My Blog List

Monday, November 14, 2005

VURUGU ZA KISIASA ZATAWALA KAMPALA

Uganda ni vurugu tupu.Ule mradi wa rais Museveni tayari ameanza kuufanyia kazi.Ikitarajiwa wiki hii atajitangaza kama atagombea urais leo hii serikali ya hapa imemkamata na kumshtaki Kiiza Besigye kwa kujihusisha kwake na uasi.
Nakwambia ghasia zililikumba jiji zima la Kampala leo hii.Huu ni mwanzo wa Museveni kutimiza ndoto yake ya ushindi uchaguzi ujao.Kuanzia chuo cha Makerere hadi katikati ya mji ilikuwa ni vurugu tupu. ONA HAPA
Mapema leo katika gazeti moja hapa tayari watu walikuwa wametabiri juu ya kukamatwa kwake na wakatoa sababu kadhaa. soma hapa

2 comments:

Indya Nkya said...

Umeupa jina zuri. Mradi wa Museveni. Ninavyojua siasa za Uganda mambo yataishia si mazuri

Innocent said...

Kweli kabisa kuna kila dalili mambo yataishia sio mazuri.
Hawa jamaa wanaamini sana mtutu wa bunduki kama suluhisho.