My Blog List

Wednesday, December 15, 2010

WILIUM RUTOHUYU NI MWANASIASA MACHACHARI SANA WA CHAMA CHA ODM. KWA SIKU ZA KARIBUNI ALISIMAMISHWA UWAZIRI KWA TUHUMA FULANI ZA FEDHA. ANATOKA KATIKA BONDE LA UFA AMBAKO NI SEHEMU YENYE WAPIGA KURA WENGI NA MUHIMU KWA MGOMBEA URAIS YEYOTE.
NI MWANASIASA WA AINA YAKE, ALIKUWA CHAMA CHA KANU WAKATI WA MOI NA AKAKIAMA KANU AKAJIUNGA NA ODINGA - ODM NA SIKU ZA KARIBUNI YUKO KAMA HAYUKO ODM. ALIKUWA ANAJIANDAA KUANZISHA VUGUVUGU JIPYA KUGOMBEA URAIS. KATIKA KURA YA MAONI YA KATIBA MPYA ALIKUWA KAMMBI ILIYOPINGA KATIBA HIYO.
HUYU NI MFUASI WA SIASA ZISIZOPENDA MABADILIKO NA ALIPAMBANA SANA WAKATI WA UCHAGUZI KUMTETEA ODINGA. HAELEWEKI SANA KWANI NI MTATA SANA LAKINI MJENGA HOJA MZURI. NIONAVYO SIDHANI KAMA ATAHUSISHWA NA TUHUMA HIZI MOJA KWA MOJA BASI HATA RAILA ODINGA HATAPONA. KWA WAKATI HUO WALIKUWA PAMOJA SANA.

No comments: