
Wengi wataona kuwa hii ni kuingiliwa kwa mambo ya ndani ya Afrika, ni ubeberu mambo leo, na ni ukoloni. Lakini, binafsi naamini si mara zote ukoloni una hasara tu. Ninaamini viongozi kama Ghadafi hawana tija sana kwa jamii kubwa; zaidi wanatumikia "uswahiba". Naamini hata maendeleo yote ya Libya hayajawafaidisha walibya kwa wingi wao,ukiacha marafiki na ndugu wa dikteta huyu.
Pamoja na madhara yote yatakayojitokeza baada ya utawawala wa Ghadafi kuondoshwa, naamini ni bora kuliko kubakiwa na kiongozi wa aina yake katika dunia ya kileo.
Usiku wa leo waasi wameingia Tripoli.