My Blog List

Thursday, September 22, 2011

PIKIPIKI (BODABODA) INANITISHA KUIENDESHA


HAPA NAJIVINJARI SIJUI NIACHE USAFIRI HUU?
Kwa mtanzania wa kawaida kama mie, usafiri ninaomudu ni bodaboda. Mie naendesha ya kwangu lakini hali ya usalama huko barabarani ni mbaya sana. Kwa miezi nane tu iliyopita tayari wamekufa watu 53 kwa ajali za pikipiki.
Najiuliza sijui niache kuendesha au vipi manake ukiacha hivyo vifo, majeruhi ndio usiseme. Angalia taarifa hii ya polisi Tanzania uniambie nifanyeje, hivi kwani nini hasa chanzo cha ajali hizi nyingi hivi? Binafsi huu ni mwaka wa nne naendesha pikipiki, nimepata ajali mara moja tu, na siku hiyo ilinibidi niache kuendesha kwa wiki hivi manake nilipatwa na kiwewe, Mungu alisaidia sikuumia ingawa nilichubuka magotini tu na mtambo haukudhurika. Mwendesha baskeli mmoja mlevi aliingia barabarani nikiwa kwenye spidi, katika kujaribu kumkwepa ndipo nikamgonga na nikaruka mtaroni. Ni Mungu alisaidia tu.
Kwa takwimu hizi za polisi, nimebaki sina majibu kwa usalama wangu, nifanyeje jamani?

1 comment:

PoeL Jurnal said...

woouw that'syourt cycle like very old rite..but looks like very matched used with you. lol..www.jurnalpoel.blogspot.com