My Blog List

Saturday, December 10, 2005

Waziri wa afya wa Tanzania, Anna Abdallah alipokuwa akizindua rasmi kiwanda cha dawa za kusaidia kuongeza maisha kwa waathirika wa ukimwi, waya,mtandao,ngoma) Tanzania Pharmaceutical Industries Ltd, DSM.

Sasa kiwanda cha madawa ya kuongeza muda wa maisha ya mgonjwa wa ukimwi kimezinduliwa rasmi Tanzania. SOMA Kuna watu wamefurahia hatua hii sana kwani kwao vifo vya ugonjwa huu vitapungua. Kwangu mimi nawaza vingine kabisa. Kwani naona ndio mwanzo wa maambukizi mengi hebu tusubiri tuone athari za kiwanda hiki kuwepo nchini mwetu.
Wabongo wengi tulivyo ni kwamba sasa mapenzi ni mbele kwa mbele na kwa maana hiyo tutakwisha zaidi. Na kama ilivyo kawaida Bongo, tutaanza kuuziwa dawa za kufoji na hapo ndio utaona utitiri wa maambukizi. Watanzania ni maskini na wapo wajanja sana ambao huu ni mwanya mzuri kwao kujipatia fedha na ndipo hapo tutakapokufa na kufaana.
Nia yangu sio kuponda ila nathubutu kusema hii ni hatua nzuri katika kupambana na janga hili ila tujiandae kwa madhara.

1 comment:

Jeff Msangi said...

Onyo unalolitoa ni dhahiri.Viongozi na washika dau kwenye masuala ya ukimwi wana wajibu wa kuelimisha umma juu ya hizo dawa.Elimu itolewe kwamba dawa za kurefusha maisha sio dawa dhidi ya ugonjwa.Hatari za maambukizi zipo palepale.Nina uhakika kwamba vijijini hivi sasa kuna watu wanadhani dawa imeshapatikana!