbunge au diwani. Nidio maana bunge letu ni taasisi ya kubariki mambo yasiyo na maslahi kwa Taifa ila Chama(CCM) na yale ya binafsi. Chama tawala kimelimeza bunge na kutupeleka kuzimu kiuchumi. Tumefika mahali mtu akiheshimu taaluma katika kusimamia au kuamua mambo ya kiuchumi na mengine ya msingi kama hayo anaonekana mwehu na si mwenzetu. Hii ndio miaka 45 ya uhuru tunayosherehekea. Hili ni lazima tulitafakari la sivyo uhuru unakuwa hauna maana.
Kwa robo mwaka sasa nchi iko gizani, hakuna umeme na viongozi na wahusika wetu hawajali kabisa. Ufisadi na kulindana ndio umetufikisha hapa tulipo na viongozi wahujumu hawaguswi bali wanahamishwa kutoka idara au wizara moja hadi nyingine kuendeleza uharibifu. Vipaumbele vyetu ni vile visivyo; viongozi wetu wamebakia kusafiri kutembeza bakuli kwa wafadhili na kuhimiza uwekezaji katika nchi isiyokuwa na umeme wa kuaminika bila aibu. Kiongozi mkuu anadiriki kusema tatizo la umeme limerithiwa kutoka serikali iliyopita bila kung'amua alikuweko ndani ya serikali hiyo.
Kisiasa, nchi imebaki hoi kabisa; vyama vya upinzani viko hoi kabisa na havionekani kuchukua hatua madhubuti kutia changamoto kwa CCM inavyoboronga. Haya yakiendelea, CCM chini ya Makamba imebakia kuwarubuni wapinzani makini kurejea CCM kama ndio kipaumbele. CCM haitaki changamoto, kwake kuwa mpinzani ni uadui, si uzalendo kwa nchi. Kweli hapa hatutaelewa wapi tunakosea kama tutaendelea hivi na ndio maana bado tuko nyuma maeneo mengi. Demokrasia yetu ni kama vile "maonesho kwa wafadhili"(show-off) na sio demokrasia ya dhati.
Viongozi wetu kama vile Lowasa na Makamba wanaongoza kwa sera kongwe za kihafidhina. Hili ni tatizo la viongozi ndani ya chama tawala, serikalini na hata vyama vya upinzani. Tunahitaji kizazi kipya cha uongozi nadhani ili tuendelee. Hata hivyo, kama Taifa tumefanikiwa kubaki na umoja wa kitaifa kitu muhimu kwa nchi yeyote.
Amani tuliyonayo ni lazima tuikuze kwa kuziunda upya taasisi za kidemokrasia katika utawala ili muongo ujao tupige hatua kwa haraka na si kama miaka hii 45 iliyopita. Katiba ni lazima iangaliwe upya ili miundo ya mihimili mitatu ya dola ifanye kazi inavyopaswa kwa uhuru na si kama sasa kwa kulinda maslahi ya chama tawala. Hii imefanya kwa mfano bunge letu kubaki kama muhuri wa udhalimu "rubber stamp" wa serikali mara kwa mara.
Mwisho, ingawa wenzetu wa magharibi iliwachukua muda mrefu kufikia mafanikio ya demokrasia, sisi isiwe kisingizio, kwani dunia ya leo mambo yamerahisishwa ni lazima tuendelee haraka. Nitoe rai: Tuna wasomi wengi wa kila aina Tanzania ila wote wamefungwa jela ya nafsi zao(conscience) na wamekuwa bendera fuata upepo(sycophants) mbele ya wanasiasa wa chama tawala. Ujasiri unahitajika kwa wasomi wa nchi hii la sivyo kama nchi tutaendelea kusherehekea uhuru wa wachache kama tunavyofanya leo hii. Kwani mantiki ya nchi huru sidhani ina maana kwa watanzania wengi wa kama kule vijijini pembezoni mwa nchi hii. Na kwa akina JK, Ngoyai na Makamba: kumbukeni turuhusu changamoto ndani ya chama na hata serikalini kwani ikiwa tutafanya hivyo hatutaona mikataba ya kijinga kama hii ya IPTL, Richmond, Usiri wa biashara ya mihadarati na mengine mengi ambayo hayasemwi kwa kuogopa kumkosoa bwana mkubwa.

Wednesday, December 06, 2006

KAGAME-MUNGU MTU- ASHTAKIWE TU

Naiangalia hali ya Rwanda kama ni tatizo ambalo waafrika hatuwezi kulitatua kwani kihistoria ni vigumu. Sina imani sana na mahakama ya Arusha kwani naiona kama mahakama iliyoundwa na washindi wa vita(RPF) ili kuwahukumu washindwa.
Ndipo hapa ninapokuwa ninamuunga mkono huyu jaji wa kifaransa kutaka pia Kagame ashtakiwe. Sidhani kuna suluhisho la kiafrika, ila naunga mkono juu ya nia ya mficho ya Ufaransa katika sakata hili. Pia nionavyo tutarajie Rwanda yenye matatizo sana hapo baadaye kwani Kagame inasemekana ni kiongozi Mungu mtu.Tatizo letu waafrika ni kutokupenda kusema ukweli na kama tutaendelea na uwongo huu wa Kagame hakuna maridhiano Rwanda.
Lakini pia ni lazima tujue pande zote mbili zilihusikaje katika kile kinachoitwa ukombozi wa Rwanda?Kwa mfano, picha halisi ya ushiriki wa Kagame na Habyarimana unaweza kuisoma na kupata hali halisi hasa hii makala ambayo mwandishi anao uelewa sana wa mambo ya Rwanda.

Tuesday, December 05, 2006

BESIGYE ALIVYOMNYANG'ANYA MUSEVENI MKE

Pamoja na kufuatilia habari za wanasiasa kadhaa ni vyema pia wakati mwingine tujue habari zao binafsi. Leo nataka nieleze habari za kiumbea ambazo niliwahi kuzisikia juu ya Museveni, Kiiza Besyige na huyu mwanamke wa chuma(iron lady) Bi Winnie Byanyima.
Inasemekana ugomvi kati ya Museveni na Besigye pia unachangiwa na kuibiana mabibi. Eti Bi. Byanyima awali alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Museveni wakati wa vita ya msituni. Wakati huo Besigye akiwa kama daktari wa Museveni. Leo hii Bi. Byanyima ni mke wa Besyigye japo nakumbuka niliwahi kumsikia akihojiwa na redio moja Kampala na akadai kuwa eti Besigye ni mshirika wake tu(companion).
Wambeya wanadai eti siku waasi wa Museveni(NRA)wanaiteka na kuitwa Kampala, waliingia Kampala huku gari alilokuwemo Museveni likiendeshwa na Bibie huyu.
Hayo yote tisa, kumi leo hii Dr. Besigye kaamua kuyaanika yote yaliyojiri kule msituni na ni jinsi gani walikutana na bibie huyu.
Kama kawaida, Uganda ni nchi iliyojaa visa vya kisiasa vya kiume kweli si kama Tanzania, soma huyu mpinzani madhila aliyokwishapitia.

RAIS NA GAVANA UGANDA--WAWAKAMUA WALIPAKODI KWA BIASHARA BINAFSI

Mimi ni kati ya wasioamini adhabu ya kifo hata kama mtu kafanya nini. Ila nimeshangazwa sana na nchini Uganda hata katiba inaruhusu kama ilivyo pia kwetu Tanzania. Lingine ni hili la Rais Museveni na gavana wa benki kuu wameamua kutumia pesa za wali pakodi kumsaidia mfanyabiashara mmoja asifilisike.Ila inasemekana huyo mfanyabishara ni jamaa tu anasimamia shughuli za mzee.
Kama kawaida yangu napenda sana kujua inakuwaje watu wengine wanafanikiwa kimaisha wangali wadogo?

Monday, November 27, 2006

MJUE GENERAL SALEH WA UGANDA

Leo nataka watu musome juu ya jamaa ambaye anajulikana kama shujaa hapa Uganda na ambaye ndie aliyesababisha kuanguka kwa serikali ya Obote.

Wednesday, November 22, 2006

MGAO WA UMEME UGANDA NI MIAKA MITATU SASA JE BONGO?

Huku tukiwa tunalaumu wanasiasa wetu juu ya labda hujuma au rushwa juu ya matatizo ya umeme nchini Tanzania kwa sasa, huko Uganda mgao wa umeme umekuweko kwa miaka mitatu sasa na ahadi kama hizi za hapa Bongo ni kawaida.
Mgao umeendelea hata pale serikali ya Uganda ilipobinafsisha shirika la Umeme kwa jamaa wale wa Afrika kusini kama tulivyofanya sisi.
Pia msome jinsi Museveni na Besyige walivyofanana.

Saturday, November 18, 2006

NIMEKOSA MKUTANO

Wanaglobu nilijaribu kuingia ukumbini mambo yakashindikana na hivyo nikakosa kikao, inasikitisha sana.
Bassi leo nikasoma haya:Soma zaidi juu ya historia ya mtu mweusi, je kalaaniwa na Mungu? Pia hebu tujue zaidi ni kwa vipi chama tawala nchini Uganda kinavyoruhusu demokrasia?
Alafu huyyu jamaa namzimia kweli kashinda tuzo ya UN.

Friday, November 17, 2006

JOJI KICHAKA ANASAIDIWA NA BABA YAKE

Baba yake Joji Kichaka karudi kumkomboa mwanaye.pIA soma jinsi mpanga mikakati wa Bush alivyochemsha.

Thursday, November 16, 2006

UKIMWI, MADEREVA WALEVI-FAIDA KWA UCHUMI

Leo nawapa vituko vya jamaa mmoja mcheshi kwelikweli. Eti anadai Ukimwi ni dili kwa bara la Afrika na ukiangamizwa, bara letu halitapata misaada.Alafu anaongeza zaidi kwamba uendeshaji magari wakati mtu ni mlevi ni faida kwa uchumi wa nchi.

KUPINDISHA HABARI(SPIN) KUNA MWISHO WAKE

Yuko jamaa mmoja alikuwa ni mwandishi mpambe haswa wa Raisi Museveni. Nakwambia alijua kazi yake haswa ya kupindisha habari (spin).Inasemekana ukweli umemsuta kaachana na Museveni sasa.
Ukiacha mambo ya habari tuangalie ni kwanini wanafunzi wanagoma haswa kule Makerere?Leo pia niwaletee hadithi juu ya mapambano ya msituni wakati Museveni alipozimia vitani kama inavyoelezewa na Dk. Kiiza Besyige aliyekuwa daktari wa Museveni. Alafu ni jinsi gani ukabila ulichangia kuuawa kwa waheshimiwa kadhaa hapa Uganda wakati ule wa vita kila kukicha.

Wednesday, November 08, 2006

OMBAOMBA WA AFRIKA CHINA

Eti marais wa afrika kule China walikuwa makini au ombaomba tu?Alafu huko China tunaambiwa Museveni alifanya mambo ya kihistoria.Wakati Tanzania tumemaliza kipindi cha jeshi letu la polisi kupoteza mwelekeo kutokana na Kamanda wa polisi wa hovyo, huko Uganda hebu msome IGP wa kule ni mtu gani na umfananishe na alipita kwetu "MAHITA".
Alafu kuhusu dini kuna wanaoamini watu weusi tumelaaniwa na Mungu. Ila huyu anakataa katakata.Pia kama mtu wa ukanda huu wa afrika, je jumuiya yetu tuianze?
Mwisho waafrika eti tumezidi kupenda watoto wadogo visivyo?

KUWAJIBIKA TANZANIA MPAKA UTOE ROHO YA MTU--JK

Hapa Tanzania wanasema "hapa ndipo patamu" yaani Anko Dito, naye yuko maabusu baada ya kutuhumiwa kuua raia mwema.Natizama tukio hili kama dhihirisho la wanasiasa wamangimeza wa kiafrika. Ulevi wa ukubwa unamfanya mtu kujichukulia madaraka mikononi mwake, kwani atafanywa nini?
Dito, ni mzalendo wa hali ya juu ninavyofikiri ndio maana JK hata aliweza kumpa madaraka.Ni kati ya vigogo wasioshikika nchi hii naweza kusema"untouchable".Ndio maaana nina wasiwasi sidhani kama atapatikana na hatia baada ya sheria kufuata mkondo wake.
Jana kasifiwa eti kujiuzulu ni kitendo bora kutokana na tuhuma anazokabiliana nazo. Kauli ya JK katika kukubali kujiuzulu kwake imenifanya nipate swali moja kwa wanaglobu wote: JE NI MPAKA MTU ATUHUMIWE KUTOA ROHO YA MWANANCHI MWENZAKE NDIO ANAJIUZULU? Nauliza hivi kwani hivi majuzi wako wakuu wa wilaya: HAWA NGULUME na Mheshimiwa fulani SABAYA wanatuhumiwa kupiga wananchi makofi na vyombo vya habari vimeamua kulamba miguu na kutovalia njuga ukiukaji huu wa haki za binadamu.
Yuko pia muheshimiwa mpendwa sana, POMBE MAGUFULI, tayari ana tuhuma kibao za ukiukaji wa maadili ya kazi, naye pia rais haoni kuna haja ya kumuwajibisha.
Tukiendelea hivi tutafika? Au mpaka mtu aue tu ndio tutawajibika?Wanablog mnasemaje hapa?

Saturday, October 28, 2006

ETI MKAPA AANZE KUPOKEA TUZO YA UTAWALA BORA?

Wengi nadhani Tumesikia eti Maraisi wa Afrika sasa watapewa zawadi kama watatawala kwa ubora.
Jamaa huko Uganda kapendeza eti Mkapa apewe tuzo hiyo kama kifuta jasho.

Friday, October 27, 2006

NILICHOSOMA

Yuko bibie Kampala hapa inaelezwa ni wanaume wenye sifa zipi watamfaa?
Kisiasa, kuna kitabu juu ya udanganyifu wa Marekani hapa duniani.

MAMBO YA JAMII LEO

Napenda Chuo hiki cha elimu ya juu Nkozi University. Kuna jamaa kaoa ndugu yake wa damu, yaani dada yake.Ulishasikia haya? Wanawake wa Uganda na malove.
Kuhusu yule fashisti Idi Amin alipompindua Obote alitoa sababu kumi na moja za mapinduzi. Pia nchi ya Uganda inaye askari mkakamavu na msomi, msome hapa.
Mambo ya maisha ya ndoa ni misuguano mitupu; kwenye siasa napo Kagame bado anamuumbua Museveni.

MAMBO YA JAMII LEO

Napenda Chuo hiki cha elimu ya juu Nkozi University. Kuna jamaa kaoa ndugu yake wa damu, yaani dada yake.Ulishasikia haya? Wanawake wa Uganda na malove.
Kuhusu yule fashisti Idi Amin alipompindua Obote alitoa sababu kumi na moja za mapinduzi. Pia nchi ya Uganda inaye askari mkakamavu na msomi, msome hapa.
Mambo ya maisha ya ndoa ni misuguano mitupu; kwenye siasa napo Kagame bado anamuumbua Museveni.

Sunday, October 15, 2006

Saturday, October 14, 2006

HANA MFANO

Nyerere haenziwi kabisa.Je tunajua asili ya waafrika ni wapi?
Alafu wale wanaoanza gemu la penzi, unajua ya muhimu hapo awali?Kwa wanaume je twajua akina mama na dada siku hizi wanapennda sana pesa?
Huu ni wasifu wa mtu ninayemhusudu sana.

Friday, October 13, 2006

UGANDA NA SALA ZA KILOKOLE

Yuko Jaji Mmoja maarufu nchini Uganda ambaye anakerwa sana na wanasiasa wa nchi hii. Basi katunga shairi babu kubwa juu ya uzandiki wa wanasiasa wa Uganda.
Kituko kingine cha wanasiasa ni tabia ya akina Museveni na mkewe kupenda kuhudhuria sala za kilokole kuiombea nchi kitu kinachoonekana hakina msaada wowote kwa nchi.Sala inaonekana ni ulevi wa wanasiasa.
Je wajua kuwa soko huria ndio balaa kuu la umasikini uliokithiri Africa? Alafu gazeti la serikali Uganda, hatimaye lamfukuza kazi meneja wake mzungu.

KUMBUKUMBU YA OBOTE BAADA YA MWAKA.

Hii ni wiki kubwa sana ya kuwakumbuka waasisi wa Afrika Mashariki. Kwanza jana imekuwa siku ya kumkumbuka Milton Obote, rais wa kwanza wa Uganda. Mkewe kaongea juu ya mumewe hasa ni yapi yanayomfanya amkumbuke.Obote kama binadamu anazo pande mbili hebu zisome:Pia ujue hivi ni upi mchango wa Obote katika siasa za Uganda na Afrika na alikuwa ni mtu wa aina gani?
Ukiacha kumbukumbu, huko Uganda baraza la mawaziri wanakosoana sio kama hapa kwetu Tanzania tunaoneana aibu na kufunika kombe mwanaharamu apite.Pia Uganda tunakumbushwa kuwa panapokuwa na amani sana basi ujue haki hakuna kabisa.
Mambo ya mahusiano, je una mpango wa kuchumbia siku za karibuni?Mwisho soma juu ya wanamuziki wa Uganda.

Saturday, October 07, 2006

WABUNGE WA UGANDA NA MAGARI YA KIFAHARI

La msingi kabisa ni Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kuna mpango umeandaliwa wa kukusanya maoni ya watu.Je ni sahihi kuutekeleza?
Leo soma haya ya wabunge wa Uganda wamehongwa na serikali yao. Wale wapenda kandanda soma uone ni timu gani angalau zinahisiwa kushinda kombe la mabingwa.
Alafu inaaminika eti Waafrika tumelaaniwa:

Friday, October 06, 2006

Eti JK kadhihakiwa?

Kuna ile katuni ambayo serikali pamoja na wanahabari wa TZ wanadai ni dhihaka kwa JK na watanzania kwa ujumla.
Eti siasa Uganda ni ndege iliyo safarini, itafika. Alafu jisomee ujichekee vituko vya vigogo wa Uganda.

Wednesday, October 04, 2006

Leo

Kuna watu na mafanikio yao pamoja na malengo.Ili kupambana na ukimwi tunaambiwa eti jibu ni ABC je hili kweli?
Pia unapoona vichaa wengi siku hizi ni dalili za umasikini eti.

Sunday, September 10, 2006

LEO NI SIASA CONGO NA UGANDA

Mambo ya kupambana na rushwa sio mcezo, hapa kuna njia mbadala zinapendekezwa. Pia magari ya wabunge ni ulaji mtupu wa vigogo nchini Uganda, je umasikini utakwisha kweli? Hili la kushangaza manake inasemekana si Kabila wala Bemba anayestahili kugombea urais nchini Jamhuri ya kidmokrasia ya Congo. Si Congo tu ila eti hata Uganda sasa iko chini ya serikali ya maharamia, unajua?
Alafu kuna mtu kasema "Ushoga na Ufirauni" haukubaliki Afrika. Alafu soma ilivyo ngumu kuzuia uvunjaji wa haki za binadamu serikalini.

Thursday, September 07, 2006

KUHAMAHAMA VYAMA SIASA

Kwa wale wanasiasa uchwara ambao hawaishi kuhamahama vyama basi hii ya kule Uganda ndio funzo. Jamaa alikuwa mkuu wa majeshi lakini sasa ndie kati ya wapinzani wakuu na hana mpango wa kurejea chama tawala. Alafu sisi watanzania tunafikiri ni Mkapa tu kauza nchi yetu kule Uganda Museveni pia kagenisha na wazawa hawana chao.
Pia ona jinsi Maadili yalivyoshuka na kuathiri jammi za kiafrika.

Wednesday, August 30, 2006

SIKU YA GLOBU DUNIANI

Kesho ni siku ya blogu duniani. Nimerudi nyumbani Tanzania hivi karibuni na kwa sasa ninajaribu kutulia na kufuatilia hali huku nikijizatiti kutafuta kazi ya kufanya. Kazi ni shida sana kupata kama hauna baba au mjomba na akina shangazi serikalini au hata katika taasisi za binafsi. Lililopo mbele yangu ni kujiajiri mwenyewe nadhani niko sahihi.
Katika siku hii sina raha kabisa na ninaisikitikia Tanzania hasa katika sekta ya habari kwani hakuna majadiliano ya maana sana katika magazeti na redio zetu. Inaonekana ari mpya na nguvu mpya imeturudisha katika enzi za "Zidumu fikra za Mwenyekiti wa Chama cha........". Habari nyingi hapa ni kusifia utendaji wa wanasiasa na kutokuwakosoa kabisa.
Redio za FM kibao lakini wao dili ni kupiga mziki, vipindi vya majadiliano sio sana ila kama unataka ukweli kuhusu nchi hii soma globu. Tatizo ni watanzania wachache wanasoma globu.
Ziko globu tano ambazo nadhani ni bora kwangu na ningependa watu wasizikose kabisa: kwanza, ni hii ya Mpiga Picha Issa Michuzi ambapo tukio kuhusu Tanzania utalipata hata kama hauko nyumbani utafurahi sana na pia kwa kumbukumbu zote za nchi zipo. Pili ni Pambazuka kwani utapata habari kiuchambuzi na kiyakinifu kuhusu mauzauza yote ya wataanzania haswa wanasiasa na viongozi wake. Alafu kuna Miruko, yeye bwana anazungumza ukweli bila uficho, si mwoga kama walivyo watanzania wengi.Huyu si bendera fuata upepo.Blogu ya nne ni Kasri la Mwanazuoni, hapa huwa napata habari za upande ambao hutapata magazetini wala redioni.Huyu bwana ni kiboko huwa napenda nimsome tu. Mwisho kabisa ni globu kutoka Nigeria, hapa kuna mijadala ya kusisimua sana.

Monday, August 28, 2006

MWISHONI MWA WIKI ILIYOKWISHA

Ukisikia serikali inapinga ukweli alafu anatokea mtu anaandika kujibu mapigo ndio haya ya Uganda.Kwenye kandanda wakati hatuna mechi yeyote ya kujipima nguvu Uganda itacheza na wapinzani wetu Burkinafaso. Matokeo wametoka sare, nasikia Tanzania tulimtuma mtu akapeleleze, sijui itakuwaje jumamosi.
Kwenye siasa nako unajua kuna waafrika mawakala wa mabepari?Kama unamfahamu profesa Maamdani ambaye alimfunda pia raisi wetu JK basi soma anasemaje juu ya umuhimu wa elimu na vyuo vikuu katika nchi?Profesa mwingine, Ali Mazrui yeye ana mengi juu Jumuiya ya Afrika Mashariki, eti tunahitaji miaka mingine arobaini.Kuna haja ya Bunge la vyama vya upinzani kuwa na malengo au visheni, je Uganda wanalo bunge la aina hii?Si hayya tu, ila huu ung'ang'anizi wa Museveni madarakani una uhusiano sana na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia mapigano yamesimamishwa na waasi wa Uganda rasmi, je ni nani shujaa katika dhahama hili la miongo miwili?
Uchaguzi wa Congo DRC utatoa rais ambaye ana maslahi tofauti kwa Uganda awe Kabila au Bemba.
Huko Burundi kama kawaida jamaa wameanza kufungana jela eti watnataka kupinduana.Huku Jumuiya ya Afrika mashariki ikisuasua
Kama unataka kujua jinsi ya kuwa tajiri na kuishi raha mustarehe bila kukopakopa.
Mambo ya akina mama pia tunakumbushwa ni jinsi gani wanafurahia mabwana jua siri

Friday, August 25, 2006

FAMILIA YA MUSEVENI YAIFANYA NCHI MALI YAKE

Vituko vya marais wa Afrika ni vingi. Nchini Uganda, Museveni naye hakosi vituko hasa vya matumizi makubwa ya fedha.Andrew Mwenda anao uelewa wa ni nani hasa ni Museveni na jinsi familia ya rais huyo inavyoiibia nchi hiyo.
Imeripotiwa pia eti ili Kony aweze kumalizwa huko misitu ya Congo basi serikali ya Uganda iilipe Congo gharama ya uporaji iliyoufanya miaka kadhaa iliyopita.
Pia tunakumbushwa tusiogope ukosefu wa ajira kwani kuna namna ya kuishi bila kuajiriwa. Pia tunaambiwa kumbe hata maaskofu wa kikatoliki na makadinali wanastaafu.
Katika siasa, NRM kama mfano wa vyama tawala vinahitaji kitu kinaitwa Matangi ya Kufikiri--think tank. Pia nchini Uganda ni vizuri tumsome na kumjua afisa mmoja wa jeshi Brigedia Jenerali Tumukunde ambaye katiwa kizuizini kwa muda sasa eti kajaribu kutikisa mkuu wa dola.
Nirudi kwenye mazungumzo ya amani huko Uganda, kauwawa kamanda wa LRA ambaye inasemekana na aliyemjua kuwa alikuwa mnyama haswa. Pia nigusie mambo ya ofisini haswa tabia ya mahusiano ya kijinsia na mabosi.
Kwenye kandanda je kuna tofauti kati ya makocha wa Ulaya na wa kwetu hapa Bongo?Pia suala la nidhamu kwenye timu za kandanda kama Taifa Stars.

Friday, August 18, 2006

MAMBO YA MSINGI

Unajua umuhimu wa michezo mashuleni? Unajua inasemekana Museveni ndio anaimaliza kabisa Uganda?
Ni vizuri pia tuelewe ni kwanini Wazungu wameamua kutunyonya kabisa. Mazungumzo ya Doha yamevunjika, kwanini lakini?

YA WIKI HII

Kuna tabia ya kuhamahama kutoka upinzani kwenda chama tawala. Alafu nchini Uganda, Raisi pekee anatumia mamilioni ya shilingi kulipa washauri wake ambao ni wengi lukuki. Soma simulizi la mwandishi maarufu nchini Uganda alipokuwa lupango.
Nchini Uganda rushwa ndio haswa, je unajua wataalam wanaeleza rushwa ni nini? Je Raisi anaweza tu kuamua kufanya ziara binafsi?

Saturday, August 12, 2006

LEO

Kuna hili la ufisadi Uganda alafu eti siasa ni mbaya kwa maendeleo. Pia unamjua Kony alivyo sasa?Alafu ona jinsi matajiri wanavyoneemeka na elimu bora Ugaanda.
Yuko jamaa anatabiri Chelsea kushinda tena taji msimu huu.Na kwa wale kapera kama mie, tunahitaji wapanga sherehe za harusi?

Friday, August 04, 2006

YALIYONIVUTIA LEO

Wakati bado timu yetu haijaanza maandallizi ya kwenda huko Ghana mwaka 2008, Uganda tayari kocha waao kaanza mambo. Tunaambiwa hata sex inataka maadili fulani yazingatiwe, unazijua?
Kuhusu politiki ni kuwa Museveni kaishiwa hana hela, rushwa imezidi na sasa chama tawala kinabidi kifunge shughuli katika ngazi za chini. Athari za Chama dola ndio hizi. Nikiwa kama bachela mzoefu basi mambo ya mapishi ni vyema niyapitie.
Angalia ukubwa wa Afrika ulivyo, hapa rais anapopita anaweza akasababisha hata mauaji.Alafu ligi ya Uingereza ndio inakaribia.
Kama unamjua Joseph Kony pata undani wa maisha yake ya sasa. Je ilikuwaje Mapinduzi yakatokea Uganda?

Saturday, July 15, 2006

SALA KUONDOA RUSHWA?

Kweli sala na mafungo ndio dawa ya Rushwa?Pia mambo ya imani yapo kweli?Na siasa mwanzo wake je?
Mpira huu ni mwaka wa Chelsea tena?Je kashfa kubwa mpirani?

Friday, July 14, 2006

KONY ATAELEWEKA?

Mambo ya Kony?

UGANDA KUNASEMAJE?

Baada ya kimya kirefu leo niangaze yanayojiri nchini Uganda: kuna huyu bwana anatuhumiwa kuuwa mkewe. Katika kesi yake anaonekana kujiamini sana kitu kinachowashangaza wengi. Alafu kama ilivyo kawaida, siku hizi tunawaza pesa tu haswa wengi wetu. Matokeo yake hata kazi zetu kwa mfano wachapishaji wa magazeti maadili ya kazi yameshuka sana. Pia nchi ya Uganda inatamani kuwa na mafuta lakini inakumbushwa kuwa hiyo ni balaa kwa Afrika na ni hatari kwa demokrasia.
Baada ya kombe la dunia hebu tujue ni nini kinasemwa pia kuhusu kosa la Zidane? Alafu kuna Padri wa Kikatoliki uzalendo umemshinda na kaamua kuvunja sheriia za useja. Pia tunakumbushwa juu ya ongezeko la ugonjwa wa moyo. Nini kifanyike?
Mwisho vipi kuhusu Kony?

Thursday, June 08, 2006

VIROJA KATIKA VIAPO UGANDA

Hebu ona jinsi mawaziri wapya walivyoonesha manjonjo wakati wakiapishwa wiki iliyopita.Pia unaweza ukasoma uswahiba kati ya mmojawapo wa mawaziri walioteuliwa na Museveni hivi majuzi.

Wednesday, May 24, 2006

BARAZA LA MAWAZIRI LA MUSEVENI HILO!

Hatimaye Rais Museveni kachagua baraza la mawaziri na kama ilivyotarajiwa kamchagua mdogo wake ambaye ni ofisa wa jeshi aliyeishia kidato cha sita kuwa waziri wa fedha. Huko nyuma Museveni aliwahi kumtimua kazini kwa kisingizio cha ulevi kupindukia.
Mambo ya ufalme labda ndiyo yanaanza hebu tusubiri. Maajabu ni huyu Eliya Kategaya ambaye alimpinga sana juu ya kung'ang'ania madaraka sasa kawa waziri.
Yamesemwa mengi juu ya sababu za uteuzi wa mawaziri mbalimbali. Pia kama kawaida ya Uganda, uongozi umekwenda kwa watu wa mashariki, yaani kule alikozaliwa Museveni. Hata jamaa mmoja kadai eti anaota mji mkuu wa Uganda ukahamia "RWAKITURA" kijijini kwa Museveni siku chache zijazo.
Mawaziri ni wapya wengi na hasa vijana.

Monday, May 22, 2006

Thursday, May 18, 2006

MARAISI "SUPA GLUU"-AFRIKA

Kuna malalamishi ambayo yanafurahisha juu ya hatua ya marais wa Afrika kuunga mkono wenzao wanaong'ang'ania madaraka.
Mwandishi mmoja kalaani ni kwa nini hata JK wetu alihudhuria kuapishwa kwa Museveni?
Alafu Obasanjo alifika Uganda baada ya Museveni kuapishwa inasemekana alikuja kumfunza Museveni jinsi ya kutawala ukiwa haupendwi. Demokrasia bado inaendelea kuchezewa hapa na Museveni kwani sasa hivi yuko tayari kutumia hela za walipa kodi kumfunga mpinzani wake.

MARAISI "SUPA GLUU"-AFRIKA

Kuna malalamishi ambayo yanafurahisha juu ya hatua ya marais wa Afrika kuunga mkono wenzao wanaong'ang'ania madaraka.
Mwandishi mmoja kalaani ni kwa nini hata JK wetu alihudhuria kuapishwa kwa Museveni?
Alafu Obasanjo alifika Uganda baada ya Museveni kuapishwa inasemekana alikuja kumfunza Museveni jinsi ya kutawala ukiwa haupendwi. Demokrasia bado inaendelea kuchezewa hapa na Museveni kwani sasa hivi yuko tayari kutumia hela za walipa kodi kumfunga mpinzani wake.

Saturday, May 13, 2006

IGIZO LA KIAPO CHA MFALME MUSEVENI WA UGANDA

Kama ilivyotarajiwa jana Rais Kaguta Museveni aliapishwa na jaji mkuu kwa mara nyingine kuendelea na ngwe nyingine ya miaka mitano katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. Ametoa rai kwa vyama vya upinzani viwe makini ili kuweza kushirikiana naye.
Pia alipata wasaa wa kuelezea mipango ya baadaye na hata mafanikio aliyoyapata kwa miaka ishirini iliyopita.Katika sherehe za jana vyama vya upinzani hasa vile vyenye wafuasi wengi havikuhudhuria katika kile kinachoonekana kama kutomkubali Museveni kama rais halali. Pamoja na kung'ang'ania madaraka kwa Museveni lakini huwezi kuamini hadi leo ni miaka miwili Uganda ina mgao wa Umeme usiokwisha na watu wanaanza kumlalamikia sana.
Mwanzoni kabla ya kula kiapo ilisemekana hata rais Hu Jintao wa China angehudhuria katika kile kinachodaiwa kama mkakati mpya wa Museveni katika kujikita katika siasa za nchi za ukanmda wa maziwa makuu.

Sunday, May 07, 2006

J 2 YA LEO

Kama kawaida kila jumapili ninaangaza magazeti ya hapa Uganda na kwingineko. Kwa akina mama wajawazito ipo makala ya jinsi ya kujipendezesha. Alafu kuna hili la mameneja wa kiume kuongoza kwa kuwachukulia wafanyakazi wao kama wanawake.

Saturday, May 06, 2006

WAGOMBEA BINAFSI WAJA

Kwa mara nyingine mahakama nchini Tanzania imeruhusu wagombea binafsi. Huu ni ushindi wa demokrasia lakini sina hakika kama una mantiki yeyote ukizingatia demokrasia yetu changa.
Wengi wamefurahia ila ni lazima turuhusu muda tuone kwani hata nchini Uganda katika uchaguzi uliokwisha hivi majuzi pia wamechaguliwa wagombea binafsi.

Friday, May 05, 2006

HAKUNA MABADILIKO?

Kweli ukoloni unatumaliza au ni porojo tu?

UNAMJUA RAIS AJAYE WA UGANDA?

Huku Uganda ikiwa inasubiri kwa hamu kuapishwa kwa Rais wa Maisha, Yoweri Kaguta Museveni hapo wiki ijayo ni wazi mtu huyu hapendwi ila king'ang'anizi tu.
Naona ni hivyo kwani kwa sasa hadithi kubwa ni juu ya nani atamrithi Museveni atakapoamua kung'atuka. Wako wengi ila huyu waziri wa ulinzi ndiye anayeonekana atakuwa rais ajaye wa Uganda.
Si haya tu ya kumrithi ila inaonekana bado serikali ya Museveni inatumia kila mbinu hata zile chafu kabisa kumtia hatiani mpinzani wake Kiiza Besigye. Hapo jana serikali iliamua kumleta mahakamani mmoja wa makamanda wa jeshi la waasi wa LRA kuja kutoa ushahidi. Nakwambia hii inaonekana ni hatua ya ajabu kabisa. Kwani hapa hata serikali inatumia wauaji ili kumtia hatiani bwana Besigye. Mawakili hawakuwa tayari kuendelea na kesi na wanataka kwanza shahidi asimamishwe juu ya koti ili ajibu mashtaka ya mauaji na ugaidi. Hali hii inafanya wanazuoni kuhoji labda hii vita ya waasi wa LRA haishi kwani kuna mkono wa serikali. Kuwatumia waasi kutoa ushahidi mahakamani kunachukuliwa kama dhihirisho la kuwepo na uhusiano kati ya serikali na waasi kwa kiasi fulani. Mwenyewe Rais Museveni hivi karibuni kazungumza kinagaubaga juu ya mzozo huu wa miaka ishirini.
Ni wazi ingawa Museveni alishinda uchaguzi majuzi, kwasasa ana kazi kubwa kuunda serikali yenye mvuto. Sasa ameanza kuwashawishi baadhi ya wanasiasa waliokuwa naye wakati akipambana msituni ambao walimkimbia na wengine aliwafukuza pale, walipopinga kampeni yake maarufu kama "EKISANJA" ya kubadili katiba ili aendelee kuwa rais wa maisha, anataka wajiunge serikali mpya atakayounda baada ya kuapishwa wiki ijayo.
Familia nzima ya Museveni sasa imeamua kujikita kwenye siasa za nchi hii kiasi kwamba kuna kila dalili hapa ni mambo ya kurithishana yatafuata pale Museveni atakapokuwa amemaliza muda wake. Kwa mfano, hata mwanaye wa kiume Museveni, ambaye afisa wa jeshi la hapa sasa kaanza kuandika makala za kisiasa hasa akiunga mkono shirikisho la Afrika Mashariki, kitu ambacho kinapigiwa upatu sana na Museveni.

Sunday, April 30, 2006

SHERIA DHIDI YA WABAKAJI YAKWAMA-KENYA

Wiki iliyopita mbunge mmoja mwanamama aliamua kupeleka muswaada bungeni ili kudhibiti ubakaji nchini humo. Matokeo yake inaonekana kagonga mwamba manake wabunge wanaume wamekuja juu na inasemekana muswaada hautapitishwa kuwa sheria.
Mwanamama mmoja kasema hii ni sababu za umangimeza wa wanaume wa Afrika. Ila kuna sababu imetolewa ni kwanini Wabunge waliamua kuzichachamalia hoja mbalimbali ndani ya muswaada huo. Vifungu mbalimbali vya muswaada huo vilikuwa na utata. Mkwamo huu dhidi ya kuwaadhibu wabakaji kwa kiasi kikubwa unachangiwa na kutobadilika kwa jamii nyingi za kiafrika hususan nchini Kenya ambapo wengine wanaamini hawawezi kuishi bila kufuata mila zenye kukandamiza wanawake kwani mababu wa zamani watachukia.

URAFIKI WA TZ NA CHINA UMEFIFIA?

Mambo yamebadilika dunia ya leo. Sijui kama kuna umuhimu sana kwa Tanzania kutembelewa na kiongozi wa China ila niseme tu ziara ya rais Hu Jintao huko Nigeria na katika kituo chake cha mwisho nchini Kenya imenifanya niwaze vipi, kulikoni Tanzania.
Si tulikuwa washirika wakubwa sana wa China wakati wa Mwenyekiti Mao?Jibu nimelipata eti mwelekeo umebadilika duniani na China ya ujamaa sio hii ya leo. Zipo sababu kwanini China ni mshirika mzuri kwa nchi kama Kenya.
Kwa Wachina ziara ya hii Hu sehemu mbalimbali ni muhimu sana na hatuna haja ya kusikiliza kelele za Magharibi. Unajua kwa mfano sekta ya mafuta barani Afrika ambayo ilitawaliwa na magharibi sasa China nayo imeamua kuingia kwa nguvu hasa barani Afrika.

LEO MAGAZETINI

Leo kuna mambo ya lugha yameandikwa jinsi jamii ilivyogawanyika na kama mtu hauko makini unaweza shindwa muelewa mwenzako katika mazungumzo. Alafu Madaraka Nyerere anatukumbusha juu ya hii dhahama ya silaha za nyuklia kati ya Marekani na Iran na anasema kuwa na silaha hizi ni sababu ya kupunguza mizozo duniani. Mwanazuoni Ali Mazrui anatukumbusha jinsi ilivyo vigumu kwa nchi za Afrika kuungana. Ugomu ambao umejionesha pia katika muungano wa Tanzania ni dalili ya ugumu wa kuunganisha bara la Afrika ukiachilia mbali hii gumzo ya kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki ambapo mwandishi mmoja kaonya nini labda kifanyike ili kufikia mafanikio.
Hapa Uganda tatizo ni umeme hakuna na hakuna mtu anayejali. Ila inasemekana ziko sababu kwanini kwa waganda hili sio tatizo la kulalamikiwa. Si umeme tu ila Uganda ina mambo kwelikweli: kwa mfano, Uganda inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi za jumuiya ya Madola mwakani ambapo Malkia wa Uingereza atakuwa ndio mgeni mkubwa kabisa. La kushangaza kuna juhudi kubwa za baadhi ya Wapinzani za kupinga mkutano huo kufanyika hapa kabisa. Ila yuko Bibie mmoja kaandika labda ni nini kinagaubaga juu ya hili.
Mwisho ni hili la hiki kitabu Da Vince Code, mengi ya msingi yameandikwa juu ya ubishi ambao umegubika toleo hili. Pia tunaulizwa hivi ni kwanini tunasoma?

Friday, April 28, 2006

JOJI KICHAKA MAMBO MRAMA?

Leo nimesoma blog moja kutoka huko Amerika kwa Joji Kichaka. Kwa mfano hata hili shirika la ujasusi, CIA, mambo si shwari kwani Joji Kichaka kamfuta kazi bosi wa shirika hilo. Halafu hali ya mzozo wa silaha za nyuklia na Iran ndio inafanya mambo yawe magumu kwa Kichaka.

Tuesday, April 25, 2006

Ile sheria kandamizi-TAKRIMA-dhidi ya makabwera imefutiliwa mbali na mahakama ya katiba nchini Tanzania. Sijui watu kama Fredrick Sumaye na Andrew Chenge watakuwa na mawazo gani. Unajua nilifuatilia hotuba zao bungeni wakati wa kuundwa sheria hii nikachukizwa sana na maoni yao.
La msingi nimefurahi sana kwani angalau maana ya demokrasia inajionesha. Kuna utafiti nimefanya kuhusu hali ya kisiasa ya jimbo la Vunjo kule Moshi Tanzania ninatarajia kuuweka mtandaoni siku chache zijazo na pia nimejadili madhara ya sheria hii.

TFF NA SOKA LA TANZANIA USINGIZINI.

Wakati bado TFF haijampata kocha wa kuinoa timu ya Taifa-Taifa Stars-hapa Uganda viongozi wapya wa shirikisho la soka hapa Uganda-FUFA- tayari wamemleta mwalimu mpya wa timu hiyo kutoka Serbia. Kocha huyo ni Tomislav Sicic kutoka Serbia.
Viongozi wapya wa FUFA wameingia madarakani mapema mwaka huu tu na tayari wanafikiria juu ya safari ya timu hiyo ya Kombe la dunia na lile la Mataifa ya Africa.
Kama tunavyojua TFF walishaadiwa ushirikiano na Rais JK. Nataka tuwaulize hawa mabwana mbona wamelala? September si mbali wajameni. Nataka niangalie hii mikakati Tenga anayodai ipo je itafanikiwa?
Si soka tu ila Tanzania chini ya JK ni lazima ichukue hatua madhubuti ili kuendeleza michezo. Mimi ninaamini kama tutaendeleza michezo basi tutawainua vijana wengi ambao hawana ajira na hawatakaa waipate kutokana na fursa chache. Ninaunga mkono juhudi za serikali kufanikisha ziara ya timu ya ndondi wiki hii kwenda nchini Uhispania.
Hii ifanyike pia kwenye soka kwani ikiwa kombe la dunia litafanyika hapa Afrika hatuna budi tuanze leo kama wenzetu wa Uganda. Hainifurahishi kwa viongozi wa TFF kutuambia eti timu inakwenda Ushelisheli kwa mechi za kirafiki baada ya kualikwa huko. Pia eti Malawi imetualika kwa michezo ya kirafiki. Nasema hivi kwani inaonesha kwamba labda TFF hawana mipango madhubuti ila wanasubiri mialiko na kama isipokuja itakuwaje? Pia nataka nitoe rai ya makocha wazalendo hawakidhi haja ni muhimu tukawa na makocha kutoka Ulaya kwani tunahitaji mambo ambayo watanzania wenzangu hawana katika suala zima la kuiandaa timu ya Taifa. Kwa mfano, nina hakika kwa aina ya makocha tulionao nchini Tanzania si makini sana kwenye masuala ya kudhibiti wachezaji kinidhamu. Nidhamu ni msingi wa wachezaji kutekeleza wajibu wao na kama wachezaji wetu hawakai kambini na kufuata taratibu za kambi tusitarajie kufuzu kwenda Ghana au Afrika kusini 2010. Tayari hata katibu mkuu wa TFF, Tenga kakiri wachezaji wa Stars ni kama "chokaraa". Sijafurahishwa kabisa na hali ya sasa ambapo inabidi Tenga awakumbushe makocha akina Msola juu ya kutoa ruhusa. Hivi kweli tuna makocha wenye taaluma ya kutosha kuongoza timu ya Taifa? Jibu ni hatuna, hebu tujaribu kufuatilia timu kadhaa zitakapoanza kupiga kambi kwa ajili ya kombe la dunia kama utakuwa unasikia mchezaji kaomba ruhusa eti akachukue begi lake nyumbani kama wachezaji wetu wanavyofanya.
Alafu ni lazima tucheze na wapinzani wenye kutumia staili ya uchezaji kama ya wale tunaotarajia kukutana nao.Nionavyo mimi hii TFF bado ni kama FAT ya akina Rage na Ndolanga kwani bado sioni mabadiliko yenye kasi na ari mpya.

Sunday, April 23, 2006

RUBANI MLEVI--CHANZO CHA AJALI KENYA

Wajameni eti ile ajali ya ndege kule Kenya siku chache zilizopita ilisababishwa na ulevi wa rubani. Hii inaonesha ni jinsi gani sisi waafrika siku hizi hatujali nidhamu ya kazi. Inawezekanaje rubani mlevi aruhusiwe kupanda ndege?

HABARI ZA JUMAPILI YA LEO

Kila jumapili napata wasaa wa kupitia magazeti mbalimbali na kuangalia kuna nini cha maana. Leo nimeona mengi: moja, kuna hili la wabunge kupenda kulipwa mishahara mikubwa, mwandishi mmoja katuhusia kuwa hili ni janga kwa mataifa ya kiafrika kama Kenya. Nafikiri pia hata kwa Tanzania makala hii itakuwa ina maana.
Pili pia kutoka Kenya, mara baada ya ajali ya ndege ambayo iliyamaliza maisha ya wabunge kadhaa wiki mbili zilizopita, mara Rais Kibaki anatangaza siku maalum ya maombi kwa Taifa.Mwandishi anatuhabarisha zaidi kunani mpaka maombi kwenye mambo ya kiserikali? Alafu kama ulinifuatilia wiki iliyopita niligusia juu ya ile Injili mpya ya Yuda Iscariot, yule anayedaiwa kuwa alimuuza Yesu kristu kwa fedha.Mwandishi anatuambia hata mapadri wamebaki kimya juu ya hili kama kweli Yuda ni msaliti au shujaa.
Alafu lililonifurahisha kabisa ni hii ziara ya Rais wa China huko Marekani na hasa juu ya nishati ya Nuklia ambayo inasemekana China ni mshikadau anayepaswa kuzingatiwa. Nafikiri ukisoma makala hii ni muhimu; utaelewa haya mambo ya mashindano ya silaha hizi kwa undani.
Kuna pia hili la maraisi wa Afrika kutaka kugombea urais zaidi ya kipindi kilichowekewa ukomo ili kukaa madarakani mpaka kifo.Iko habari moja huko Marekani, jamaa wanajiuliza vipi tena hivi hata kama hujawahi kuwa Raisi pia kuna ukomo wa kugombea.Jamani simnajua watu kama akina Mrema na Lipumba na akina Maalim Seif wataendelea kugombea sijui mpaka lini.
Hapa Uganda, inasemekana vyama vya upinzani vimeshindwa kutekeleza yale ambayo vinapaswa kufanya. Hali hapa si tofauti sana na upinzani wa kule Tanzania.
Mwisho kabisa nimeshangazwa kiasi fulani eti vijana wengi wa Kimarekani hawana habari na mambo ya msingi ya serikali yao. Hii imenifanya nivute pumzi na kuangalia huku kwetu na kwa kiasi fulani hata kwetu Tanzania na hata hapa hali ni moja tu.

Sunday, April 16, 2006

NI PASAKA-ETI YUDA HAKUMSALITI YESU?

Nimepitia habari leo jumapili ya pasaka nikakunwa kuhifadhi haya: Moja Eti Yuda Eskarioti, yule mtume wa Yesu inasemekana ni shujaa na hakuna haja sisi waumini kumfikiria kama msaliti.bonyezahapa Eti inasemekana kuna injili ya Yuda ambayo kanisa limeikataa ambayo inaeleza kinagaubaga juu ya hili. Papa Benedict tayari ameikana ripoti iliyotolewa hivi karibuni juu ya injili ya Yuda. Nakwambia haya mambo mtu unaweza usiwe muumini wa dini yoyote. Sijui wanaglobu mnasemaje, mmeshafikiria hili? bonyeza hapa
Pia nikamsoma Papa Benedict-16 ana ujumbe gani leo hii. Ameushangaza umma kwa kubadilika kama kinyonga kinyume na alivyodhaniwa atakuwa Papa Ngangari.bonyeza
Pili, kuna huyu mtoto wa Mwalimu Nyerere, basi nikaamua nimsome nijue anaandika juu ya nini unajua inawezekana ana falsafa za baba yake. bonyezahapa
Alafu nikakunwa na umuhimu wa kuheshimu na kuilewa demokrasia, mwanamama mmoja kaandika kweli hapa Uganda. bonyeza

TUNAHITAJI SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI?

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeingia katika hatua ya kuwa shirikishio. Ili kujua ni nini kinatarajiwa kufanyika, bonyezahapa ili umsome mwanamama ambaye atatuletea shirikisho. Pia kuna machache aliyoyasema Katibu mkuu wa jumuiya Bw Mushega wakati akiaga ili kuhitimisha muhula wake. Amemponda sana Bw Njonjo, waziri wa zamani wa Kenya kwa kuiponda jumuiya.Hebu soma mahojiano kamili ya mwanadiplomasia huyo aliyemaliza muda wake.Pia kuna ripoti maalum ambayo itatolewa hivi karibuni juu ya kama kweli hii jumuiya inawezekana.Hapa nataka tusome taarifa tangulizi ya ripoti hiyo.
Mimi sio muungaji mkono sana Shirikisho ila tu jumuiya manake najua ni ndoto. Hata JK bado anaweka msisitizo zaidi kwenye SADC. Ila kwa baadhi ya wananchi wana wasiwasi juu ya hizi nchi za Rwanda na Burundi kwani zitatuletea balaa.

Friday, April 14, 2006

TANZANIA KUWA BORA KULIKO UGHAIBUNI--JK.

Unajua mara nyingi nikisoma anayosema JK kila anapopewa nafasi huwa ninacheka alafu ninajaribu kufikiri hivi kweli itawezekana?
Leo anaripotiwa eti ataondoa ile kasumba ya wasomi kukimbilia ughaibuni.somahapa
Haya hebu ngoja tuishi kwa matumaini manake huyu jamaa anafurahisha sana. Ila nimefurahishwa na makala moja hapa Uganda juu ya tatizo la utegemezi wetu waafrika huko ughaibuni.Nimeona ni vizuri tulinganishe yaliyojadiliwa hapa na hayo JK anayosema alafu tuamue je kweli JK ataweza kuboresha na kuzuia tamaa ya kwenda Ughaibuni?somahapa

Sunday, April 09, 2006

MTANZANIA KASHIKWA UGONI HOTELINI NA MWANABALOZI

Ni wiki moja sasa ambapo mwanadiplomasia mmoja wa Rwanda alizusha sekeseke kama sio kasheshe pale alipokamatwa ndani ya hoteli moja ya kitalii akijinjiri na mwanamama mmoja ambaye ni mke wa mtu. somahapa
Mengi yamesemwa ila pia kumekuwa na utata juu ya kukamatwa kwa mwanadiplomasia anavunja sheria za nchi ikimaanisha ni kuvunja mkataba wa Vienna.Ila hili limefanunuliwa vizuri na msomi mmoja hapa Uganda somahapa
Sina hakika kama ninavunja Azimio la Dodoma, ila napenda nieleze kushtushwa kwangu eti mwanamama huyo alikuwa ni Mtanzania.
La msingi nataka nitoe hoja na ijadiliwe: Hivi kuwa mwanabalozi ndio tiketi ya kufanya maovu? Eti ukifanikiwa kuhodhi au kumiliki kile kitambulisho cha uanadiplomasia basi ndio mwisho wa kubughudhiwa na wakora-mapolisi na wanausalama wengine?
Serikali ya Rwanda imelalamika sana juu ya kukamatwa mwanadiplomasia wao. Ila zaidi ni kwamba kuna hali tete sana katika tukio hili: Unajua kuna uadui mkubwa sana kati ya Museveni na Kagame na hali hii imepelekea mwanamama, ndugu yetu mtanzania mwenzetu kuhusishwa katika kuendeleza sokomoko kati ya wakubwa wawili hawa.
Unaambiwa udikteta wa Museveni sasa unaingilia starehe za watu bonyezahapa na kuzihusisha katika kuaibishana kati ya serikali hizi mbili. Mambo si mambo hapa. bonyeza hapa

MPASUKO WA KISIASA PEMBA

Nimesoma makala moja kwenye IPP Media ikanikuna sana. Unajua hii siasa ya Pemba watanzania wengi hatuifahamu kabisa. Ule MPASUKO wa kisiasa JK aliodai upo eti inasemekana hata yeye hajui kuuziba.
Kujua zaidi hebu soma makala hii: bonyeza
Zaidi ya hapo, mwandishi kaongeza makala yake katika sehemu ya pili akichambua zaidi hasa baada ya kiongozi wa chama pinzani, CUF, kufika pia Pemba na kumsifia JK. bonyezahapa
Lakini inafurahisha zaidi kwani JK kasifiwa na wasomi wa Bongo juu ya jinsi ambavyo analifuatilia suala la Muungano.

Sunday, April 02, 2006

JK SIKU 100

Eti rais Jakaya Kikwete kafikisha siku mia moja madarakani. bonyeza hapa Binafsi nafikiri anastahili pongezi.
Ila leo kanifurahisha zaidi katika kupambana na majambazi kwani kaanzisha kikosi maalum dhidi ya ujambazi; bonyezahapa ni hatua ya muhimu nainga mkono.
Ila tahadhari imetolewa leo hii juu ya utendaji mzima wa serikali ya JK kama inataka iendeleze mafanikio zaidi ya haya yaliyotokea kwa siku mia moja. somahapa

Sunday, March 19, 2006

HABARI ZA LEO MAGAZETINI

Katika pitiapitia yangu ya habari leo nimekunwa na jinsi wanaume wa siku hizi wanavyochagua wanawake wanaowapenda wawe wenza wao. Mwandishi kaandika kwelikweli na akaonya sana juu ya makosa tufanyayo sisi wanaume. somahapa . Kuna hili la haki za ukombozi wa wanawake: inasemekana wengine wamejisahau na wakavuka mipaka. soma
Habari nyingine ni kuwa eti dunia ya leo mambo ya elimu sio tena msingi wa kufanikiwa kimaisha. Ukisoma mwandishi wa makala ile ameniacha nikipigwa butwaa ni kwanini ninasoma sasa? bonyezahapa
Alafu ningependa tumsome raisi wa hapa Yoweri Museveni katika mahojiano yake ya kwanza tangu achaguliwe kuwa raisi hivi majuzi. bonyeza

Saturday, March 18, 2006

HISTORIA KUJIRUDIA KOMBE LA MABINGWA ULAYA?

Arsenal ndio timu pekee kutoka ligi kuu ya Uingereza iliyobakia katika ligi ya mabingwa Ulaya. Sikutarajia hili kabisa ila napenda niwasifu wapiga bunduki wa London kwa hili. Waingereza huwa wanasema ‘due credit’.
Hii siyomara ya kwanza Arsenal kufikia hatua hii ya robo fainali ila emeweka rekodi ya ulaya kuiondoa Real Madrid. Hii, kwa kuzingatia misingi ya kihistoria katika soka la Ulaya, Arsenal itafika fainali kama kweli historia hujirudia. Nimechambua historia ya mashindano haya inaonesha kila timu iliyoweza kuondoa Real Madrid ilifika fainali. Hebu tujitahidi kukumbuka Bayern Munich, AC Milan, Juventus na Monaco katika miaka kadhaa michache iliyopita.
Ushindi wa Benfica dhidi ya Liverpool ni historia nyingine katika soka la Ulaya. Sio tu ni timu ya kwanza kuiondoa Liverpool katika vikombe vya Ulaya bali pia ni timu ya kwanza barani Ulaya kuifunga Liverpool ugenini na nyumbani tangu mwaka 2001/ 2002. Hii inanifanya niamini kuwa timu yeyote yenye uwezo wa kuiondoa Man United na Liverpool katika mashindano ni bora kufikia fainali. Labda hapa niwakumbushe kuwa Bayer Leverkusen iliiondoa Liverpool mwaka 2001/ 2002 na ikatinga fainali. Porto chini ya mtaalam Mourinho iliiondoa Man United mwaka 2003/ 2004 na wakafika fainali na kushinda.
Hadi sasa Arsenal wana rekodi bora kabisa ya kufungwa magoli mawili tu na ni timu pekee pamoja na Barcelona hazijapoteza mchezo wowote. Timu imebadilika ikicheza kwa umoja na nidhamu ya mchezo katika kulinda na kushambulia.
Kwa upande wa Chelsea, iliaminika na wengi kwamba ingeondolewa tu. Barcelona ni timu yenye vipaji asili (natural) pamoja na ufundi wa hali ya juu. Ukizingatia timu ya Mourinho inayotegemea ufundi wa kisayansi—yaani mtizamo wa kibinadamu (artificial) niwazi njia za asili zingeshinda tu. Kushinda ligi ya mabingwa unahitaji wachezaji wenye vipaji vya asili ambavyo vituvizidi vile vya kufundishwa na walimu wa timu pinzani. Mourinho alikosa jibu la Lionel Messi na Ronaldino katika timu yake.
Liverpool haina wafungaji magoli na ndio maana ikatolewa. Unapopata nafasi nyingi za kufunga alafu hufungi magoli ninachoweza kusema ni kuwa timu ni mbovu. Magoli ndio kiashirio cha ushindi na wala sio chati ya vielelezo vya umilikaji au majaribio mangapi timu imefanya golini mwa timu pinzani.
Mwisho, Liverpool kuondolewa katika ligi ya mabingwa ni sheria wala sio jambo la kustaajabisha. Hakuna bingwa mtetezi aliyewahi kutetea kombe hili. Arsenal wanalihitaji kombe hili na inaonekana matumaini yapo. Kwani nina hakika Juventus watapata shida sana kuenda na kasi na ari ya Arsenal. Hebu tusubiri robo fainali tuone.

Thursday, March 16, 2006

MKAPAISIM--LEGASI YA AWAMU YA TATU

Mimi ni mmoja wa watanzania wachache sana ambao wakati JK anaingia madarakani sikuwa namwamini kabisa. Unajua nimezaliwa nikakuwa nikiona wanasiasa wa CCM wakituongoza kwa migengwe ya kila aina. Ndio maana niliwahi kuandika JK Anatania tu. SOMA
Kama nilivyosema katika makala ile, kuwa JK anawafahamu walarushwa waliojikia mizizi ndani ya dola. Na nikahisi ataendeleza sera ya kulindana ya aliyemtanglia, mheshimiwa Mkapa. Nafurahi kusema kwa ninayoyaona sasa, JK kadhihirisha kuwa nilikosea. Kwa kiasi fulani ninaanza kuona Kasi Mpya. Na hii ni wazi kwangu ni juu ya suala la “Ujambazi”.
Ninasoma habari jinsi ambavyo serikali imewavalia njuga baadhi ya matajiri ambao wanalea majambazi nikafurahi sana. Imani yangu imeanza kumea kwani nataka niseme baadhi ya matajiri waliokamatwa ni watu ambao wamekuwa wakitawala tetesi kuwa ni majambazi tangu nikiwa mtoto nasoma shule ya msingi. Kwa hiyo mimi nimefurahishwa na hatua ya serikali.
Labda nimkumbushe kamanda Saidi Mwema kuwa tafadhali hakikisha dola inajua shughuli za wenye fedha wote. Kuna umuhimu wa serikali kujua baadhi ya wafanyabishara wanapata wapi mitaji mikubwa ya kuendeshea miradi yao feki. Utandawazi isiwe ndio mwanzo wa watu kuachiwa huru kujifanyia chochote watakacho. Nikumbushe pia hawa wafanyabiashara wanajihusisha na vigogo wa serikali; hivyo ni muhimu na vigogo kadhaa waanze kuhoiwa kama kweli tunataka kupambana na ujambazi kwa ari mpya na kasi mpya. Hii mambo ya kuhamisha baadhi ya maofisa polisi na kuwapeleka jijini makao makuu nataka niseme ni doa katika hii vita ya ujambazi. Yaani mtu anahamishwa eti kutoka mkoa unaosemekana ni kitovu cha ujambazi alafu anakwenda makao makuu? Kwa nini tusiwastaafishe watu kama hawa kwa manufaa ya umma? Hapa nimechanganyikiwa kabisa.
Katika gazeti la Nipashe toleo la tarehe 10/3 nilisoma eti kuna afisa wa polisi eti akaunti zake zimesimamishwa. Hakutajwa kwa jina na mimi naona nisimtaje ila walipoandika eti anatoka mikoa ya kaskazini hisia zangu zilinicheza. Unajua Tanzania watu wa kawaida wanaishi na kuzungumza tetesi nyingi sana. Ila tatizo ni kwamba hasa kipindi cha Mkapa alikuwa akipiga tetesi kabisa. Alikuwa anasisitiza eti wananchi walete ushahidi. Dhihirisho la jinsi ambavyo alivyokuwa anapenda kulea watendaji wake, wengi wao wakiwa wala rushwa na mafisadi wakubwa. Hii madhila ya jeshi la polisi ni dhihirisho la sera mbovu za uongozi mbovu wa awamu iliyopita.
Madhila ya ujambazi tunayoyaona leo ni matokeo ya sera: MKAPAISM—kuficha maovu, wala rushwa, mafisadi na kutochukua hatua dhidi ya maafisa wakubwa wa serikali pale walipokwenda mrama. Hii ilipelekea kwa mfano jeshi la polisi likafika mahali haliheshimu hata raia. Jeshi linaendeshwa kama mali ya mtu binafsi bwana. Nakumbuka kila mara ninapokuwa kule Moshi huwa nashangaa sana. Sina hakika kama ni watu wote wanashangaa kama mimi pale unapoona askari polisi wa usalama barabarani wanasimamisha vipanya navyo havisimami na unasikia kondakta akitumwa akawaone hawa mabwana. Huko nasikia huwa anapeleka noti ya shilingi 1500 au 2000. Huwa nabaki kujiuliza je hawa ni wafanyakazi wa umma au wakusanya ushuru? Kama unataka kuyaona haya nenda karibu na kituo cha mabasi Moshi Mjini sehemu inaitwa BORA, kuna nguzo ya umeme na utakuta askari kasimama pale mida ya asubuhi.
Hapa kamanda Saidi Mwema atajiju kwani jeshi letu la polisi lilikuwa likiendeshwa bila maadili, kizamani na kila aina ya michezo michafu. Mwisho, niulize: polisi imewatia kizuizini matajiri kadhaa lakini nikumbushe kitu kimoja: wataalam wa sosholojia wanasema wanawake pia wanajihusisha sana na uhalifu. Mbona hamjawatia lupango Wabejing? Wanalea majambazi sana pia.
Pamoja na kumkandia Mkapa na "Mkapaism yake" nafikiri ni bora pia tujue anaendeleaje na mapumziko yake. Hebu bonyeza hapa uone.

Sunday, March 12, 2006

USHOGA KUKUBALIKA KAMA DESTURI HIVI KARIBUNI

Nimekutana na makala moja ambayo imenikuna sana juu ya ushoga.
Ama kweli hivi majuzi katika nishani za Oskar kule kwa Joji Kichaka, walifikia mahali na kuitunza filamu ya ushoga.
Kwa kweli nina wasiwasi sasa si muda mrefu 'Ushoga utakuwa sio dhambi'. Jamani mimi nimechanganyikiwa manake sasa wazungu wanatuwekea viwango kwenye kila kitu. Na wakishapitisha kwamba kitu fulani ni bora ndio hivyo tena sisi makabwela tunaona ni fasheni. Bonyeza hapa uone yuko mzungu mmoja hapa Uganda ana maoni fulani.

NCHI INAPOMILIKISHWA KWA MTU BINAFSI

Ama kweli kuna viongozi wanaopenda kumiliki nchi kama mali yao. soma hapa

Tuesday, March 07, 2006

MAMBO YA LUGHA NA FRED MACHA

Makala ya Fred Macha imenikosha na nimeona niifadhi ili tuisome na tujikumbushe umuhimu wa kulea lugha yetu. soma

UGANDA BAADA YA UCHAGUZI

Kama kawaida hapa Uganda mambo ya siasa yanaendelea kuchacha. Museveni kashinda uchaguzi kwa mbinde. Leo mahakama kuu imetoa hukumu soma dhidi ya Dk Besyige kuwa hana hatia ya ubakaji. soma
Ni aibu kwa Museveni tena lakini yeye anaendelea kujitapa katika makala aliyoiandika mwenyewe leo magazetini hapa soma. Pia leo imeandikwa makala juu ya udhalimu wa serikali ya Museveni kutumia jeshi kwa manufaa yake binafsi na kuvunja katiba. Hebu soma uone udikteta ulivyokomaa.
Ni wazi majaji wa hapa wako makini kwani serikali inapoteza kila kesi si kawaida lakini ndio hali halisi bonyeza

Monday, February 27, 2006

UCHAGUZI SAFI KWA VIWANGO VYA KIAFRIKA

Leo nimeona niwape habari za ushindi wa Museveni. Niseme tu kwa nilivyouona uchaguzi huu hakuna tofauti na chaguzi za Tanzania au Kenya.
Wapinzani wanalalamika lakini ndio kawaida yetu tumezoea. Sikutarajia Uganda inaweza kufanya uchaguzi kwa ustaarabu niliouona.
Dosari ni kule Museveni kubadili katiba; ila ameonesha alishawasoma watu na akagundua asilimia 59 wanampenda. Sasa kashinda ila swali ni: Demokrasia ni nini kweli? Je ni ipi demokrasia ya kweli ya Magharibi au ya kifalme kama hii ya Museveni? Wananchi wa hapa wametoa jibu hebu soma matokeo kamili hapa
Basi hebu tuangalie mambo yatakuwaje?

Saturday, February 25, 2006

KANDANDA LEO

Siku nyingi sijaandika juu ya soka.Kama baadhi yenu mnavyojua mimi ni mnazi wa Liverpool. Wiki hii tulipoteza mechi dhidi ya Benfica ila nina matumaini tutashinda mechi ijayo.
Leo nataka nizungumzie juu ya Manchester United kwani leo ndio wanamaliza msimu.Huwezi kuamini siku hizi ni faraja kwa Manchester kushindani kwa nguvu vikombe vidogo kama hili la leo la Carling.Siku za nnyuma Ferguson alikuwa akidharau mashindano haya ila leo hii ni shida hata kushinda kikombe hiki.
Klabu hii imeporomoka kwa kila kitu: kocha mzee, wachezaji dhaifu na wasio na ujuzi wa kutosha.Rooney na Ronaldo walisemekana kama kizazi cha baadaye.Inavyoonekana sivyo kwani hata sifa ya kuwa kiongozi hawana. Mara nyingi utawaona wakishindwa hata kujidhibiti wenyewe.Sasa ligi ya Uingereza ni ya Liverpool na Chelsea kama klabu imara.
Arsenal pamoja na kuifunga Real Madrid wiki hii naweza kusema sio klabu imara. Real Madrid wajinga kweli. Huwezi cheza na Arsenal alafu ukawaruhusu wacheze katika kiungo. Ni hatari sana na ndio maana walifungwa. Niionavyo Arsenal haiwezi kufurukuta kwa timu kama Chelsea au Liverpool.
Nitoe ushauri kwa Ferguson astaafu na pia klabu isainishe wachezaji wapya.
Mwisho kuhusu Tanzania, kama mjuavyo, wiki hii nchi yetu ilipangwa katika makundi ya michuano ijayo ya kandanda ya Afrika. Senegal, Burkinafaso sio mchezo kabisa,sidhani kama tutafika mahali.Kwa ufupi tusahau fainali hizi manake bado sijaona program yeyote ya vijana chini ya TFF.Hatuwezi kushinda katika mazingira kama hayo.

UHURU WA HABARI KAPUNI?

Mwezi wa kwanza, tarehe ya 16 niliandika makala juu ya jinsi gani uchaguzi mkuu kule Moshi ulivyoendeshwa.
Nilijaribu kugusia juu ya hisia mbalimbali za watu mara baada ya uchaguzi ule na nikaonesha ni jinsi gani kwa kiasi fulani demokrasia ilifanyiwa mchezo mchafu.
Nilisisitiza kwamba ilikuwa ni hisia zaidi za watu.Nahisi jamaa kadhaa hawakufurahishwa na makala ile.Kwani nadhani wameamua kuizuia makala hiyo isisomeke kabisa.
Nawaomba radhi wanaglobu ila niseme tunalo tatizo la uhuru wa habari katika nchi yetu.Siku za usoni nitaandika ni kwanini hali iko hivyo hasa nikijaribu kufananisha na kile kinachotokea hapa.

Thursday, February 23, 2006

UCHAGUZI UGANDA LEO

Kwanza kabisa niwaombe radhi kwa kupotea kwa muda mrefu. Unajua tena mihangaiko ya maisha. Tatizo kubwa hapa Uganda ni umeme kwani kuna mgao wa umeme hatari sana. Huwezi kuamini hapa tunapata umeme kila baada ya masaa ishirini na nne.
Kwa hali hii mara nyingi mchana huwezi pata mahali pa kufanyia kazi kwa kutumia umeme. Kwa wananchi wao ni kawaida kwani hii japo imesababishwa na uzembe wa viongozi wao wanaamini eti ni ukame tu.Hayo tuyaache kwani yanakera kweli pale ulafi na rushwa ya wanasiasa wetu zinapoua uchumi wa nchi alafu wanasingizia eti hali mbaya ya hewa.
Leo kutwa nzima nimekuwa nikipitia vituo mbalimbali vya kura hapa Jinja na kufuatilia yanayojiri huko Kampala. Kwa ufupi kura zimepigwa shwari na ni dhahiri bwana Besigye anaongoza mijini. Ngoma imebaki huko vijijini kwani Yoweri ndio ngome yake.
Watu wanafurahi dikteta atashindwa ila mimi siamini manake ni vigumu. Hebu tusubiri tuone.

Thursday, February 02, 2006

KWANINI MUSEVENI NDIO PEKEE KINARA?

Haya tena sasa ni mwezi ambao nchi ya Uganda itafanya uchaguzi wake mkuu.
Baada ya kukaa kimya kwa kipindi nikiwajulisheni siasa za hapa leo narejea tena. Kama inavyoeleweka na wengi ugombea wa rais ambaye alitarajiwa kumaliza muda wake umekuwa na utata sana hasa baada ya kubadili katiba kidemokrasia kupitia wabunge kuondoa ukomo wa vipindi vya kukaa madarakani.
Leo Rais Museveni kaandika makala maalum somahapa kuelezea ni kwa nini wananchi wanamkubali na kuwa ilikuwa ni sahihi kubakia madarakani.

Monday, January 30, 2006

JK ANATANIA TU.

Nakumbuka mzee kifimbo alipong’atuka mwaka 1985, nchi yetu ilikuwa hoi kiuchumi. Mzee Ruksa alikuja kama mkombozi. Wakati huo nasoma shule ya msingi, basi redio Tanzania ilizoea kucheza nyimo kuonesha mwelekeo mpya; nakumbuka kibao kimoja: ‘Usiopowajibika Ole Wako, Utakumbwa na Fagio la Chuma’. Pia kulikuwepo tangazo katika redio kila mara redioni eti: Mdudu rushwa ni hatari na anapiga na anaua’.

Hii yote ilikuwa kuonesha eti Mzee Ruksa kaja na ari mpya dhidi ya rushwa. Matokeo yake utawala wake uliikumbatia rushwa hadi mzee Kifimbo kumkemea kiana wakati Fulani pale Kilimanjaro Hoteli.Baadaye akaja Mkapa na kauli mbiu ilikuwa ‘Uwazi na Ukweli’. Kinyume chake huyu bwana hakupenda uwazi kabisa; ukweli ndio usiseme, waandishi wa habari watakuwa mashahidi hapa.

Sasa kaja Kikwete na kauli mbiu—Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya. Hisia zangu zinaniambia hivi: Kuna hatari haya majigambo tu. Katika uteuzi wake anaonekana kuja na sura mpya nyingi tu. Hii ni habari njema isipokuwa utendaji wao sidhani kama utafanikiwa.

Hii ni kwasababu raisi anapaswa, nafikiri analijua hili kwamba CCM imejaa wala rushwa wakuu nchi hii. Vyombo vya dola, mfano jeshi la polisi limejaa wala rushwa na huu ni utamaduni ndani ya chombo hiki inavyoonekana.

Nilipokuwa natizama hotuba ya JK ya ufunguzi wa bunge niligundua mambo mengi. Wapo wabunge kadhaa walionesha sura za woga na chuki dhidi ya maneno ya raisi. Wengi wa wabunge wazee pamoja na wabunge wanawake kadhaa walionekana kuogopeshwa na hotuba ile.

Kwa mtu yeyote aliyezoea kuishi kiujanjaujanja aliogopa sana. Nani asiyejua wabunge wengi wanalitumia bunge kama tanuri ya utajiri? Nani asiyejua wabunge wengi ni vihiyo ambao hata hawafahamu nchi yao kwa dhati. Mheshimiwa JK anaongea kama vile hajui wapo wazee, vigogo ambao hawashikiki nchini mwetu (untouchable) wamejazana bungeni ili kulinda maslahi yao. Hawa ni kikwazo kwa Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya.

Mwisho niseme tu ninamuunga mkono mheshimiwa JK, ila nina hakika itakuwa vigumu kwake kuleta mabadiliko tunayoyatarajia. Kutamba kwa majambazi ni kielelezo cha kwanza. Ila itabidi raisi awe mkweli tu kuwaridhisha watanzania. Kama waswahili walivyonena: “Bahari haiishi Zinge” nami ninene: JK anatania tu.

Monday, January 16, 2006

UCHAGUZI NA ODA KUTOKA JUU NANI ATANGAZWE MSHINDI

Hili nataka nilieleze kama nilivyolipata kupitia tetesi zilizozagaa mitaani pale Moshi mjini baada ya uchaguzi wa ubunge ambapo mgombea wa Chadema, Mzee Ndesamburo alimshinda yule wa CCM, Mama Elizabeth Minde. Nitaeleza mara baada ya kuweka wazi wasiwasi wangu juu ya hali ya usalama pale Moshi.

Kwa kipindi cha wiki tatu nikiwa Moshi mjini nilishuhudia hali ambayo kwangu ilinitia wasiwasi sana. Eti siku hizi ujambazi umeongezeka sana Tanzania hasa Moshi na utawala umeamua kwamba askari polisi lazima wapite mitaani wakiwa na silaha kuhakikisha usalama. Kwa kweli mitaa imejaa askari ila katika hali ya kunishangaza sikujiona salama kabisa. Niwachekeshe: katika matembezi yangu nilikutana na kijana, charafu, hajachana nywele, amevaa suruali ya jeanse chafu sana ambayo imechanwa sehemu mbalimbali na amebeba bunduki( short gun). Nusura nianguke manake nikajua huyu ni jambazi bahati nzuri watu wengine wakaniambia ni askari yuko kazini.

Nililoliona hapa ni kwamba tofauti ya jambazi na askari haionekani manake usalama unakuwa haupo, raia hawezi kumjua askari ni yupi.Nidhamu ya askari haipo kabisa hili nitalizungumzia siku nyingine kwani nina mifano mingi tu.

Basi nieleze juu ya uchaguzi pale jimbo la Moshi manispaa hasa kuhusu tetesi ambazo kama waswahili walisema: “lisemwalo lipo na kama halipo…….”.Mwaka jana mara baada ya CCM kuteua wagombea wake wa ubunge nilieleza uvumi uliokuwa umezagaa kule Moshi. Mgombea wa chama hicho, Mama Minde, ni wazi alikuwa ni chaguo bovu kwa wapiga kura.

Nilikuwa Moshi wakati ule na nikasema hatashinda huyu mama. Na kweli imekuwa hivyo; ila nilipokuwa huko hivi karibuni nilikusanya tetesi zingine ambazo nafikiri ni vizuri wanablogu mnisaidie kuchambua.

Ni hivi: uchaguzi wa Tanzania uliokwisha hivi karibuni umesifiwa sana na wanahabari na hata waangalizi mbalimbali. Kwa wapinzani umekuwa ni bumbuwazi kubwa sana. Ila kwangu naomba nijibiwe hili:

Kwa mfano, pale Moshi manispaa, inasemekana msimamizi wa uchaguzi, mkurugenzi wa manispaa, alichelewa sana kutangaza matokeo mara baada ya hesabu kukamilika. Eti ilimbidi afanye mawasiliano na wakubwa ili aruhusiwe kuyatangaza. Habari aisizothititishwa ni kwamba ilikuwa ni janja ya kumtangaza mgombea wa CCM kama mshindi. Ila hapa ilishindikana kabisa. Wigo wa kura ulikuwa mkubwa sana na inasemekana hata hizo alizopata mwanamama sizo zilizotangazwa kuondoa aibu. Je huu ndio uchaguzi ulio huru na haki?

Inasikitisha sana hizi sera za Mao hazifai kabisa.

KUTOKA TANZANIA HADI UGANDA

Mara ya mwisho niliaga kwamba sitakuwepo ulingoni mwaka jana. Nilikwenda mapumzikoni kule kwetu Moshi. Niliondoka hapa Uganda nikiacha hali ya kisiasa ikiwa ya vurugu, vitisho na udikteta ukiashiria kila hali ya zari kama sio dhahama ama kasheshe. Nimerudi hapa Uganda; ni wiki moja imekwisha sasa na hali imebadilika haswa kinume na nilivyokuwa nimetabiri kwamba hatima ya Besigye kisiasa. Nitaeleza baadaye.

Niwapashe wanaglobu wenzangu ni nini nilikikuta huko Moshi, uchagani katika wilaya ya Moshi Vijijini, jimbo la uchaguzi la Vunjo. Nilifika tu na Raisi mpya akatangazwa. Hii haikuwa tashwishwi kwangu kufuatilia kwani dhahiri nilijua JK angeshinda. Ila uchaguzi wa ubunge ulinikuna sana.

Baada ya miaka kumi ya utawala wa mbunge wa chama cha upinzani hatimaye jimbo langu la Vunjo likamchagua mbunge kutoka CCM kwa mara ya kwanza tangu siasa za vyama kurejeshwa. Hili lilinifurahisha kwani hawa jamaa wa upinzani wameirudisha Vunjo nyuma sana. Nasema hivi kwani katika eneo ninaloishi, kijiji cha Uparo, Kirua Vunjo, palw maeneo ya Kawawa Road ni dhihirisho tosha.

Nyumbani pale hakuna maji ya bomba tangu uhuru saa. Umeme ndio usiseme hakuna kabisa. Barabara ya kwenda Kirua Vunjo haifai kabisa; ikinyesha mvua inabidi magari yasubiri jua litoke ili pakauke ndio watu waweze kusafiri. Kuhusu mambo ya elimu ndio usiseme: eneo la Kawawa Road kwa mfano halina shule ya sekondari wala msingi na lina makaazi ya watu wasiopungua elfu tano. Watoto inawabidi kutembea kwa miguu zaidi ya kilomita saba kwenda shule kama za Pakula Sekondari, Mashingia na Uchira Sekondari. Hii ni hatari sana sasa tuone hawa CCM watafanya nini.

Niliposikia Kikwete na ari yake mpya, nguvu mpya na kasi mpya sikumwelewa sana ila nampa matarajio kama mkazi wa Kawawa Road kwani tumempa mbunge labda matatizo yetu yatapungua. Nafikiri mheshimiwa mbunge anajua hili.

Sasa niwarejeshe hapa Uganda: Mnakumbuka Museveni aliamua kumweka jela mpinzani wake mkuu Dr. Kiiza Besigye. Chama cha Besyigye kikaweka ukinzani wa hali ya juu. Nakwambea imesaidia sana , hali ya siasa ya Uganda kwa sasa ni shwari hata mimi nashangaa. Besigye yuko nje kwa dhamana ila kampeni in kama kawa. Vitisho dhidi ya fyombo vya habari na wapinzani vimekomeshwa; wale wanajeshi waliozoeleka kujazana mitaani hawapo tena.

Museveni kabadilika sana; uchaguzi utakuwa shwari kama hali itaendelea hivi. Nitaendelea kuwapasha zaidi ila tu Besigye anatuhumiwa kubaka na kesi inaendelea na imejaa vituko kwelikweli.