Hii ni globu iliyovumbuliwa nchini Uganda inajaribu kukazia matumizi ya lugha ya kiswahili na kuhabarishana kuhusu maswala mbalimbali ya kijamii hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kat na kwingineko. Siasa na mambo ya michezo na kijamii kwa ujumla ndio itakayokuwa mada kuu hapa.Nitakaribisha maoni yenu.
My Blog List
Wednesday, January 30, 2013
JESHI KUCHUKUA SERIKALI UGANDA?
Kuna kila dalili Rais Museveni anazeeka na hataki madaraka yaende kwingine zaidi ya taasisi pekee anayoiamini: Yaani Jeshi la Uganda. tayari kaonesha kuwa atatengeneza mapinduzi ya kijeshi; kwa maana nyingine atajipindua mwenyewe ili madaraka yabakie chini ya jeshi akiamini itampa wakati mzuri wa kkustaafu.
ALIYEPIGA RISASI YA KWANZA UKOMBOZI WA UGANDA
Generali Elly Tumwine ndiye askari aliyefyatua risasi ya kwanza kuashiria vita ya ukombozi wa Uganda chini ya chama cha Rais Museveni NRM wakati huo kikiitwa NRA. Huyu bwana ana mengi ya kuyafahamu na ni jinsi gani anajisikia kuhusu maendeleo ya Uganda kwa sasa.
Tuesday, January 29, 2013
KIZUNGUMKUTI CHA UTAJIRI WA DRC
Eti si kweli kuwa DRC ni nchi tajiri na Rwanda inafuata utajiri wake.
GESI YA MTWARA NA HISTORIA YA UKOMBOZI WA WANYONGE
Vita kati ya Matajiri na Masikini Tanzania ndiyo taswira ya yanayojiri kule Mtwara. Jenerali Ulimwengu anamulika jambo hili na anaonya matajiri (elites) wakae chonjo.
Anakazia na kukumbusha historia tangu enzi ya Wayahudi utumwani Misri hadi Ubepari mkongwe kwenye viwanda vya Nike kule bara Asia, masikini wanateseka na ni wengi kweli ila mapambano yao yanaendelea. Ni vita iliyopitia enzi za The Magna Carta (1215), Oliver Cromwell’s rebellion (1640s)hadi The French Revolution (1789)iliyowakomboa wanyonge lakini moto wake ukazimika na Russian Revolution (1917).
Je nchi yetu itaweza kuondokana na tatizo hili tukizingatia kuwa tawala za kiafrika nyingi ni mawakala wa mabepari?
Wednesday, January 02, 2013
MBUNGE MACHACHARI AUAWA UGANDA
Kama ilivyo kawaida kwa siasa za Africa, ukiwa mwanasiasa wa kiafrika, usijaribu kusimamia maslahi ya umma hadi utishie maslahi ya watawala. Watakukolimba, ndivyo inavyooonekana huko Uganda.
Mbunge mwanamke,na kijana mdogo, msichana bado mbichi kabisa CERINA NEBANDA amefariki katika mazingira ya utatanishi mkubwa. Ni mbunge ambaye alikkuwa miongoni mwa kundi la wabunge wa chama tawala NRM waliojulikana kama Rebels au Waasi" kwa ukosoaji mkubwa wa serikali ya chama chao.
Kifo hiki kimeleta msuguano kati ya Serikali ya Museveni na wabunge na inaonekana kuna wabunge wanafanya juhudi kwa serikali kufanya juu chini ili ripoti ya kifo hiki ijulikane kisayansi.
Subscribe to:
Posts (Atom)