My Blog List

Monday, September 05, 2005

MAWAZO YAKINIFU, YASIYOHITAJI UHARIRI KOKO WA KUZUIA HABARI: SIRI NI KUGLOBU TU.
Wakati Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi bado hatujaweza kuwapambanisha wagombea wa uraisi kwa hoja. Kuna fununu eti Kikwete hataki mdahalo japo mimi naona ni jambo zuri vyombo vya habari kulishughulikia kwa sasa hizi porojo za kampeni si pimajoto zuri kujua uwezo makini wa mgombea.
Je TV zetu nchini zinaliona jambo hili? Ujerumani inapoelekea kwenye uchaguzi jana iliandaa mdahalo mzito ambao uliwahusisha wagombea wawili wakuu: mwanamama Angella na Schroder minya hapa.Wananchi hawakubanduka kutoka runinga zao na wengi wanasema Schroder alimbwaga mwanamama huyo kwa hoja. Sijui inaashiria nini katika uchaguzi ila ni hatua nzuri ambayo inahitajika kwa watanzania pia.

No comments: