My Blog List

Sunday, April 16, 2006

NI PASAKA-ETI YUDA HAKUMSALITI YESU?

Nimepitia habari leo jumapili ya pasaka nikakunwa kuhifadhi haya: Moja Eti Yuda Eskarioti, yule mtume wa Yesu inasemekana ni shujaa na hakuna haja sisi waumini kumfikiria kama msaliti.bonyezahapa Eti inasemekana kuna injili ya Yuda ambayo kanisa limeikataa ambayo inaeleza kinagaubaga juu ya hili. Papa Benedict tayari ameikana ripoti iliyotolewa hivi karibuni juu ya injili ya Yuda. Nakwambia haya mambo mtu unaweza usiwe muumini wa dini yoyote. Sijui wanaglobu mnasemaje, mmeshafikiria hili? bonyeza hapa
Pia nikamsoma Papa Benedict-16 ana ujumbe gani leo hii. Ameushangaza umma kwa kubadilika kama kinyonga kinyume na alivyodhaniwa atakuwa Papa Ngangari.bonyeza
Pili, kuna huyu mtoto wa Mwalimu Nyerere, basi nikaamua nimsome nijue anaandika juu ya nini unajua inawezekana ana falsafa za baba yake. bonyezahapa
Alafu nikakunwa na umuhimu wa kuheshimu na kuilewa demokrasia, mwanamama mmoja kaandika kweli hapa Uganda. bonyeza

3 comments:

ndesanjo said...

Najaribu Inno kama umerekebisha suala la maoni kutokea kwenye blogu.

Indya Nkya said...

Kuna injili nyingi Inno ambazo zinasemekana ziliondolewa katika biblia kukidhi matakwa ya watu fulani. Kwa mfano kuna injili kama ya Maria Magdalena, Injili ya Philipo nakadhalika. Mimi kama Yuda alimsaliti Yesu sioni ajabu hata kidogo kwani si alifanya hivyo ili maandiko yatimie? Hilo lisingetokea basi andiki lisingetimia na hakuna andiko ambalo halitakiwi kutimia

Bwaya said...

Kaka nimekutembelea nyumbani kwako. Unatisha! Mambo yako ni makubwa. Karibu na kwangu nitafurahi.
Habari ya Yuda imenisisimua sana. Ninavyojua ni kwamba Yuda alikuwa shujaa sivyo kama tunavyomfikiria.
Aliamini kuwa Yesu asingeweza kukamatwa. Kwa sababu Wayahudi walijaribu mara kadhaa kumkamata lakini majaribio yote yaliishia patupu.
Kwa akili ya kawaida Yuda akajua kuwa hata akimsaliti hakuna lolote litakalotokea, hela atakula na wasimpate wala nini!
Kasheshe ikaja pale alipojua kuwa Yesu ndio kakamatwa kikwelikweliii tofauti na matarajio yake. Jambo la kufanya ni kujimaliza kwa staili ya mkwawa.
Yuda alikuwa shujaa asikudanganye mtu. Kwanza suala lenyewe lilishatabiriwa na Yesu mwenyewe. Ubavu wa kulikwepa ungetokea wapi?