
Naamini huyu ndiye mwanamke ambaye alikuwa makini kwa kile alichokiamini. Lakini kama kawaida yetu wanadamu, kifo kimemfika na sasa serikali imeamua itampa maziko ya kitaifa. Profesa Wangari, aliweka wosia kuwa akifa asizikwe na jeneza la mbao kwani ni kuharibu misitu.
Alikuwa ni mwanamke mwanaharakati haswa wala si hawa wanaharakati wa kijinsia ambao uswahiba wao na mafisadi ndio mtindo. Huyu alisimamia alichokiamini akiboresha mazingira na wanawake wa kawaida vijijini na sio hawa wanawake wasomi ambao kwao kutetea wenzao si jambo la msingi sana.
Kifo cha mama huyu kina maana nyingi sana mojawapo ikiwa ni hii hapa na pia alikuwa anajituma kwa alichokipambania. Hii ilimfanya awe tofauti na wengine na pia kwa kiasi kikubwa wengi waliomjua siku zile, wanadai alikuwa mbele yetu sana kiuelewa.
1 comment:
Nice blog and article, thanks for sharing
Post a Comment