Leo kama mtanzania hapa nchini Uganda sina budi kumkumbuka mpendwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.Mengi yamesemwa ila huyu ni mtu wa kipekee kuwahi kutokea katika kizazi cha viongozi wa bara la Afrika.
Ila nimechoshwa sasa na kila mwaka tunapoadhimisha siku kama hii utasikia wanasiasa wakilia eti "Tumuenzi Baba wa Taifa".Sina hakika kama kweli tunamuenzi ipasavyo ila natumaini siku moja tutahukumiwa na kauli zetu.
Hapa nchini Uganda, siku hii imekuja katika wakati ambao swahiba wa Mwalimu, yaani Raisi wa zamani wa nchi hii amefariki dunia akiwa uhamishoni huko nchini Zambia.
Vyombo vya habari hapa vimetawaliwa na habari kumhusu huyu mzee ambaye alipinduliwa mara mbili wakati wa uongozi wake.Tukiwa bado tunasubiri kumzika marehemu Milton Obote,hapa hakuna mengi juu ya Mwalimu Nyerere.Nimesoma Nkya kule Cape Town wameandaa mdahalo maalum juu ya Mwalimu nafikiri ni hatua kubwa na ya kujivunia.Isipokuwa kilichonipa ahueni wiki hii lile gazeti maarufu katika ukanda huu wa Afrika,"The East African" lilichapisha makala kadhaa za kumsifu na kumkukumbuka Mwalimu.
Kuna kitu kimoja ambacho kilinifanya niamini kweli Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi wa kuigwa. Mwanaye wa kwanza, Madaraka Nyerere alichapisha makala nzuri inayoelezea maisha ya Mwalimu baada ya kustaafu.Ni makala ambayo ningependa wanaglobu wote waisome.Hivi mnajua kanisa katoliki nchini Tanzania limeanza kufanya taratibu za Mwalimu kutangazwa "MTAKATIFU"?bofya hapa
Binafsi siungi mkono mtu kuwa mtakatifu kwa vigezo ambavyo huwa vinaangalia upande mmoja ila nadhani hii ni hatua dhahiri kuonesha huyu mtu alikuwa ni kiumbe cha ajabu.
Mimi nimemkumbuka kwa kusoma makala kadhaa katika toleo la The East African wiki hii.

3 comments:
Ukweli ndio huo. Watu wanadhani kumuenzi mwalimu ni kupumzika na kuvipa viwanja na mitaa jina lake. Mwalimu ni zaidi ya hapo. Kumuenzi ni kukaa chini kujadili zile falsafa zake na kuona kama tunaweza kuzitumia vipi katika dunia hii iliyobinafishwa kwa fikra za aina moja.
Nimemaliza kusoma makala ya Madaraka. Nzuri sana. Na kama anavyosema Idya, kumuenzi Mwalimu sio kuvipa viwanja jina lake bali kulinda na kuendeleza msingi aliotuachia.
Ninaomba kuuliza kwamba kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere alikuwa mtu mwenye sifa nyingi namna hiyo kwa nini hakuandika (autobiography) au hakuandikiwa (biography) sharija ya maisha yake?
Nasubiri majibu yenu,
F MtiMkubwa Tungaraza.
Post a Comment