My Blog List

Saturday, July 28, 2012

OLYMPIC IMEANZA RASMI LONDON

Michezo ya Olimpiki imeanza na Tanzania kama kawaida imepeleka timu ya wachezaji sita (6) tu. Ni kiohoja lakini kama kawaida yetu ndo tulivyo yaani hatuna habari na kuwa serious ila tumebakia kila mtu anawaza kupata fedha tu bila kujali zinakujaje. Nasema hivi kwani nionavyo, sidhani kama tutaambulia kitu katika michezo hii; sanasana tunakwenda kutalii. Ninaguswa kwani nchi yetu ni masikini sana, ina vijana wengi wamejaa vijuweni hawana cha kufanya ila miongoni mwao wangeandaaliwa nadhani leo tungekuwa na angalau timu ya watu kama mia moja hivi na kwa hakika tungekuwa na uhakika wa medali angalau hata moja. Napendekeza tubadilike, leo naangazia mchezo wa ndondi, je bondia wa Tanzania atafanyaje? Leo anacheza pambano la kwanza.