Kama ilivyotarajiwa jana Rais Kaguta Museveni aliapishwa na jaji mkuu kwa mara nyingine kuendelea na ngwe nyingine ya miaka mitano katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. Ametoa rai kwa vyama vya upinzani viwe makini ili kuweza kushirikiana naye.
Pia alipata wasaa wa kuelezea mipango ya baadaye na hata mafanikio aliyoyapata kwa miaka ishirini iliyopita.Katika sherehe za jana vyama vya upinzani hasa vile vyenye wafuasi wengi havikuhudhuria katika kile kinachoonekana kama kutomkubali Museveni kama rais halali. Pamoja na kung'ang'ania madaraka kwa Museveni lakini huwezi kuamini hadi leo ni miaka miwili Uganda ina mgao wa Umeme usiokwisha na watu wanaanza kumlalamikia sana.
Mwanzoni kabla ya kula kiapo ilisemekana hata rais Hu Jintao wa China angehudhuria katika kile kinachodaiwa kama mkakati mpya wa Museveni katika kujikita katika siasa za nchi za ukanmda wa maziwa makuu.
1 comment:
Kaka Innocent,
Igizo hili hata sisi tumelishuhudia huku ingawa wakuu wetu wameonekana katika sherehe hiyo, naona ni usanii mtup, huyu mtu ana uroho wa madaraka ulioigeuza ikulu ya Uganda na serikali mali ya familia na analenga kwenye urais wa shirikisho la Afrika mashariki.
Heh balaa tulikuwa tukilaani hapa kwetu mgao uliodumu miezi miwili kumbe kwenu miaka miwili sasa poleni sana haya mambo magumu sana.
Post a Comment