My Blog List

Tuesday, September 13, 2011

TUMEANZA NA MELI BADO NDEGE

Ajali haina Kinga - Wahenga walisema. Sijui wenzangu mtasemaje ila hizi ajali mbili zilizotokea moja, Zanzibar ambapo meli imezama na ya pile kule Kenya ambapo bomba la mafuta limepasuka na likaua wakazi wengi masikini ambao waliamua kujenga nyumba juu ya bomba la mafuta linadhihirisha kuwa "Ajali ina kinga bwana".
Hebu ona hili: Meli ina uwezo wa kubeba abiria idadi fulani; lakini kwa tamaa na utamaduni wa kuvunja sheria abiria wanashindiliwa kwenye meli mpaka inaelemewa na kuzama. Kama Sheria ya Sumatra juu ya udhibiti wa usalama vyombo vya majini ingesimamiwa, je ajali ingetokea? Tujiulize.
Jambo lingine, jana wakati wa hitma ya kkuwakumbuka marehemu hawa wa meli, Rais JK alieleza jinsi uokozi ulivyofanyika nikashangaa sana. Eti meli imezama saa 7 usiku, yeye kapewa taarifa saa 9. Alafu vyombo vya uokozi vya jeshi na polisi vilishindwa kuiona meli ilipo hadi saa 11 alfajiri, karibu masaa 5, pale helkopta ilivyofanikiwa. Hivi kweli ni sahihi kutumia helkopta moja kutafuta meli? Kwanini hazikutumika helkopta nyingi?
Inashangaza sana, wakati wa Kampeni za Siasa, Raisi anatumia takriban helkopta nne zilizokodiwa kwa mahela lukuki; lakini inaonekana jeshi halina helkopta au hakuna utaratibu wa helkopta sijui nini.
Naamini haswa, kuwa ajali hii ya meli ingeepukika ama pasingetokea kifo hata kimoja.
Maadam watanzania tumekubali kuishi kwa kutozingatia usalama wa maisha yetu; basi sitashangaa hata tukaanza kushuhudia ajali za ndege, kwani sasa hivi, usafiri wa ndege umekuwa sana, na ninaamini kwa tabia yetu ya kutojali usalama, sitashangaa ajali za ndege zikianza.

No comments: