My Blog List

Monday, July 16, 2007

HATUHITAJI SHIRIKISHO ILA JUMUIYA INATOSHA--EAC

Ripoti ya maoni ya wananhi wa Tanzania imetoka na ni wazi wananchi wengi wana woga mkubwa na hawataki shirikisho.Binafsi sitaki shirikisho ila tu napenda tuwe na jumuiya kwani nadhani Shirikisho ni maslahi ya wanasiasa tu na kwa mwananhi wa kawaida si tija.

Lakini pia, kama mtanzania, mimi ni mmojawapo wa wale wasioridhishwa bado kama kweli tunahitaji kuwa na shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) .Ukiusoma mkataba wa kuanzishwa kwa EAC unaeleza kinagaubaga mtiririko mzima unaopaswa kufuatwa na nchi wanachama ili kufikia shirikisho.

Yanayotokea kwa kipindi hiki, kidogo yananishangaza hasa "uharakishwaji wa kupata shirikisho" fast traking.Kwenye mkataba wa jumuiya-mataifa shirika-Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi-yanawajibika hatua kwa hatua, taratibu; yaani kwanza, muungano wa mapato(custom union), pili, soko la pamoja(common market), tatu, sarafu moja(monetary union) na mwisho Shirikisho la Kisiasa(Federation).

Lengo la mchakato huo ni ili kupata ushirikiano makini wa kiuchumi ambapo watu wenngi masikini wataweza kuishi na kumudu maisha ya kiwango cha juu katika eneo hili. Inapowezekana kunyanyua kiwango cha maisha cha raia wengi masikini basi shirikisho linakuwa linawezekana. Shirikisho lingetakiwa lifikiriwe katika kipindi kifupi hadi 2013 kuweza kuzibadili taasisi mbalimbali za kitaifa katika mataifa shirika ziwe chini ya mtandao mmoja wa shirikisho.
Sioni itawezekanaje katika kipindi kifupi hadi 2013 kuweza kuzibadili taasisi mbalimbali za kitaifa katika mataifa shirika ziwe chini ya mtandao mmoja wa shirikisho. Hebu nitoe mifano michache:

Moja, Nchi ya Kenya iko tayari kwa shirikisho kwani ni njia mojawapo ya kuimarisha zaidi nguvu yake ya kiuchumi na kibiashara. Uchumi wa Kenya inasemekana ni karibu asilimia 50% ya uchumi wa Uganda na Tanzania kwa pamoja. Pili, ukienda Uganda na Tanzania hapa pia kuna kiini macho. Taarifa za kiuhumi zinaonesha kiwango kidogo cha biashara kati ya nchi hizi mbili. Kwa mfano, Uganda Bureau of Statistis-2004 zinaonesha mwaka 2003 Uganda iliuza bidhaa za thamani ya dola 78 millioni kwa Kenya, alafu ikauza dola 5.8 milioni kwa Tanzania.
La kushangaza kabisa ni kwamba mwaka huohuo Uganda iliuza bidhaa za thamani ya dola 13.7 milioni kwenda Sudan ambayo sio nchi mwanahama wa EAC.

Ninachokiona hapa kuna hatari inakuja hapo baadaye: Uganda inafanya biashara zaidi na Sudan kuliko Tanzania. Tukumbuke mwaka 2003, Sudan ya Kusini bado ilikuwa itani; sasa hii hali imebadilika kabisa hali ni shwari, na mpaka 2011 upo uwezekano wa Kusini mwa Sudan kuwa taifa huru.

Na kwa hali iliyo sasa biashara kati ya Uganda na Sudan itakuwa sana na wala Uganda haitahitaji nchi kama Tanzania kibiashara kabisa. Haya yote yameshaanza kutokea sasa. Kwa ushahidi tu, mtu aende kushuhudia ni malori mangapi yanapita usiku na mhana yakiwa na shehena ya bidhaa kutoka Uganda na Kenya katika barabara ya Yei hadi Juba.

Uchumi mzuri unapimwa na biashara, na kama ni hivyo je shirikisho la nini?Jumuiya inatosha kwani vikwazo vyote ya biashara vitaondolewa. Shirikisho ni mzigo kwa wanasiasa kutafuna kile kinachozalishwa na faida ya jumuiya kwa kuwakirimu wanasiasa na misafara yao ya kifahari.Nawaunga mkono wananchi kukataa shirikisho ila nasisitiza Jumuiya ni muafaka.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Kweli kabisa!Hili swala mimi naliogopa sana!Halafu kutokana na taaluma zilizo onyeshwa na wataalamu wetu bongo za kuingia mikataba ya ajabu, Richmond moja wapo, na pia Raisi kukiri huko Norway kuwa taaluma ya kuingia mikataba ni duni bongo, mimi naaogopa kujiingiza katika maswala ambayo baadaye tunaweza kujikuta tumeliwa tu.

Innocent Kasyate said...

Nashukuru bwana Kitururu, nakwambia hapa Bongo kuna wasomi lakini tatizo pesa zinafanya bongo zinakufa ganzi. Yaani waheshimiwa wa hapa wameenda shule ila ile "Role Model" hakuna.
Tumekwisha.