My Blog List

Sunday, April 09, 2006

MTANZANIA KASHIKWA UGONI HOTELINI NA MWANABALOZI

Ni wiki moja sasa ambapo mwanadiplomasia mmoja wa Rwanda alizusha sekeseke kama sio kasheshe pale alipokamatwa ndani ya hoteli moja ya kitalii akijinjiri na mwanamama mmoja ambaye ni mke wa mtu. somahapa
Mengi yamesemwa ila pia kumekuwa na utata juu ya kukamatwa kwa mwanadiplomasia anavunja sheria za nchi ikimaanisha ni kuvunja mkataba wa Vienna.Ila hili limefanunuliwa vizuri na msomi mmoja hapa Uganda somahapa
Sina hakika kama ninavunja Azimio la Dodoma, ila napenda nieleze kushtushwa kwangu eti mwanamama huyo alikuwa ni Mtanzania.
La msingi nataka nitoe hoja na ijadiliwe: Hivi kuwa mwanabalozi ndio tiketi ya kufanya maovu? Eti ukifanikiwa kuhodhi au kumiliki kile kitambulisho cha uanadiplomasia basi ndio mwisho wa kubughudhiwa na wakora-mapolisi na wanausalama wengine?
Serikali ya Rwanda imelalamika sana juu ya kukamatwa mwanadiplomasia wao. Ila zaidi ni kwamba kuna hali tete sana katika tukio hili: Unajua kuna uadui mkubwa sana kati ya Museveni na Kagame na hali hii imepelekea mwanamama, ndugu yetu mtanzania mwenzetu kuhusishwa katika kuendeleza sokomoko kati ya wakubwa wawili hawa.
Unaambiwa udikteta wa Museveni sasa unaingilia starehe za watu bonyezahapa na kuzihusisha katika kuaibishana kati ya serikali hizi mbili. Mambo si mambo hapa. bonyeza hapa

2 comments:

charahani said...

Innocent

Hujakosea kabisa kuweka haya wazi. Kwa maana kwamba hujakiuka azimio la Dodoma una uhakika
Huyu mwanadada ni Mtanzania na hapa ofisini kwetu ana kaka yake kabisa.

Baba yake yupo Mikocheni hapa Dar es Salaam. Suala ni kwamba mahusiano ya kidiplomasia kati ya Rwanda na Uganda ni yenye wasiwasi sana sasa mtu akitafuna mke wa mtu tu ndiyo inakuwa ishu kubwa sana. Simfagilii yule mwanabalozi lakini ishu imekuzwa mno.

rodgerz.blogspot.com said...

KAKA MABO VIPI???
KWANZA NAKUPONGEZA KWA "COMENTS ZAKO" NA PIA KAZI NZURI UNAYOFANYA KUWAELIMISHA WATU NA KUWAFANYA WAUJUE UOZO WA WATU NA VIONGOZI WAO WANAOWATEGEMEA ..
WAKIDHANI NI MASHUJAA KUMBE NI WASALITI....

see you bro...rodgerz.blogspot.com
i will ectivate the blog and concern your coments..
byeee