My Blog List

Tuesday, September 20, 2011

UGANDA - WEAKLEAKS HAIKANUSHWI ILA YANAFAFANULIWA
Uganda ni nchi ambayo imekuwa chini ya utawala wa Rais Museveni kwa miongo kadhaa sasa. Rais huyo inasemekana sasa ameanza kuwa dikteta na anamuandaa mwanae kumrithi kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa kiafrika. Ndani ya chama chake wako watu ambao wamethubutu kuweka wazi juu ya kupinga baadhi ya mambo ambayo anayafanya.
Yuko bwana mmoja, Kapteni Mike Mukula, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa NRM kutoka ukanda wa Mashariki na aliyewahi kuwa waziri wa Afya, amenukuliwa na Wiki Leakes akisema kuwa hakubaliani na mambo ya Museveni na alipohojiwa hakupinga mambo ambayo aliongea na Balozi wa Marekani. Huyu bwana jasiri kwelikweli, tungekuwa na viongozi wa aina hii wanamzunguka Rais wa Tanzania, mbona ingekuwa raha!

No comments: