My Blog List

Thursday, November 17, 2005

UNG'ANG'ANIZI MPAKA KWA OBASANJO?

Baada ya maneno mengi hapa Uganda, ambayo yalipelekea watu kulalama eti Museveni anang'ang'ania madaraka kwa kubadilisha katiba hatimaye yametimia.
Museveni kachukua fomu somahapa za kuomba kugombea uraisi kwa tikiti ya chama tawala NRMO. Lakini kimefanyika kiroja kimoja cha kisiasa hapa. Wanachama wa chama hicho wameamua kujifanya wamemlazimisha agombee kwani hakuna mtu mwenye kile wanachokiita "visheni" ya kuongoza Uganda.
Ung'ang'anizi huu wa madaraka unanipa wasiwasi juu ya kuwaamini viongozi wanajeshi kwani hata leo asubuhi nimesikia eti hata Obasanjo naye yuko mbioni kubadili katiba.
Jamani naomba maoni yenu nini kifanyike?Manake hawa viongozi ving'ang'anizi wakipata mpinzani wanatuma askari mipakani na wanawakamata alafu wanaigiza eti ni waasi na wanawahusisha na uasi. Ndio yanayomkuta Besigye sasa hivi.

2 comments:

Indya Nkya said...

Inno cha kufanyika ni kujitahidi wapiga kura waelewe na kuwakataa pia tujifunze namna ya kuwaondoa hata kama wakiiba kura. Maandamano kama ya Ukraine Krugstan na mengineyo ni mifano mizuri. Tukishaweza kuwafanya watu wakawa na ujasiri wa kukuambia hapana ni lazima utaondoka tuu. Kingine ni kwamba watu wajue hakuna mapinduzi yasiyo na gharama zake.

Innocent said...

Kweli hapo ni pagumu kwa watu wetu.Hapa ni wachache wako tayari kwa hilo ila naona dalili.
Tuombe Mungu.