My Blog List

Saturday, November 06, 2010

JAKAYA KIKWETE AAPISHWA

Nilichokiona leo uwanja wa Uhuru ni maombi ambayo yalikuwa yanaashiria mawazo na mitizamo ya viongozi wa dini.
Kwa mfano huyu shehe wa waislamu, yeye alikazia kwa ufupi sana juu ya:

Ee Mola wetu, tunaomba wakinge viongozi wetu na fitna ya uongozi

Uiepushe na siasa za kidini *3

2.Mtu wa pili alikuwa Askofu Valentino Mokiwa akiwakilisha Umoja wa Makanisa Tanzania. Yeye alisisitiza katika sala yake yafuatayo:

Eti Raisi JK apewe na kujaliwa Nguvu katika kuongoza na hekima kutawala
Eti Mungu atuepushe na Tofauti za kisiasa na za itikadi, kidini,
Mungu aepushe dhidi ya Machafuko, pia Mungu ampe JK nguvu za akili, roho, mwili, hekima, busara, na uwezo wa kutafakari mbele.

3. Maombi ya tatu yalitoka kwa kanisa mama: Baraza la maaskofu Tanzania , Askofu Michael

Akiwa na karatasi alisoma sala yake kama ifuatavyo:
Aliamua kuitumia sala ya Nabii Suleiman akimuomba Mungu amtie JK yafuatayo:
Moyo wa hekima na akili, uwajibikaji, baraza la mawaziri, bunge na mahakama na vyombo vya ulinzi waweze kuongoza kuleta heri ya milele mbinguni.

4. Baadaye ikafuata hotuba ya shukrani ya JK na hakusema mengi kwani ameahidi atasema sana siku ya uzinduzi wa Bunge.rais amesema tutembee kwa kifua mbele kwani bado watanzania wengi wanakipenda chama cha mapinduzi.Amewashukuru watu wawili: Dr. Gharib Billali na Mke wake mpendwa Salma Kikwete kkusaida kutafuta ushindi CCM.
Mama Ngangari kutafuta ushindi, lakini pia amewashukuru wagombea wenzake waliowania uongozi na akakiri changamoto zao na ni lazima CCM igangamale kwani huko mbele kutakuwa kugumu.

5. Ameahidi kutibu majeraha ya kampeni ambayo yamegawa watu na jamii za nchi yetu kidini, rangi, jinsia na umaeneo. Amewaomba vyama vya upinzani visaidiane naye kudumisha amani na kuondoa nchi kugawanyika. Hapa atawategemea viongozi wa dini na wanahabari wasaidie kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.

6. Jk hakuisahau Tume ya Uchaguzi kwa kazi bora iliyofanya. Ila kazi kubwa iliyo mbele yetu ni kufanya tathmini kujua ni yapi yaimarishwe kuleta chaguzi zijazo zenye ufanisi zaidi.

7. Watu wa ulinzi na usalama nao hawakubaki nyuma kushukuriwa na amewaomba waendelee kusimamia utulivu na pia kwa gwaride zuri ambalo walilifanya mbele ya umati wake.

8. Pia ameshukuru UNDP kwa msaada wao katika kufanikisha uchaguzi, Katibu Mkuu kiongozi kwa kuandaa sherehe na pia viongozi wa dini kwa dua zao.

2 comments:

emu-three said...

Sehemu `iliyooneka' ngumu imeisha, lakini sehemu ambayo ni ngumu, na watu hawaionei kuwa ni ngumu, ndiyo hiyo inayokuja mbele kwa hawo waliochaguliwa. Hii ni sehemu ambayo kazi kubwa inahitajika. Hii ni semeu ya kutimiza kile ulichoahidi!
Je ahadi ni deni?

Innocent Kasyate said...

Kweli waliochaguliwa wana kazi hasa. Hebu tusubiri.