Wakati watu wote makini hapa Uganda wakiwa wamesikitishwa na hatua ya rais Museveni kung'angania madaraka, magazeti mengi yamekuwa yakimsihi Museveni afuate mfano wa rais Mkapa.
Ila leo ndio ilikuwa fungakazi manake gazeti moja hapa liliandika tahariri kumsifu raisi Mkapa kama mfano mzuri wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. somahapa
Kwa Museveni yeye kasema kila nchi ni tofauti na hakuna haja ya kufananisha mifano kwani kila mtu ana njia zake binafsi za kutatua matatizo. Mnasemaje hapo?
2 comments:
Suala siyo kuachia madaraka kwa wakati. Watazame huyo Mkapa katika Tanzania alivyotanua lindi la umaskini miongoni mwa raia. Kuna swali la kujiuliza, wanadhani Tanzania mambo ni shwari maana ufalme wa Uganda upo kwa Museveni lakini ule wa Tanzania wanagawana wana wa familia ya kifalme na ndio maana maisha yao wote safi na wananchi kilio. Afrika tuna kazi kubwa ya kufanya ili kuweka mkondo sawia wa mambo.
Ingawa sera nyingi na utendaji kazi wa Mkapa ninapingana navyo, suala lake la kuachia madaraka kama katiba inavyosema ni jambo la kuzungumzwa hasa katika bara ambalo ni kawaida kabisa kwa watwawala kutaka kuwa kwenye ulaji maisha yao yote. Museveni hupenda sana kusema kuwa Uganda ni tofauti na nchi nyingine na eti ndio maana mfumo wa vyama vingi haufai Uganda bali Mfumo wa Vuguvugu. Kila nchi ni tofauti na nchi nyingine ila sidhani kuwa kuna nchi ambayo katika wakazi wake wote ni mtu mmoja tu anayeweza kuwa kiongozi wa nchi.
Inno, asante kwa kutupatia taarifa mara kwa mara kuhusu Uganda. Endelea kutupa kuhusu kesi ya Kiiza maana wengi tunaifuatilia.
Post a Comment