My Blog List

Wednesday, September 07, 2005

WARIOBA NAYE MNAFIKI TU.

Yaani leo nimehuzunishwa sana na maneno ya Jaji Joseph Warioba. Eti anasema matajiri wameiteka siasa; yaani ina maana alikuwa hajui. Huyu nadhani mnafiki sasa; angetuambia amefanya nini yeye katika kipindi alipokuwa kiongozi kama sio pia kuwa ni kundi la matajiri hao?
Wanasiasa wa Afrika wanachosha sana. Huyu bwana baada ya kufaidi anajifanya anaona huruma. Kweli anatufanya watanzania ni wajinga. Hebu bofya hapa uone amesemaje juu ya mwelekeo wa siasa zetu. Mimi nafikiri ni kujaribu kujionesha mtu mzuri kumbe wapi.

1 comment:

Jeff Msangi said...

Innocent,kwanza hongera kwa blog nzuri na makini,nimeipenda sana.Mimi sio mtetezi wa wanasiasa kwa sababu naamini wanasiasa wote ni wabinafsi,waongo na takataka.Nazungumzia wanasiasa wote,wa dunia nzima.Ninapojaribu kupiga darubini yangu naona Warioba ana nafuu kidogo.Kama ulikuwa kipenzi cha Mwalimu Nyerere basi naweza kukuambia kwamba Warioba ni chembe chembe hai za wanasiasa angalau wenye nafuu.Unajua kwamba alichukua msimamo gani serikali ilipotaka kumuuzia nyumba ya serikali?Unakumbuka ripoti yake juu ya rushwa ambayo nchi nyingi duniani zimefaidika nayo isipokuwa Tanzania?Tumpe sifa zake kidogo jamani.Au siyo?