My Blog List

Thursday, November 10, 2005

MGOGORO WA ZANZIBAR--SIASA MBOVU ZA NYERERE NA KARUME

Mgogoro wa siasa za Zanzibar kwa mara nyingine ni kielelezo kwamba Rais Benjamen Mkapa amefeli kuvirejesha visiwa hivi katika amani iliyopotea kwa muda mrefu.Inavyoelekea tunakwenda kumchagua Kikwete kuwa rais wetu kwa miaka mingine mitano au hata kumi kwani CCM ni utamaduni mtu hang'oki mpaka apige miaka kumi hata kama uchumi unakwenda kombo.
Katika pitia zangu za magazeti basi nikakutana na makala moja ndani ya East African, mwandishi anajaribu kuelezea mchango mkubwa wa hayati Mwalimu Nyerere katika siasa za muungano.Ni makala nzuri bonyezahapa ambayo kwangu imenifanya nione chanzo cha matatizo yote haya ni Mwalimu Nyerere na Karume kutuunganisha katika misingi mibovu.Kama unavyojua ukijenga nyumba katika msingi mbovu basi ujue utakuwa ukifanya ukarabati wa mara kwa mara.
Nimalizie tu kwamba Muungano huu ulijengwa katika msingi mbovu na ndio maana Mwalimu aling'ang'ania Mkapa awe rais ili aendeleze sera zake za kutoruhusu wapemba katika nafasi za uongozi kirahisi.Je Kikwete atafanya nini?Mimi nafikiri ni yaleyale tu.Dawa ni Wapemba waache siasa au wajiunge na CCM ili watoe upinzani wakiwa ndani ya CCM kwani tukumbuke upinzani ndani ya Bunge na Baraza la Wawakilishi ulikuwa mkubwa sana kabla ya siasa za vyama vingi kulinganisha na sasa.
Kweli tumekwisha.

1 comment:

FOSEWERD Initiatives said...

kaka kessy wewe uko kama mimi. suala la watu kudhani kuwa wana copy right ya kutawala na kucheza na maisha ya watu ndilo mimi huwa ninalikataa!! na mimi kimsingi nimeamua kufanyia kazi maovu yoote ya mwalimu ambayo ukilinganisha utagundua ni mazito pengine kuliko mema aliyofanya! karibu globuni kwangu - nitaendelea kuandika kwa sasa suala la muungano liko mahakamani. tukilimaliza hilo ni awamu nzuri sana!

ninamsikiliza abubakar mgunmia sasa hivi akiwa huko shinyanga anafungua kongamano la madaktari anadai eti mgomo wa madaktari ni siasa!!! MY GOD SIJUI TANZANIA TUNAKWENDA WAPI!!

usijali wale wapemba wako makini na kwa sasa huko bungeni wameishawasha moto! mwanablogu materu yuko zenji anatuambia CUF wamekataa kuutambua muafaka rasmi na hapo january wataitisha maandamano nguvu ya umma nchi nzima kuonesha dunia kuwa mabo si kama wanavyodhani!

cheers