My Blog List

Saturday, December 03, 2005

MAGAZETI YAFUNGIWA TANZANIA

Hapa Uganda mambo yamepoa kiasi fulani kuhusu siasa.Inavyoelekea Museveni ni mbabe vya kutosha na hakuna njia ya kumdhibiti.
Kiiza Besigye ni wazi hatagombea uraisi nionavyo;kwani inaonekana kuna migongano ya muda mrefu ya kibinafsi kati yake na Museveni pamoja na maofisa wengine wa serikali hasa wanajeshi. somahapa Kwa hali hiyo hawataruhusu agombee na kama atagombea ninaona hali mbaya baadaye kama atakuwa rais.
Lakini labda tusubiri tuone.Leo niangaze Tanzania manake sasa Mkapa naye kaanza kufungia magazeti.somaSina hakika kama ni halali kulifungia gazeti ila nafikiri hii sio dawa manake kama serikali ingaling'amua nguvu ya mtandao basi isingechukua hatua hii.
Lakini kuna udhaifu sana Tanzania juu ya matumizi ya mtandao, manake sioni magazeti yetu mengi mtandaoni. Hapa Uganda ukifungia gazeti linaendelea kuchapisha mtandaoni.
Nataka niulize hivi kama gazeti linaandika kashfa ya kigogo ambayo inaisumbua familia yake ni makosa ya gazeti au kigogo mwenyewe?Nani alaumiwe hapa?

1 comment:

Ndesanjo Macha said...

Innocent, hivi Museveni kawahi fungia magazeti hapo Uganda siku za karibuni? Halafu sijui nani anafahamu mara ya mwisho gazeti kunfungiwa nchini Kenya. Una taarifa hizo?