My Blog List

Sunday, November 21, 2010

VITI MAALUM - ITAFUTWE FOMULA NYINGINE

Binafsi sipendi kabisa kusikia mtu anatambulishwa kama Mbunge wa Viti maalum. Sidhani kna manufaa yoyote ya umma kutoka kwa wabunge hawa. Hii ni upotezaji wa fedha za umma kwa wabunge ambao sijaona wana tija gani bungeni.
Naomba nipewe jina la mbunge wa viti maalum ambaye amewahi kuwa agitative enough kuonesha anawakilisha kundi fulani la jamii. Itafutwe fomula nyingine ya kupata wabunge hawa, kwa mfano kuwe kuna uchaguzi wa mbunge mwanamke kila mkoa kwa kushindanisha kila chama kutoa mgombea wakati wa uchaguzi.Hii itasaidia kupunguza matumizi yasiyo na tija.

Ndio maana nashangaa kwa nini wako zaidi ya 100 sasa bungeni, je hii ni nzuri kwa mwanamke wa kawaida ama ni mradi wa kifisadi?

2 comments:

emu-three said...

Mimi hata sijui mchakato wake unakuwaje, nahisi hawa ni wale anaowapenda `mwenyewe' ili kulipa fadhila au kuwakislisha kundi ambalo ni muhimu liwakilishwe!

Innocent said...

Ni nani huyo anaowapenda? Nijuze na mimi simjui.