My Blog List

Monday, December 20, 2010

WAFANYABIASHARA KUKAMUA WANYONGE

Maskini wafanyabiashara kila kukicha wanahangaika kujua wapi watapata fedha. Sasa wagonjwa wa Ukimwi wanatarajia kushindwa kumudu dawa zao kwani kuna makubaliano ya kibiasha kati ya India na Jumuiya ya Ulaya yanakuja kudhibiti uuzaji kiholela wa dawa hizo. Inatarajiwa dawa hizo zitauzwa ghali, tuombe Mungu aepushe mbali.

Lingine juu ya wafanyabiasha, eti Tanesco imeruhusiwa kuongeza bei ya umeme. Bado umeme ni wa wasiwasi, sasa tujue hii nyongeza ya bei ya umeme ni kwa ajili ya tumbo za vigogo wa Tanesco, au kuhudumia matumizi ya kisiasa ya chama fulani au nini? Mimi nashindwa kumuelewa huyu jamaa wa Ewura hivi katika kupokea maombi ya Tanesco aliwahoji juu ya huduma zao? Kwanini nchi hii tumefika hapa? Yaani hatujali unyonge wa wananchi wengi wa nchi hii? Kwanini jamani? Is this fair?

Hili lingine, hebu angalia wanavyoiibia nchi hii alafu wakisemwa wanachukia.

4 comments:

emu-three said...

Lazima maandiko yatimie mwenye nacho ataongozewa na asiyekuwa nacho, atanyang'anywa hata kile kidogo alichokuwa nachp. Sasa huna kabisa, ...!
Hujaweka umeme, umepanda bei, ufanyeje...mishumaa itauzwa kama njugu...mmh, mwisho wa siku TB's, ...sijui na nini tean!

Innocent Kasyate said...

Thanks emu, it will be a feast for viwanda vya madawa.

Yasinta Ngonyani said...

Hodi wenyeji nimepita hapa nimekukuta kwa Mtakatifu simon nimeona nikusalimie .nawe unakaribishwa Maisha na Mafanikio.mmmhh, naona haupo nitarudi tena .....

Innocent Kasyate said...

Nakushukuru kwa kubisha hodi, karibu sana. blog nzuri, hii ni ya kusini mwa tz nadhani. Huko sijawahi kufika, iko siku.