My Blog List

Monday, September 05, 2005

KOMBE LA DUNIA--WAWAKILISHI WAPYA MWAKANI?

Usiku wa jana nilifadhaika sana manake timu ya Cameroon iliifunga ile ya Ivory Coast bonyeza hapa na kuharibu kabisa ndoto ya akina Drogba, Dindane na Kollo Toure kucheza kombe la dunia hapo mwakani.
Timu ya Cameroon imeshiriki kombe hili mara nyingi lakini imekuwa ikinisikitisha sana na ndio maana nilitaka timu mpya ziwakilishe bara letu la Afrika.
Naomba Mungu asaidie Cameroon isiende; nafikiri tunahitaji changamoto mpya.Hebu tusubiri mechi za mwisho mwezi ujao.Hatari iliyopo pia nadhani Nigeria nao watakosa nafasi ya kushiriki mwaka huu. Ni dhahiri Angola, Togo na Ghana watakuwa wawakilishi wapya kabisa katika fainali hizo. Tusubiri tuone.

No comments: