My Blog List

Tuesday, November 25, 2008

MAWAZIRI WAANDAMIZI WATUHUMIWA UFISADI KUTOKA KILIMANJARO


Hatimaye JK kaanza kuonesha kuwa hacheki na kima. Jamaa anaanza kutupelekea mahakamani watuhumiwa mawaziri waandamizi katika wizi na kukuza umasikini Tanzania. Pichani juu ni mawaziri Daniel Yona na Bazil Pesambili Mramba ambao leo wamefikishwa kizimbani.
Wamesomewa mashtaka ya kufanya maamuzi bila kujali maslahi ya nchi na wanatakiwa watoe dhamana ya shilingi Bilioni 3.9 kila mmoja. Je watatoa dhamana hiyo?

Je hapa ndio gemu la JK limeanza? Mie sitaki kusapoti sana manake najua hawa jamaa watakuwa nje tu baada ya siku chache kwani walishaiba hela nyingi sana. Na kama watatoka kwa kuweza kumudu dhamana basi namuunga mkono rafiki yangu mmoja aliyesema Tanzania iondolewe katika kundi la nchi Masikini sana duniani. Tutajua jinsi nchi yetu ilivyotajiri sana.

2 comments:

Simon Kitururu said...

Wabongo rahisi kusahau na kusamehe!Wasamehewao kirahisi ni wenyenazo!Tusubiri tuone!

Anonymous said...

Oh please, lets face it, hiki ni kiini macho tuuu, wenye kuchota hela nyingi ni wakina Kagoda agriculture wath not, ambao hawajui hata kilimo ni nini. if we are to be realistic, na kama ni kuburuzana mahakamani nafikiri, ya kagoda yakifichuka hata huyo aliyeshikamadaraka ya nchi aweza buruzwa mahakamani!!!!!!!!, walioko madarakani wengi ni mafisadi, ila wanataka kutoa wenzao sadaka kusafisha uovu wao, kwa mtazamo wangu jk hajafichua makucha lolote, anatumia wenzie kama chambo kuficha mambo yake, watutangazie wamliki wa kagoda , uone kama nchi nzima haijaandamana .