My Blog List

Saturday, November 19, 2005

KITENDAWILI CHATEGULIWA

Rais Yoweri Kaguta Museveni hatimaye jana usiku alifanya yale yaliyokuwa yametawala vinywa vya wengi hapa Uganda kwa siku nyingi.Ametangaza rasmi kwamba atagombea urais soma tena baada ya kubadili katiba na kuruhusu agombee kwani alikuwa tayari katimiza vipindi viwili vya miaka 5.
Nilitaraji hili, ila nataka niulize hivi kweli kuna tatizo hata mtu akiitawala nchi yake kwa miaka 50?
Na kama watu, wanachama wa chama chako, tena chenye wafuasi wengi ndani ya nchi wakakusukuma ugombee, ni muhimu kweli kufuata utashi wako?
Hebu pitia makala moja soma hapa ambayo inazungumzia ni njia ipi Museveni ataifuata sasa alafu unaweza ukaelezea hisia zako.
Mimi ninabaki kumshangaa BEN MKAPA eti anaachia ofisi, mbona wenzake bado wamebaki?

1 comment:

Ndesanjo Macha said...

Sidhani kama kuna tatizo mtu kukaa madarakani miaka hata 200. Ila ukitaka kufanya hivyo usichukue cheo cha Urais. Jiite mfalume au malikia. Hapo tutakuacha.