My Blog List

Wednesday, December 06, 2006

KAGAME-MUNGU MTU- ASHTAKIWE TU

Naiangalia hali ya Rwanda kama ni tatizo ambalo waafrika hatuwezi kulitatua kwani kihistoria ni vigumu. Sina imani sana na mahakama ya Arusha kwani naiona kama mahakama iliyoundwa na washindi wa vita(RPF) ili kuwahukumu washindwa.
Ndipo hapa ninapokuwa ninamuunga mkono huyu jaji wa kifaransa kutaka pia Kagame ashtakiwe. Sidhani kuna suluhisho la kiafrika, ila naunga mkono juu ya nia ya mficho ya Ufaransa katika sakata hili. Pia nionavyo tutarajie Rwanda yenye matatizo sana hapo baadaye kwani Kagame inasemekana ni kiongozi Mungu mtu.Tatizo letu waafrika ni kutokupenda kusema ukweli na kama tutaendelea na uwongo huu wa Kagame hakuna maridhiano Rwanda.
Lakini pia ni lazima tujue pande zote mbili zilihusikaje katika kile kinachoitwa ukombozi wa Rwanda?Kwa mfano, picha halisi ya ushiriki wa Kagame na Habyarimana unaweza kuisoma na kupata hali halisi hasa hii makala ambayo mwandishi anao uelewa sana wa mambo ya Rwanda.

1 comment:

Anonymous said...

Sielewi kuna tatizo gani Kagame kushtakiwa. Kama hana hatia, hana hatia. Kushtakiwa sio kudhalilishwa. Kupinga kushtakiwa ndio kosa. Kama huna hatia hofu ya nini? Hakuna binadamu anayepaswa kuwa juu ya sheria za kimataifa, hasa zinazohusu mauaji ya halaiki. Awe rais, awe mfalme.