My Blog List

Monday, January 30, 2006

JK ANATANIA TU.

Nakumbuka mzee kifimbo alipong’atuka mwaka 1985, nchi yetu ilikuwa hoi kiuchumi. Mzee Ruksa alikuja kama mkombozi. Wakati huo nasoma shule ya msingi, basi redio Tanzania ilizoea kucheza nyimo kuonesha mwelekeo mpya; nakumbuka kibao kimoja: ‘Usiopowajibika Ole Wako, Utakumbwa na Fagio la Chuma’. Pia kulikuwepo tangazo katika redio kila mara redioni eti: Mdudu rushwa ni hatari na anapiga na anaua’.

Hii yote ilikuwa kuonesha eti Mzee Ruksa kaja na ari mpya dhidi ya rushwa. Matokeo yake utawala wake uliikumbatia rushwa hadi mzee Kifimbo kumkemea kiana wakati Fulani pale Kilimanjaro Hoteli.Baadaye akaja Mkapa na kauli mbiu ilikuwa ‘Uwazi na Ukweli’. Kinyume chake huyu bwana hakupenda uwazi kabisa; ukweli ndio usiseme, waandishi wa habari watakuwa mashahidi hapa.

Sasa kaja Kikwete na kauli mbiu—Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya. Hisia zangu zinaniambia hivi: Kuna hatari haya majigambo tu. Katika uteuzi wake anaonekana kuja na sura mpya nyingi tu. Hii ni habari njema isipokuwa utendaji wao sidhani kama utafanikiwa.

Hii ni kwasababu raisi anapaswa, nafikiri analijua hili kwamba CCM imejaa wala rushwa wakuu nchi hii. Vyombo vya dola, mfano jeshi la polisi limejaa wala rushwa na huu ni utamaduni ndani ya chombo hiki inavyoonekana.

Nilipokuwa natizama hotuba ya JK ya ufunguzi wa bunge niligundua mambo mengi. Wapo wabunge kadhaa walionesha sura za woga na chuki dhidi ya maneno ya raisi. Wengi wa wabunge wazee pamoja na wabunge wanawake kadhaa walionekana kuogopeshwa na hotuba ile.

Kwa mtu yeyote aliyezoea kuishi kiujanjaujanja aliogopa sana. Nani asiyejua wabunge wengi wanalitumia bunge kama tanuri ya utajiri? Nani asiyejua wabunge wengi ni vihiyo ambao hata hawafahamu nchi yao kwa dhati. Mheshimiwa JK anaongea kama vile hajui wapo wazee, vigogo ambao hawashikiki nchini mwetu (untouchable) wamejazana bungeni ili kulinda maslahi yao. Hawa ni kikwazo kwa Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya.

Mwisho niseme tu ninamuunga mkono mheshimiwa JK, ila nina hakika itakuwa vigumu kwake kuleta mabadiliko tunayoyatarajia. Kutamba kwa majambazi ni kielelezo cha kwanza. Ila itabidi raisi awe mkweli tu kuwaridhisha watanzania. Kama waswahili walivyonena: “Bahari haiishi Zinge” nami ninene: JK anatania tu.

4 comments:

mloyi said...

Ari mpya,kasi mpya na nguvu mpya. Imeanza lakini imeshajipiga stop namba wani! kwenye vita dhidi ya ujambazi. Sijui hizo vita nyingine itaingia na style gani? Wawe waangalifu ausiyo itakuwa kama waliotangulia.

Ndesanjo Macha said...

Safi unavyotukumbusha. Kwa uchambuzi wako inaonyesha kuwa "ari mpya na kasi mpya" haijanza na Kikwete. Na kuwa pamoja na hiyo "kasi" mpya mambo huendelea kuwa vile vile.

Nadhani kuna haja ya kuanza kuelimisha umma namna ya kutafsiri kauli za viongozi.

boniphace said...

Huu mtazamo mzuri na unaweza kutumika kama good prediction of what gonna come. Tungoje na tuwape muda maana naona JK kama bado anadhani yuko kwenye kampeni maana kila kukicha anataja matatizo tu wakati ni jukumu lake kuyapa masuluhisho na sisi wananchi kuona utatuzi na sio kutajiwa maana tunayafahamu tayari na yanatuumiza.

FOSEWERD Initiatives said...

Innocent! katika maisha inabidi kuchagua kuwa optimist, au pessimist - la kwanza ukiamini kuwa mambo yatanyooka na ya pili ukiamini mbele ni kweusi! kwa sasa hivi sina cha kufanya ila kumuunga mkono nikiamini nia yake ni njema!! na inaonekana itawezekana! mimi ni optimistic!! kumweka Ngoyai kulia kwake kunanipa imani sana - labda na ufuatiliaji hapa mwanzo mwanzo - tuombe mungu!