My Blog List

Saturday, November 19, 2005

EBO! MADAKTARI SI BORA KAMA WANASIASA.

Haya leo turejee Tanzania: somahapa kuna hii kasheshe ya madai ya posho za madaktari. Jamani mimi huwa nachanganyikiwa ninapoona daktari kasoma na akahitimu lakini hana mapato mazuri.
Ukipima kile wanachopata watawala wetu usiombe. Hasa wanasiasa, wabunge na madiwani ndio wanaopata pato kubwa sana. Naomba mniambie wenzangu na mie, hivi ni kwanini tuwalipe mamilioni ya shilingi wabunge alafu madaktari tuwakamue?
Tumekwisha.

2 comments:

mark msaki said...

bwana kessy,

inauma sana lakini! lakini tutafika! tunataka tufike wakati tuwe na nchi ambayo ili uishi vizuri si lazima uwe mwanasiasa! pia inabidi tufike mahali tusiwe na viongozi wa kulipwa - profession leaders bali viongozi waliopewa ridhaa na wananchi! mbona kuna nchi hazijali kama zina raisi au la?

mark msaki said...

mimi niko mbele kuwalaani hawa wanasiasa wenye mawazo mgando na kugeuza siasa kuwa kazi ya kulipwa yaani proffessional leaders!! hawajui ni nini kinaendelea huku uraiani. lakini ndo hao wameanza kupigwa chini! si umemuona mume wa yule mama steringi wa kutesa madaktari kapigwa chini bungeni? anatakiwa akakazane kusomea sheria mlimani angalau afungue practice pale dar! angekuwa ameenda shule kidogo angejua nini maana ya mtu mzima kusoma mwongo mmoja! na mifululizo ya kukosa usingizi wachilia mbali kupasua maiti! wao wanadai wengine wawe na wito wao aahhh!!