My Blog List

Saturday, November 26, 2005

NITAKAMATWA SIKU YOYOTE KUANZIA LEO

Nataka niseme kwa sasa niko hatarini kukamatwa wakati wowote. Unajua kuanzia juzi serikali imepiga marufuku kuandika, kuzungumza juu ya Dr. Kiiza Besyige, mpinzani wa Museveni ambaye yuko lupango.Kama mnavyojua hapa kila kitu ni kijeshi tu kwa hiyo mkisikia nimetiwa korokoroni msishangae kabisa.
Lakini kabla hayo hayajanikumba labda niseme tu kwamba bado hali sio shwari. Jana Besyige kapewa dhamana bonyezahapa ila bado anabakia ndani ya lupango. Kujua zaidi hebu bonyezahapa. La kushangaza zaidi hapa polisi ndio hao hao wanajeshi na kuna wanajeshi wengi sana Kampala onahapa
Katika kuhakikisha uhuru wa kusema, kuandika na kutangaza unadhibitiwa, serikali imemteua mwanajeshi bonyeza kuongoza bodi ya gazeti la serikali-New Vision. Hii inatafsiriwa kama kuhakikisha hata gazeti la serikali linamchafua mpinzani yeyote na haliandiki habari njema kumhusu.
Kwa Museveni hii ndio demokrasia.

3 comments:

nyembo said...

HAPA LAZIMA NISEME! NI MUHIMU KUSEMA KWA NINI NISISEME,WA NDANI YA UGANDA NA SISI WA NJE TUTASEMA TU, HATA KAMA TUKIBANDIKWA GUNDI MIDOMONI TUTAFUTA NJIA NYINGINE YA KUSEMEA KWA NINI TUSISEME KAMA mUSEVENI HATAKI KUZUNGUMZA! MIMI NAMUONA SI MTWAWALA TENA NI MFALME BARADHULI! AKIWAKAMA WA HUKO WA HUKU TUTASEMA KUKAMATA SIO HOJA ILETAYO TIJA KWA SASA UGANDA.

Ndesanjo Macha said...

Inno,
Asante kwa vipande unavyotupa kuhusu si-hasa za Uganda. Makubwa yanatokea hapo. Hasa hili la kupiga marufuku vyombo vya habari kujadili masuala ya Besigye. Ningependa kujua kama kuna redio, vituo vya luninga, na magazeti yanayofuata haki ya kikatiba ya kujadili na kujieleza na sio matamko ya wa-twawala

Halafu kuna kiungo kimoja hapo juu hakifanyi kazi (kimekosewa) na kingine hakipo kabisa (pale unaposema "ona hapa.")

FOSEWERD Initiatives said...

mshenzi sana museveni. na anadhani kwa mwendo huo atakuwa raisi wa federation mwaka 2013 subutu....CV chafu kabisa! ningekuwepo dar alivyokuja kumuapisha kikwete ningempiga maganda ya ndizi!!endelea kutupa mavitu vitu!