My Blog List

Monday, August 22, 2005

KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA--NA NJAA YA WAPINZANI.

Jumapili ya jana kampeni zilianza rasmi; la kushangaza wako wagombea kumi wa vyama vya upinzani hii ni hatari kwa demokrasia. Wanatudanganya eti wanataka nchi yetu iwe na demokrasia kumbe wao ndio wanazuia isifanye kazi.
Huo mgawanyo wa kura utakaojitokeza siku ya uchaguzi ndio utakawamaliza kabisa; chama tawala bila wasiwasi kitaibuka kidedea. Kwa mara nyingine tena nchi yetu inapata nafasi ya kuwa na bunge goigoi, litakalokuwa na wabunge wa chama kimoja, watakaokuwa wakitetea sera za chama kimoja hata pale zitakapokosa maslahi kwa walalahoi wa Tanzania.
Nimefikiri nakosa cha kusema zaidi, ila tuombe Mungu miujiza ijitokeze; japo hapa ni vigumu.
Naomba tulijadili hili zaidi wanaglobu wenzangu.

No comments: