My Blog List

Sunday, November 06, 2005

RAISI ANAYEPENDA UJIKO HUYU HAPA

Tunaelekea katika uchaguzi wa hapa Uganda mwaka ujao.Rais Museveni ni dhahiri atashinda, baada ya kufanikisha mradi wake wa kufuta katiba ili awe huru kugombea tena.
Huyu ni mtu mwenye jina haswa hapa Uganda, ingawa siku za karibuni amepoteza sifa na haiba miongoni mwa watu makini baada ya kuonesha dhahiri anapenda madaraka kuliko demokrasia. Sasa hivi ameanza wazi kampeni za kupita na kusalimia wananchi huku binyahapa akiendesha gari mwenyewe. Huwezi kuamini lakini ndio katika njia moja ya kuonesha ukaribu na wananchi.Wengine watasema anajikomba lakini ndio siasa.
Mimi sina maoni sana isipokuwa nilifurahi kuona rais anaendesha mwenyewe, sijawahi kuona kabisa.Nafikiri hii mambo ya kutembea kwa misafara ni utumwa fulani ndio maana nimevutwa na hili.

1 comment:

Ndesanjo Macha said...

Inno,
Hii ni kali kweli. Unajua wa-twawala wanapotaka kuonekana kuwa ni watu wa watu wanaweza hata kutembea pekupeku. Hizi ni geresha tu. Kala. Kaiba. Katesa. Kadanganya. Sasa anajifanya eti anaendesha gari mwenyewe. Tunaweza kutafsiri kuwa anavyoendesha gari mwenyewe ni sawa na anavyoendesha nchi mwenyewe na kubadili katiba kwa matakwa binafsi.