My Blog List

Thursday, August 16, 2012

KIPROTICH ALIKUWA NA DHAMIRA YA KUTWAA MEDALI OLIMPIKI

Dhamira ya kutwaa medali kwa mwanariadha wa Uganda Stephen Kiprotich yalikuwepo tangu alipoondooka nyumbani kwao Kijijini huko Kapchorwa. Alimuaga mke wake na kumtamkia kkuwa lazima arudi na medali. Dhamira yake inashuhudiwa na mke wake hapa.

UGANDA INAVYOMTHAMINI MSHINDI WA DHAHABU OLYMPIC

Stephen Kiprotich ndiye mshindi wa mbio za nyika (marathon) katika michezo ya Olimpiki ya London iliyokwisha jumapili iliyopita.
Rais Yoweri Museveni amewaongoza waganda kumpokea kijana huyu ambaye anatoka katika familia masikini ya kiafrika kule Kaskazini mwa Uganda eneo la Kapchorwa. Rais Museveni ameweza kuwaalika wazazi wa kijana huyu Ikulu hapo jana na waganda wamechanga fedha nyingi sana kumzawadia kijana huyu.
Kijana huyu ana mke na walikuwa wanaishi kijijini kabisa maisha ya kienyeji kabisa; na ndiye amekuwa akiibeba familia yake wazazi na ndugu zake.Siku ya jumatatu wiki hii kijana huyu aliwasili Kampala na amekuwa akilakiwa kila mahali alipokwenda, hii imejumuisha kukagua gwaride maalum uwanja wa ndege; na kutembelea Ikulu.
Kuonesha jinsi gani Waganda wanamjali mwanamichezo shujaa huyu, gazeti la serikali "New Vision" limeandaa utaratibu wa kumchangia kiasi cha dola za Marekani 500 Milioni kama zawadi kupitia wasomaji wake. Hadi naandika ilikuwa tayari kuna dola 375milioni. Mimi binafsi Kiprotich amenifurahisha sana na ninadhani ni funzo kwa watanzania vijana kibao ambao wamejazana mitaani eti hawana kazi.