My Blog List

Monday, August 28, 2006

MWISHONI MWA WIKI ILIYOKWISHA

Ukisikia serikali inapinga ukweli alafu anatokea mtu anaandika kujibu mapigo ndio haya ya Uganda.Kwenye kandanda wakati hatuna mechi yeyote ya kujipima nguvu Uganda itacheza na wapinzani wetu Burkinafaso. Matokeo wametoka sare, nasikia Tanzania tulimtuma mtu akapeleleze, sijui itakuwaje jumamosi.
Kwenye siasa nako unajua kuna waafrika mawakala wa mabepari?Kama unamfahamu profesa Maamdani ambaye alimfunda pia raisi wetu JK basi soma anasemaje juu ya umuhimu wa elimu na vyuo vikuu katika nchi?Profesa mwingine, Ali Mazrui yeye ana mengi juu Jumuiya ya Afrika Mashariki, eti tunahitaji miaka mingine arobaini.Kuna haja ya Bunge la vyama vya upinzani kuwa na malengo au visheni, je Uganda wanalo bunge la aina hii?Si hayya tu, ila huu ung'ang'anizi wa Museveni madarakani una uhusiano sana na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pia mapigano yamesimamishwa na waasi wa Uganda rasmi, je ni nani shujaa katika dhahama hili la miongo miwili?
Uchaguzi wa Congo DRC utatoa rais ambaye ana maslahi tofauti kwa Uganda awe Kabila au Bemba.
Huko Burundi kama kawaida jamaa wameanza kufungana jela eti watnataka kupinduana.Huku Jumuiya ya Afrika mashariki ikisuasua
Kama unataka kujua jinsi ya kuwa tajiri na kuishi raha mustarehe bila kukopakopa.
Mambo ya akina mama pia tunakumbushwa ni jinsi gani wanafurahia mabwana jua siri

1 comment:

Jeff Msangi said...

Inno,
Nimependa sana mahojiano ya Prof.Maamdani.Namuheshimu sana huyu bwana na nadhani anachokiongelea hapo ni kweli kabisa.Nimekishuhudia kwa macho yangu nilipokuwa hapo chuoni Makerere miaka kadhaa iliyopita.