My Blog List

Sunday, November 28, 2010

WAJUE MAWAZIRI WALIOAPISHWA

Baada ya baraza la mawaziri kuapishwa hapo jana, sasa ni wakati wa kujua sifa au wajihi wa wateule hawa maalum wa serikali yetu tukufu.Inasemekana wengi ni majeruhi na wanaodai hivyo wanayo mengi ya kusema juu ya mapungufu ya baadhi yao.Mtizamo wa mapungufu unatolewa zaidi na wale ambao ni wapinzani wa CCM.
Naye Lowasa ameamua kutoa tamko juu ya tuhuma kumzidia.

Thursday, November 25, 2010

MAONI YA WANANCHI JUU YA CABINET LA JK

Nilipofuatilia vyombo vya habari leo, kuna maoni tofauti juu ya cabinet ya Jk.
Baadhi wana tafsiri zao tata na wengine ndio hivyo tena. Pia wengine walitaka hata baadhi ya wateule waachwe sijui kwanini.

Wednesday, November 24, 2010

BARAZA LA MAWAZIRI LATANGAZWA



Hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr.Jakaya Kikwete amelitangaza baraza lake la mawaziri. Taarifa kutoka Mawasiliano Ikulu imesomeka kama ilivyo hapo chini.

Katika Muundo wa Serikali hakuna mabadiliko makubwa isipokuwa yafuatayo:

1. Idara ya Umwagiliaji tumeiunganisha na Kilimo ambako ndipo ilipokuwa zamani.

a. Imeonekana upangaji wa maendeleo ya kilimo unakuwa hauna hakika bila ya umwagiliaji kuwa sehemu ya kilimo. Tuliihamishia maji kurahisisha pia upangaji na hasa kwa vile maji ndiyo wanaotoa haki ya matumizi ya maji.

b. Kwa kuwa tatizo la uhaba wa maji ya binadamu ni kubwa sana na tunataka tuongeze kasi ya kukabiliana na tatizo hilo tumeona tuiondolee wizara hii mzigo wa umwagiliaji ili ibaki na kazi moja tu ya kuhakikisha kuwa watu wanapata maji safi na salama mita 400 kutoka wanapoishi.

2. Idara ya Vijana tumeihamisha kutoka Wizara ya Kazi na kuihamishia Wizara ya Habari kwa sababu kuu 2.

a. Kwanza inashabihiana na michezo na utamaduni.

b. Tunataka Wizara ya Kazi ipate muda wa kutosha wa kushughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi ambayo sasa yamepanuka.

3. Shughuli za Uwezeshaji wa Wananchi zilizokuwa Wizara ya Fedha na Wizara ya Kazi zitahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

4. Marekebisho mengine ni madogo:

a. Katika Ofisi ya Rais tunairudisha shughuli ya mahusiano na jamii hivyo tunaongeza Waziri wa Nchi ambaye pia atashughulikia shughuli zilizopanuka za Tume ya Mipango, MKURABITA na TASAF.

b. Katika Ofisi ya Waziri Mkuu tutakuwa na Waziri wa Nchi wa kushughulikia Uwekezaji na Uwezeshaji wa Wananchi.

c. Katika Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya TAMISEMI tumeongeza Naibu Waziri wa kushughulikia masuala ya Elimu.

Baada ya kusema hayo nitangaze orodha yetu:

MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

Ofisi ya Rais

1. WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe
2. WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Hawa Ghasia
Ofisi ya Makamu wa Rais
1. Muungano
Samia Suluhu
2. Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa
Ofisi ya Waziri Mkuu
1. Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi
2. Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
George Huruma Mkuchika
1.Aggrey Mwanri
2. Kassim Majaliwa

Wizara ya Fedha
Mustapha Mkulo
1. Gregory Teu
2. Pereira Ame Silima
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Shamsi Vuai Nahodha
1. Balozi Khamis Suedi Kagasheki
Wizara ya Katiba na Sheria
Celina Kombani
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard K. Membe
1. Mahadhi Juma Mahadhi
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. Mathayo David Mathayo
1. Benedict Ole Nangoro
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
1. Charles Kitwanga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Prof. Anna Tibaijuka
Goodluck Ole Madeye

Wizara ya Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige

Wizara ya Nishati na Madini
William Mganga Ngeleja
1. Adam Kigoma Malima

Wizara ya Ujenzi
Dr. John Pombe Magufuli
1. Dr. Harrison Mwakyembe
Wizara ya Uchukuzi
Omari Nundu
1. Athumani Mfutakamba

Wizara ya Viwanda na Biashara
Dr. Cyril Chami
Lazaro Nyalandu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru Kawambwa
1. Philipo Mulugo

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Haji Hussein Mpanda
1. Dr. Lucy Nkya

Wizara ya Kazi na Ajira
Gaudensia Kabaka
Makongoro Mahanga

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Sophia Simba
Umi Ali Mwalimu

Wizara ya Habari, Vijana na Michezo
Emmanuel John Nchimbi
1. Dr. Fenella Mukangara

Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Samuel John Sitta
Dr. Abdallah Juma Abdallah

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Prof. Jumanne Maghembe
1. Christopher Chiza

Wizara ya Maji
Prof. Mark James Mwandosya
Eng. Gerson Lwinge

Nitawaapisha Jumamosi tarehe 27 Novemba, 2010 saa 05:00 asubuhi

Sunday, November 21, 2010

VITI MAALUM - ITAFUTWE FOMULA NYINGINE

Binafsi sipendi kabisa kusikia mtu anatambulishwa kama Mbunge wa Viti maalum. Sidhani kna manufaa yoyote ya umma kutoka kwa wabunge hawa. Hii ni upotezaji wa fedha za umma kwa wabunge ambao sijaona wana tija gani bungeni.
Naomba nipewe jina la mbunge wa viti maalum ambaye amewahi kuwa agitative enough kuonesha anawakilisha kundi fulani la jamii. Itafutwe fomula nyingine ya kupata wabunge hawa, kwa mfano kuwe kuna uchaguzi wa mbunge mwanamke kila mkoa kwa kushindanisha kila chama kutoa mgombea wakati wa uchaguzi.Hii itasaidia kupunguza matumizi yasiyo na tija.

Ndio maana nashangaa kwa nini wako zaidi ya 100 sasa bungeni, je hii ni nzuri kwa mwanamke wa kawaida ama ni mradi wa kifisadi?

DU! CHADEMA AU CCM, NANI YUKO SAHIHI?

Eti Jakaya Kikwete alichaguliwa kwa udini au siasa? Je ni kweli kuna udini Tanzania? Kuna jamaa kajadili hapa, kasheshe kwelikweli. Hii demokrasia yetu bwana, ina vituko sana,yaani kama ni kweli Raisi anajiandaa kufanya uteuzi huku baadhhi ya wabunge wanamshinikiza ni wizara ipi awape. Hapa Rais wa nchi ni yupi? Anayejichagulia cheo au anayetoa cheo? Jiulizeni.

Kuna madai kuwa wabunge wa chadema wamegawanyika wengine wakiona kuwa walikosea. Huu ni wakati wabunge waelewe kuwa in order to prevent the country not been thrown to the dogs completely, ni wakati wa ujasiri. Kama ni kweli Chadema wako makini na wana dhamira basi tutarajie kuwa tanaweza shuhudia maandamano na hata mikutano ya hadhara tena siku si nyingi. Nchi imefika mahali panapohitaji mkombozi na ni vyema wajiandae, kwani kuwa upinzani si kupiga makofi tu mjengoni bali ni kazi haswa.

Kitendo cha Chadema kina asili ya kihistoria.

Saturday, November 20, 2010

CHADEMA WANA KAZI KUITHIBITISHIA JAMII JUU YA UHALALI WA KUSUSA BUNGE

Watu wameendelea kuilamu Chadema kumgomea Raisi Kikwete Bungeni.
Inaelekea CCM watazua hoja binafsi Bungeni kuwaadhibu wabunge wa Chadema. Hapa napo ni utata mtupu, kwani yatatokea yaleyale ya Zitto Kabwe.
Mtizamo wangu ni kuwa nadhani ni vyema Chadema watoe maelezo ya kina kwanini waliamua kufanya vile. Manaake watanzania wengi wanalitizama tukio lile kama vile kukosa adabu.Inashangaza sana kuwa watanzania wengi hawaelewi njia mbalimbali ambazo ni sehemu ya kuwasilisha ujumbe kuwa kuna tatizo linahitaji ufumbuzi.
Inaonekana nchi imejaa "laymen" wengi sana ambao kwao wanaaona nchi yetu inatawaliwa vizuri. Ukisoma makala hii katika "The Citizen" la leo ni wazi hata wasomi wengi wanahimiza eti kuwe na dialogue, maridhiano. Hivi kweli tunahitaji maridhiano hapo ama ni Katiba ibadilishwe?

KATIBA MPYA NDIO SULUHISHO
Watu kadhaa wanatoa maoni na mitizamo yao kuwa Katiba kama
sheria mama
, ni wakati wa kutengenezwa upya.

SPIKA MWANAMKE - ILIKUWA SAHIHI?
Unajua wengi wamesema na hata mimi naamini kilichotokea ni ubaguzi wa kijinsia. Kinachobakia ni mama kuhakikisha she has to prove wrong that she's an agents of the mafisadi. Ningependa tumsome huyu mzee hapo chini ana mtizamo wake juu ya hili:

Is the procedure to elect House Speaker fundamentally flawed?

digg
By Karl Lyimo
Last Friday, Tanzania came into a newly constituted National Assembly – ‘Bunge’ – and a new Speaker, Anna Makinda. The significance of this is three-fold… One: almost a third of the 339-seat House is from Opposition political parties. Two: a goodly proportion of the new MPs are youngish…


But, perhaps the most important aspect of the whole shebang is that, for the first time in the country’s 49-year Independence History, the Speaker is a woman. This has thrown a spanner in the gender-inequality works.
At long last, the Legislature – one of the three statutory Estates of the Realm… Or four, if you take into account the de facto the Independent Press Estate – is headed by a daughter of the soil.

For better or for worse, this – taken together with the fact that nearly a third of the august House is also ‘manned’ by Lady Members – is another major step in the way forward to entrenching gender equality in Tanzania.
Of course, the Lady Speaker didn’t fall like manna from Heaven. She was tactically maneouvred into the scoring position by her ‘Nambari Wan’ patron, the veteran ruling party CCM. The top party caucus axed ten of its members who’d come forward to contest the post, leaving three aspirants – all women, as it ‘conveniently’ happened!
The field included Samuel Sitta, the immediate past Speaker, and Andrew Chenge – a decoy if I ever saw one! But, that’s another story…

Considering that gender equality’s a fashionable clarion call, there was no better vehicle to convey one of the three into the Wool Sack (House-of-Lords pardon!). In the event, Ms Makinda easily won the post with 265 votes against 53 for his formal rival from the Opposition, Mabere Marando.
This wasn’t surprising – especially considering that her party already had 251 MPs as of November 12, compared with a combined total of 82 ‘Opposition’ MPs… as well as scores of fellow women MPs!

However, what’s surprising – if that’s the correct word – is that Marando could only muster 53 of the votes… One would’ve naturally expected him to garner all the ‘Opposition’ votes! What happened to the other 29?
Of course, the easy answer’s that ‘they virtually crossed the floor,’ going to their political rivals who were already heavily fortified, anyways! But, this wasn’t necessarily the case – or she’d have won by 280 votes (251-CCM-plus-29 Opposition ‘defectors’).
Equally interesting is that some CCM MPs may’ve also voted for the Opposition candidate – thereby reducing Makinda’s ideal total from 280 to 265.

That’s if only because among them must be ‘male chauvinist pigs’ (Angela Davis pardon); disappointed Sitta-supporters, Opposition Camp followers-at-heart…
(Would you believe it? Nine ballots were spoiled!)
Confused? Let’s leave that and move on! Ideally, such crucial voting shouldn’t be secret… MPs should’ve the courage of their convictions, stand up and be counted as supporting who – and may the best candidate win!
(Indeed, the best candidate, Samuel Sitta, was jettisoned via caucus fiat. In my view, Sitta did much to put Tanzania in the good books of the comity of nations than most any other person – bar Mwalimu Nyerere… But, again, that’s another story).

Finally, regardless of what the Constitution says in the rider to Article 68, the Speaker wasn’t elected by MPs in the real sense of the term.
One really doesn’t become an MP unless and until one formally takes and subscribes the Oath of Allegiance…


Only then can we nail them to the masts if, say, it is found that they had sold their vote for a mess of pottage!
Then there’s the small matter of the Public Leaders Ethics Code… Is the Speaker (Article 84(5) and her MPs (Article 70(1) able, willing and ready to publish formal statements regarding their property… Sorry. Cheers!
[ Israellyimo@yahoo.com

Ukishaisoma hiyo makala nataka uniambie unaonaje? Mie nampa shavu mzee kwa kujenga hoja.

Thursday, November 18, 2010

JK AFUNGUA BUNGE LA 10 - CHADEMA WAMSUSIA

Nimemtizama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Bunge mjini Dodoma. Lilikuwa ni tukio la aina yake kwani serikali ya CCM ilijitahidi kuonesha kuwa kwa sasa ni wazi kule Zanzibar CCM na CUF ni kitu kimoja. Maridhiano yamekuwa ni machungu kwa kambi ya upinzani kwani kwa sasa itapata wakati mgumu kwa idadi kinyume na watu walivyofikiri awali kuwa upinzani Bungeni ungekuwa umeimarika kumbe wapi.
Kuhudhuria kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, kumeonesha wazi kuwa kwa sasa CUF kama mshirika mkuu wa CCM Zanzibar ni wazi kuwa serikali ya CCM imefanikiwa kuleta amani Zanzibar na hapo hapo kudumaza nguvu ya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

1. CHADEMA WAMSUSA RAISI
Baada ya Raisi kukaribishwa na Spika wakati akianza kumshukuru Spika, nilimwona mbunge wa Hai, na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitizamana na mwenzake na mara moja wabunge wote wa Chadema ambao wanaunda Kambi ya Upinzani bungeni walisimama na kutoka nje huku wakizomewa na wenzao wa CCM kwa makofi ya kejeli. Rais alibakia akitabasamu; Rais wa Zanzibar alionesha uso wenye kutaharuki na kuwaza sana wakati huo. Nilitegemea rais Kikwete azungumzie hali iliyojitokeza lakini alijifanya hajali na akamaliza hotuba yake bila kusema lolote lakini hakuacha kupiga mkwara kuwa wapinzani watambue kuwa yeye ndiye Rais wao.

Hili la utambuzi nadhani Raisi bado hajalielewa; hapa kuna swala la kupinga utaratibu mzima wa uchaguzi wa Raisi na hasa muundo na utendaji wa Tume ya Uchaguzi kama kiini cha hali tata na kasoro ambazo hazielezeki kimantiki kwa mtu yeyote mwenye akili ya kufikiri kimakini. Tatizo ambalo limejitokeza nadhani ni “legitimacy” ya uraisi wa Kikwete. Ni kweli tayari ameapishwa lakini suala wabunge kumgomea si la mzaha ni suala lenye kuhitaji kujiuliza hivi tumefikaje katika hali hiyo?

2. UTAWALA BORA – UFA WA KIDINI
Raisi katika hotuba yake ya ufunguzi wa bunge la tisa miaka mitano iliyopita alidhamiria kuimarisha taasisi za kidemokrasia ili zifanye kazi kisasa. Hadi leo unapoona kuna mapungufu mengi sana katika suala zima la uchaguzi ni wazi raisi kashindwa kutimiza ahadi yake. Taasisi zote za kidemokrasia kuanzia msajili wa vyama hadi Takukuru, haziko huru na zinaendeshwa kama vile bado tuko katika nchi za kikomunisti. Huo kwa Rais Kikwete ndio usasa anaoutaka alafu anashangazwa na aibu hii ya wabunge kumsusa.

Nimefuatilia hotuba ya Rais Kikwete anasema eti nchi ina ufa wa kidini ambao unatishia mgawanyiko wa kitaifa. Kila hili linaposemwa na viongozi wetu tangu wakati wa Kampeni linanishangaza sana. Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuja kipindi ambacho demokrasia imekuwa hadi asasi na viongozi wa kidini tayari wameanza kushiriki katika kushawishi masuala ya kisiasa. Hali hii haikwepeki katika maendeleo ya kidemokrasia na kwa wahafidhina “conservatives”, kwao wanadhani viongozi wa dini wameamua kumpigia chapuo mgombea Fulani. Ni vyema Raisi pamoja na wanaomshauri wafuatilie maendeleo ya demokrasia kule Amerika ya Kusini ambapo pamewahi kuwa na udikteta sana hapo nyuma. Lakini tangu kuibuka kwa wimbi la “ Theolojia ya Ukombozi” viongozi wa dini waliamua kuungana na waumini wao kupigia chapua katika kutoa elimu ya uraia wakibainisha sifa za kiongozi bora. Matokeo yake walichaguliwa viongozi bora na leo uchumi wa nchi hizo umeimarika na utawala bora ndio usiseme.
Kipindi chote cha kampeni sikuwahi kusikia viongozi wa kidini wakiendesha kampeni au mahubiri dhidi ya mgombea Fulani kwa kuvutia watu wao wachague muumini wao. Ila viongozi wa dini wengi wa kikristo walikazia sana sifa za kiongozi bora ambazo kwa kiasi Fulani ziliwagusa wagombea Fulani bila kujali dini zao. Huu ndio ulikuwa msisitizo na ni wazi kwa mtanzania yeyote mwenye akili timamu atakubaliana na mimi kuwa, katika sifa za kiongozi bora ambazo ziliainishwa na viongozi wa dini hasahasa zilikuwa zikitaja kiongozi atakayechaguliwa awe na sifa ambazo zitasaidia Taifa kuepukana na changamoto ambazo serikali ya Kikwete iliyopita ilikuwa imeshindwa kuzishughulikia.

Ni wazi viongozi wengi wa dini walionesha kuwa hawakuwa wanaridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya awamu iliyopita. Bahati mbaya sana viongozi wengi wa aina hiyo walikuwa wa dini za kikristo. Hali hii ya kuelezwa hisia za ukweli ndizo zinamfanya Raisi Kikwete na wapambe wake kutafsiri hali ile kama vile kuna ufa wa kidini. Ninaamini kwa viongozi wengi wa kidini wa kikristo ambao naamini wamekwenda shule vizuri, hata kama leo hii Tanzania ingekuwa chini ya raisi mkristu, na uongozi kuwa wenye mapungufu kama ya awamu iliyopita bado wangepiga kampeni katika mwelekeo ambao ulijitokeza. Siamini kabisa kuwa kuna ufa wa kidini Tanzania wala hakuna chuki dhidi ya kiongozi wa Taifa ambaye ni muislamu bali tatizo ni aina ya uongozi uliokuwepo.

4. AHADI
Kama kawaida yake Raisi Kikwete ametoa ahadi lukuki kupitia mpango wa Maendeleo 2025. Kazungumza mengi matamu masikioni juu ya ndoto yake kichwani juu ya Taifa hili. Kwa mazoea na rais Kikwete sidhani kama ni kweli ana dhamira ya dhati kwani ili tuifikie ndoto hiyo, ni wazi inambidi abadili staili yake ya utawala.

Huku tukisubiri Baraza la Mawaziri kutangazwa, ni wazi tayari serikali atakayoiunda imeshaonesha kuwa haina dhamira ya kupambana na ufisadi kwani uchaguzi wa Spika mpya wa Bunge kwa kumuengua Spika aliyekuwepo umeonesha kuwa Bunge limetekwa nyara na Chama tawala. Serikali yake inataka Spika ambaye ataminya haki ya Wabunge kuhoji serikali katika baadhi ya mambo ambayo yana maslahi ya Chama. Bunge kwa kutumia kisingizio cha “ni wakati wa mwanamke kuongoza mhimili mmoja wa dola” limeonesha wazi halitaki Spika ambaye ataruhusu kila jambo lenye maslahi ya umma kujadiliwa kwa undani. Majadiliano ya aina hii tayari yamewaumbua baadhi ya vigogo wenye fedha ndani ya chama katika Bunge lililopita. Hali hii inaonekana imeleta migawanyiko na hivyo ni afadhali wezi wa mali za umma wasizungumzwe kwani Chama kitachafuka.

5. SERIKALI NA WOGA ISIOUJUA “PARANOIA”
Maadam serikali itakayoundwa itaendeshwa kwa kuhakikisha mambo yote ya kifisadi yanafichwa basi ile “moral authority” mamlaka ya kimaadili ya Raisi Kikwete kuahidi kkuwa atapambana na ufisadi inakuwa haina mashiko kabisa. Nchi imefika hatua inaendeshwa kwa staili ya “Kleptocracy” badala ya “Democracy” alafu watu wanafanya mzaha kwa kusingizia kuna ufa wa kidini au waziri Mkuu Pinda anaonya kuwa kuna Chama Fulani kinatishia amani na umoja wa kitaifa. Hivi hata Pinda haoni ilivvyo vigumu kutumika katika serikali ambayo maslahi ya umma yanashika nafasi ya tatu? Ya kwanza ikiwa ni maslahi ya makundi Fulani ya wakwasi, la pili ni chama na mwisho wananchi. Maadam viongozi wengi wameamua kuchagua “unafiki” kutumika, basi sitashangaa hata yule Spika aliyechinjiwa baharini atapewa zawadi ya uwaziri na atakubali kutumika kwa kufuata misingi ambayo haiamini bali ili mradi mkono unaenda kinywani. Aina hii ya viongozi ndio ambao wamelifikisha Taifa hili kwa sasa halina viwango katika kila kitu ni usanii tu “mediocrity”.

Ukitizama elimu inazalisha wahitimu mediocrity kuanzia ngazi zote hadi vyuo vikuu. Asilimia kubwa ya watanzania hawana uwezo wa kufikiri kwa kina katika mambo mbalimbali. Tumefika mahali sasa Bunge linakuwa na wawakilishi karibu mia mbili wa viti maalum ambao hawana tija kwa Taifa zaidi ya kula fedha za bure tu. Yako mengi nikiyatizama naogopa hivi watoto wangu wataishi Tanzania ya aina gani? Waama! Mungu aepushe mbali, kwa kweli sioni kama tunaelekea kuzuri huko mbele kama Raisi Kikwete asipobadilisha namna ya kuongoza Taifa hili.

HAYA NI MAFANIKIO
Hotuba ya Raisi imedhihirisha mafanikio katika ukusanyaji kodi kumeongezeka, utegemezi wa wafadhili kumeshuka hadi 28% kutoka 42% nadhani. Si haba hapa serikali imejitahidi. Lakini napo pananishangaza sana; hebu fikiria mbona hali za maisha ya watu wa chini ziko hoi bado? Ile “trickle down effect” mbona haipo? Hapa sitasita kusema ufisadi, anasa na matumizi holela ni tatizo ambalo linaondoa ile umaana wa makusanyo lukuki.

Si hilo la makusanyo tu, bali kkuna hili la “mfumuko wa bei umeshuka”, Raisi Kikwete katoa sababu nyingi sana kuhusu misukosuko ya kiuchumi iliyoikumba nchi yetu. Juhudi zilifanyika na tukamudu lakini pia amesema eti mauzo ya nje yameongezeka sana hasa kupitia sekta ya madini. Mimi mwenyewe wakati namsikiliza nilipitia bei ya dhahabu nikaona imeongezeka zaidi sokoni lakini nikashangaa kama wazalishaji mbona bado mfumuko wa bei ni tatizo kwetu ilihali “export” ni kubwa? Kuna nini hapa? Hayo madola ya madini yanaingia serikalini au yapo mifukoni mwa mafisadi? Anajua mwenyewe, lakini sikuona mantiki katika kutetea mfumuko wa bei.

Raisi anadai eti kwa sasa Tanzania inauza zaidi bidhaa nchini Kenya kuliko Kenya inavyouza Tanzania. Imenishawishi nifuatilie mauzo ya Kenya na Tanzania nione inawezekanaje hili litokee kwa nchi ambayo bado tunaona karibu kila kitu kina chapa ya Kenya madukani? Viwanda vyetu bado vimelala, kilimo chetu anajua mungu, utendaji kazi wetu ndio huo ambapo watanzania wengi starehe ndio jambo la mbele zaidi.

6. MICHEZO
Mwisho, Raisi kagusia kuhusu michezo. Hapa alinikuna kiasi Fulani kwa kueleza jinsi ambavyo zamani wakati akiwa shuleni alivyokuwa akifundishwa michezo na mwalimu wa michezo. Ana mawazo mazuri kuhusu kuimarishwa kwa sekta ya michezo hapa nchini na anajua ni nini chanzo cha kudorora kwa michezo. Ila kuna kitu ambacho bado kama watanzania hatujakitilia maanani kama kweli tunataka maandalizi ya michezo na hata sanaa kwa ujumla.

Hapo awali nimeeleza masikitiko yangu juu ya hali mbaya Taifa lilipofikia na nikasema kuwa kwa sasa kwenye elimu hatujali viwango “quality” sisi tumebakia bora liende. “mediocrity”. Michezo na utamaduni ni kielelezo cha jambo hili pia. Ningedhani Raisi Kikwete angepaswa kuelewa kuwa sekta ya michezo imekuwa ni aibu ya Taifa kwa sasa. Michezo haizingatii elimu; na ningedhani kuna haja ya fani ya michezo katika vyuo vikuu na vile vya ualiimu ianzishwe kwa kasi ya hali ya juu. Ukitizama wawakilishi wetu kwenye michezo kama “Olimpiki, Jumuiya ya Madola na hata Soka” pamoja na kuwa na makocha ambao serikali inawalipa bado ni vituko tu. Mediocrity, hali inayosababishwa na wanamichezo wasio na uelewa wa michezo kama fani ya kielimu. Michezo imebakia kkuchezwa na wengi wa vijana walioshindwa kusoma kabisa, wahuni, wavuta bangi, watukutu na watu mbalimbali ambao ni “ant – social katika jamii.

Matokeo yake kuanzia viongozi hadi wachezaji wote hawana maono “vision” wala mtizamo wa mbali ukiacha fedha kama posho za kusafiri tu. Bahati mbaya sana kwa kuzingatia hii hali ya “mediocrity” katika fani mbalimbali hapa nchini, hata wataalamu lukuki pale wizara husika na michezo wamebakia wasindikizaji wa wanamichezo katika matamasha makubwa ya kimataifa ya michezo. Hawana jipya katika kubuni mbinu za kuendeleza michezo nchini. Raisi Kikwete anapaswa aone uendelezaji michezo katika jicho la mtizamo ninaoujadili. Kuna haja ya michezo kuanzia mashuleni na shule ndio ziwe kisima cha kuandaa vijana katika michezo mbalimbali.

Hata kwenye sanaa za maonesho, Raisi amedai kuna mafanikio. Lakini mimi nadhani yapo ya kuboresha zaidi. Ingawa mimi si mtizamaji sana wa filamu za kibongo, lakini nadiriki kusema inanishangaza kila nikitizama filamu, mada ni mapenzi tu. Mtu atasema eti ndio inayouza. Naamini kuna haja ya kuhimiza mada zingine kwenye mambo kama ufisadi, kilimo, siasa na mambo yote yanayoikumba jamii.

HITIMISHO
Taifa limepoteza tunu ya utendaji kazi wa kizalendo na uwajibikaji. Mambo yanafanywa kiujanjaujanja sana. Katika kila fani wataalam kuanzia kilimo hadi michezo wao ni kufukuzia mapato ambayo hawajayafanyia kazi. Utashangaa utawaona wataalamu wa elimu, kilimo hadi michezo wakinawiri kimaisha lakini mambo wanayoyasimamia yako hoi bin taabani. Ripoti zao ziko safi sana ila kimatendo ni bure sana.

Raisi Kikwete hajui kuwa Taifa kwa sasa ni mediocrity kila pahala. Uelewa wa mambo na kuzingatia kanuni za utendaji kazi kwa tija ya maslahi ya umma unapotea. Mfumo wa siasa na utawala una matatizo, watanzania wengi ni wagonjwa kisaikolojia. Their psyche is in disarray. Sina hakika kama hujachelewa; lakini naamini sasa tumefika point of no return. Kama Raisi wetu mpendwa hutabadilika kwa kuanza kuwawajibisha na hata kukaa mbali na mafisadi, hakika kiama cha nchi yetu kitaanza sasa. Na ndipo hapo tutajua legacy ya Kikwete. Nabakia nikisubiri Baraza la mawaziri na nitaweka waraka mwingine.

Saturday, November 13, 2010

MWELEKEO WA SIASA ZA TANZANIA BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2010

Ukizitizama siasa za kiafrika, UKABILA, haukwepeki. Tangu juzi nimetizama wabunge wakiapishwa huku wakiwa wamesindikizwa na ndugu na hata vikundi vya kikabila utadhani mwisho wa siku matokeo ya utendaji wao yatawafikia wanakabila wenzao. Yuko bwana mmoja amejadili jinsi siasa zetu zilivyojaa ukabila.
Huku tukiwa tumemaliza uchaguzi, ni wazi kuwa CCM imethibitisha kuwa ni chama ambacho ni nguva wa kisiasa. Pamoja na kutotegemea tena hekima za Nyerere lakini bado CCM inapeta.
Kudhihirisha kuwa CCM itaendelea kutawala kwa miongo kadhaa, hebu ona jinsi ambavyo itakavyoweza kutawala siasa za Tanzania hadi 2030.

Saturday, November 06, 2010

JAKAYA KIKWETE AAPISHWA

Nilichokiona leo uwanja wa Uhuru ni maombi ambayo yalikuwa yanaashiria mawazo na mitizamo ya viongozi wa dini.
Kwa mfano huyu shehe wa waislamu, yeye alikazia kwa ufupi sana juu ya:

Ee Mola wetu, tunaomba wakinge viongozi wetu na fitna ya uongozi

Uiepushe na siasa za kidini *3

2.Mtu wa pili alikuwa Askofu Valentino Mokiwa akiwakilisha Umoja wa Makanisa Tanzania. Yeye alisisitiza katika sala yake yafuatayo:

Eti Raisi JK apewe na kujaliwa Nguvu katika kuongoza na hekima kutawala
Eti Mungu atuepushe na Tofauti za kisiasa na za itikadi, kidini,
Mungu aepushe dhidi ya Machafuko, pia Mungu ampe JK nguvu za akili, roho, mwili, hekima, busara, na uwezo wa kutafakari mbele.

3. Maombi ya tatu yalitoka kwa kanisa mama: Baraza la maaskofu Tanzania , Askofu Michael

Akiwa na karatasi alisoma sala yake kama ifuatavyo:
Aliamua kuitumia sala ya Nabii Suleiman akimuomba Mungu amtie JK yafuatayo:
Moyo wa hekima na akili, uwajibikaji, baraza la mawaziri, bunge na mahakama na vyombo vya ulinzi waweze kuongoza kuleta heri ya milele mbinguni.

4. Baadaye ikafuata hotuba ya shukrani ya JK na hakusema mengi kwani ameahidi atasema sana siku ya uzinduzi wa Bunge.rais amesema tutembee kwa kifua mbele kwani bado watanzania wengi wanakipenda chama cha mapinduzi.Amewashukuru watu wawili: Dr. Gharib Billali na Mke wake mpendwa Salma Kikwete kkusaida kutafuta ushindi CCM.
Mama Ngangari kutafuta ushindi, lakini pia amewashukuru wagombea wenzake waliowania uongozi na akakiri changamoto zao na ni lazima CCM igangamale kwani huko mbele kutakuwa kugumu.

5. Ameahidi kutibu majeraha ya kampeni ambayo yamegawa watu na jamii za nchi yetu kidini, rangi, jinsia na umaeneo. Amewaomba vyama vya upinzani visaidiane naye kudumisha amani na kuondoa nchi kugawanyika. Hapa atawategemea viongozi wa dini na wanahabari wasaidie kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.

6. Jk hakuisahau Tume ya Uchaguzi kwa kazi bora iliyofanya. Ila kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kufanya tathmini kujua ni yapi yaimarishwe kuleta chaguzi zijazo zenye ufanisi zaidi.

7. Watu wa ulinzi na usalama nao hawakubaki nyuma kushukuriwa na amewaomba waendelee kusimamia utulivu na pia kwa gwaride zuri ambalo walilifanya mbele ya umati wake.

8. Pia ameshukuru UNDP kwa msaada wao katika kufanikisha uchaguzi, Katibu Mkuu kiongozi kwa kuandaa sherehe na pia viongozi wa dini kwa dua zao.

Monday, November 01, 2010

UCHAGUZI MKUU KWISHA KWA HASIRA ZA BAADHI YA WANANCHI WA MIJINI

Uchaguzi mkuu ndio leo na ninaamini watanzania watapiga kura kumchagua kiongozi wanayemhitaji katika wakati tulionao kama Taifa. Ni wazi kama kuna haja ya mabadiliko basi wapiga kura hawatasita kutumia wasaa mfupi katika chumba cha kkupigia kura na kuhakikiksha kuwa ile karatasi ya kupigia kura haitumiki vibaya. Binafsi sipigi kura leo kwa sababu za msingi kabisa kwangu ingawa ni wazi ninapoteza haki yangu ya kiraia. Nitaeleza baadaye kwanini sipigi kura.

Katika uchaguzi huu watanzania watahitaji kupiga picha ya miaka mitano iliyopita na wajionee wenyewe kama kweli Taifa la Tanzania linahitaji mtu mbadala na vilevile chama mbadala. Ni kipindi kigumu kuamua kwani si rahisi kwa watanzania wengi kuamua kutaka mabadiliko na wala si rahisi pia kwa watanzania wengi kuchukua uamuzi kuendelea na aina ya uongozi ambao umemaliza muda wake. Nitajadili mambo haya mawili kuona ni kwanini wapiga kura leo wako njia panda?

Moja, wapiga kura wengi leo hii watapenda kuendelea na chama pamoja na viongozi wa chama kilekile ambacho wamekizoea kwa miaka nenda rudi. Ni chama ambacho kwao kimekuwa ndio kinachohakikisha uwepo na upatikanaji wa mahitaji yao. Nitatoa mifano kadhaa kuonesha uzuri wa chama hiki kikongwe: Hebu fikiria mfanyakazi wa serikali, mtumishi wa umma ambaye anafika kazini muda anaotaka kama vile yeye ndiye mwenye mali. Haulizwi kwanini amechelewa na mara nyingine hata asipofika kazini haulizwi.

Mwingine anafika kazini lakini hafanyi kazi yeyote na mwisho wa mwezi analipwa mshahara na pia anapandishwa cheo. Si hili tu, pia hebu fikiria wako watanzania kibao ambao kitaaluma ni sawa na bure kabisa, mbumbumbu kabisa, yaani hata kuandika vizuri hawawezi kabisa, mtu hajui hata kuandika barua au taarifa yoyote ikaeleweka na kupeleka ujumbe. Aliajiriwaje? Ni mfumo wa chama na serikali iliyopo. Pakitokea mabadiliko mtu huyu atakuwa hatarini sana.

Si hayo ya wafanyakazi wengi wa kada za chini. Nenda kada za juu. Hapo napo ni kasheshe tu. Wako wengi wamegawiwa vyeo na nafasi walizonazo katika ngazi mbalimbali. Kwao urafiki na uswahiba wao kwa wenye chama ndio njia pekee ya kufaidika na nafasi na vyeo katika taasisi mbalimbali. Hawa ni wengi sana na sidhani kama watakubali kupiga kura kukiondoa chama cha ccm madarakani. Hawa wote, ni kutetea maslahi yao kibinafsi zaidi pamoja na tabaka tawala na kuendeleza hali iliyopo “status quo”.

Kwa upande mwingine kuna watanzania wengine ambao kwao kura yao itataka mabadiliko. Kwao kuendelea na utawala uliopo si hatua muafaka. Kwao wanataka Tanzania mpya wakiamini yako mambo mengi ambayo yanapaswa kubadilika. Kwa mfano, habari ya ufisadi iliyokithiri hapa nchini kwa takriban katika serikali inayomaliza muda wake ni hadithi ambayo kwao ni chungu ambayo haivumiliki. Kwa mfano, wizi wa fedha za EPA, Kashfa za Meremeta, Richmond, na nyingine nyingi hazina majibu.

Kwa wapenda mabadiliko wanashangaa jinsi ambavyo chama kilichopo madarakani kilivyoshindwa kutoa majibu ya msingi juu ya hatua madhubuti kuondoa ufisadi nchini. Wanakasirishwa zaidi na hatua ya chama kuwapiga marufuku wagombea wake wote kushiriki midahalo ambayo ingeruhusu wahojiwe na watoe maelezo kwa wananchi juu ya mapungufu yanayoonekana katika utendaji wao kwa miaka mitano iliyopita.

Wanaopenda mabadiliko wanashangazwa na jeuri iliyooneshwa na chama kilichopo madarakani wakati wa kampeni. Hii ni jeuri ya fedha katika matumizi ya vifaa vya kampeni wakati wananchi wengi wakipata shida juu ya huduma mbovu na kupanda sana kwa gharama za maisha kunakosababishwa na kushuka kwa thamani ya shilingi. Wanapotaka majibu hawapewi na wanapoleta majukwaa kama vile midahalo pia wenye nchi hawako tayari kutoa ushirikiano. Hali hii ni wazi kuwa watawala hawataki kuwa “accountable” na kwa wapenda mabadiliko hili si jambo la enzi hizi.

Kwa ufupi makundi haya mawili ya wapiga kura: Lile la kuendeleza hali iliyokuwepo “statua quo”, na lingine la mabadiliko yaani kuhimiza “accountability” ndiyo yanayoshindana leo. Litakaloshinda litakuwa na wajibu wa kuhakikisha jamii ya watanzania inaendeshwa kwa kufuata matakwa yake. Nitaendelea kumsubiri mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi amtangaze mshindi na ndipo tutajua hatima ya nchi yetu. Hapo tutajua tutajua nchi itaenda kwa staili ipi kati ya kifisadi fisadi ama ile ambayo tunaahidiwa tu lakini hatuna hakika kwa dhati kama kweli itatimizwa ama inatekelezeka.

Mwisho niseme tu kwanini sijapiga kura leo: kwanza kabisa sijawahi kujiandikisha kwa makusudi kabisa kwa kuzingatia kuwa siamini kuwa kwa muundo wa Tume ya uchaguzi tuliyonayo haiwezi kuwa huru katika utendaji wake wa kusimamia zoezi la uchaguzi. Mpaka hapo Tume huru kwa kuzingatia matakwa ya demokrasia itakapokuwa imeundwa ndipo nitakaposhawishika kupiga kura.