My Blog List

Wednesday, May 24, 2006

BARAZA LA MAWAZIRI LA MUSEVENI HILO!

Hatimaye Rais Museveni kachagua baraza la mawaziri na kama ilivyotarajiwa kamchagua mdogo wake ambaye ni ofisa wa jeshi aliyeishia kidato cha sita kuwa waziri wa fedha. Huko nyuma Museveni aliwahi kumtimua kazini kwa kisingizio cha ulevi kupindukia.
Mambo ya ufalme labda ndiyo yanaanza hebu tusubiri. Maajabu ni huyu Eliya Kategaya ambaye alimpinga sana juu ya kung'ang'ania madaraka sasa kawa waziri.
Yamesemwa mengi juu ya sababu za uteuzi wa mawaziri mbalimbali. Pia kama kawaida ya Uganda, uongozi umekwenda kwa watu wa mashariki, yaani kule alikozaliwa Museveni. Hata jamaa mmoja kadai eti anaota mji mkuu wa Uganda ukahamia "RWAKITURA" kijijini kwa Museveni siku chache zijazo.
Mawaziri ni wapya wengi na hasa vijana.

1 comment:

Jeff Msangi said...

Inno,
Habari zako ni nzuri sana ila naona kuna tatizo katika viungo unavyoweka.Hebu jaribu kuliangalia hilo.