My Blog List

Tuesday, September 13, 2005

SUMMIT YA UMOJA WA MATAIFA-- POROJO TENA

Kuanzia kesho siku ya Jumatano, mjini New York kutakuwa na mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa ambao utajihusisha zaidi na mageuzi ya umoja huu.Maraisi wapatao mia moja themanini watakutana. Kwenye mkutano huu wa siku tatu, Umoja wa Mataifa unatarajiwa kupitisha malengo ya Milenya uliyojiwekea miaka mitano iliyopita. Zaidi ya hapo wahusika wanatarajia kupitisha mageuzi ya ndani ya umoja huu ili kwa mfano kuboresha kazi zinazofanywa na Umoja wa Mataifa kwenye upande wa kulinda amani na haki za binadamu. Lakini kwa mara nyingine tena Marekani imekuja na mapendekezo mapya ambayo inataka yazingatiwe kwenye maazimio ya mkutano huu.

Kwenye mkutano huu wa kilele wa Umoja wa mataifa, Marekani itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nchi za nje, Bi. Condoleeza Rice. Mwanasiasa huyu wa ngazi ya juu kwenye serikali ya Rais Bush tangu wiki iliyopita ameonyesha wazi utayarifu wa Marekani kuunga mkono mageuzi ya ndani ya Umoja wa Mataifa.

Lakini kwa mara nyingine tena Marekani ina mapendekezo yake ambayo ingependa sana yazingatiwe kwenye maazimio yatakayopitishwa kwenyse mkutano huu wa siku tatu mjini New York.

Tangu mwezi wa Agosti, balozi wa Marekani kwenye uMoja wa Mataifa amewasilisha maependekezo ya marekebisho 700 hivi. Kwa mfano Mfano kipengee kinachozungumzia malengo ya Millenya.

Itakumbukwa kuwa malengo haya yalipitishwa na nchi zote wanachama miaka mitano iliyopita. Miongoni mwa malengo yaliyopitishwa ni kupunguza umaskini duniani kote kwa asilimia 50. Serikali ya Bush inataka kuondoa mwanya wa kuendelea kuziwajibisha nchi za viwanda kutoa misaada mikubwa zaidi ya maendeleo, kama ilivyokuwa imenuiwa hapo awali. Badala yake Marekani inadai masoko ya kimataifa yanaweza kutoa mchango mkubwa zaidi, hususani mageuzi ya ndani katika nchi zinazoendelea. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleeza Rice akizungumzia uzizo wa biashara na masoko ya kimatafa alisema: “Tunataka kusisiziza uzito wa biashara duniani ili kuwanasua watu kutokana na umaskini. Baada ya kuongeza msaada tunaotoa kwa nchi zinazoendelea, tunataka sasa kuhakikisha sasa mifumo ya utawala inabadilishwa ili misaada tunayotoa itumiwe ipasavyo. Hapa tunamaanisha hususani utawala wa kisheria, mageuzi ya mfumo wa uchumi na vita dhidi ya ulaji rushwa”

Kwa mantiki hii hakuna tena uhakika kama kwenye azimio la mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kutakuwa na kipengee cha kuziwaibisha nchi tajiri za viwanda kutoa silimia 0.7 ya pato jumla la ndani kwa ajili ya misaada ya maendeleo. Lengo hili halijafikiwa na Marekani wala hakuna matarajio ya kulifikia hivi karibuni.

Kwa hiyo, msimamo huu wa Marekani unaweza kuzifanya nchi zinazoendelea nazo zikatae kupitisha mambo ambayo Marekani inaona ni muhimu. Kwa mfano vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa au marekebisho ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani alisema nchi yake inataka tume hii ifanyiwe marekebisho. Alisema: “Tume ya haki za binadamu inayotaka kuundwa lazima iwe na uwezo wa kutekeleza mambo na ifuate misingi tuliyojiwekea. Hatuwezi kuwa na tume ya haki za binadamu inayojumuisha nchi kama vile Sudani ambayo inatuhumiwa kwa mauaji ya wananchi”.

Upande mwingine ambao Marekani unataka ufanyiwe marekebisho ya kina ni kazi zinazofanywa na vikosi vya kulinda amani vya umoja wa Mataifa. Mageuzi ya Umoja wa Mataifa yanataka kuuwajibisha zaidi Umoja wa Mataifa, na ikiwezekana uwe na uwezo wa kuingilia kati katika nchi nyingine ili kulinda haki za binadamu na hivyo kuzuia mauaji ya halaiki kama yake yaliyotokea Rwanda. Marekani haifikiani na mageuzi haya, kwani italazimika kutoa majeshi yake kwa kazi za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa.

No comments: