My Blog List

Thursday, May 19, 2011

MATAJIRI, WAKUBWA NA KASHFA ZA NGONO



Kwa mfuatiliaji wa mambo yanayotokea duniani, mwezi wa May 2011 umenigusa kwa Kuvunjika kwa ndoa ya Arnold Schwarzeneger, aliyekuwa gavana wa California ambaye amemaliza kipindi chake majuzi. Pia haswa kumenigusa zaidi baada ya huyu jamaa mkubwa wa Benki ya Dunia, Dominick Straus Khan kukamatwa nchini Marekani baada ya kujaribu kufanya ubakaji.
Hawa wote wawili yaliyowatokea ni kwa sababu wameendekeza sana ngono; Arnold yeye hatimaye imegundulika kuwa alikuwa amezaa na mfanyakazi wake kama gavana na kwa miaka kumi (10) alikuwa amemficha mkewe. Naye Straus Khan yeye ni mtu ambaye na kashfa za ngono ni marafiki. Kule Ufaransa wanamwita "hot rabbit" yaani sungura wa moto kwa mabibi, akimpania mtu lazima ampate. Ni kwa hali hiyo ya historia yake lililomtokea na kumsababishia aibu na kupoteza cheo chake cha Ukurugenzi wa IMF ni uzumbukuku wa vigogo na matajiri mbele ya vimwana. Ukisoma historia hii utaona ni jinsi gani hawa mabwana wamedhalilika. Lakini pia kwa marafiki zangu wengi nimewasikia wakibishana sana eti yule mwanadada alitegeshwa na CIA. Jamani, nasema, tuache hisia potofu, binafsi ninaelewa wazungu hawana simile kwenye makosa ya kuingilia maisha ya hasa mwanamke.

6 comments:

Kitoto said...

Bw mkubwa hii blogu yako inanifurahisha kutukuza Kiswahili fasaha. Naona tukiendelea kushambulia kwa maandishi na blog kama yako Inosenti, vita vya fasihi yetu vitaleta ushindi fulani kwa Kiswahili. Miye huwa nnajisikia kama nimechomwa mwiba, nimepigwa konzi au mtu kamtemea mwenzake kohozi pale jamaa atakavyoongea Kiswahili kisha ghafla akarushia Kiingereza uchwara ndani. Ukweli ukichunguza wanaofanya vile si wengi wanaozimanya hizi lugha mbili sawasawa!!!

Simon Kitururu said...

Ukichunguza Bongo waweza kukuta hakuna kiongozi asiye na kashfa kama hizi !

Ila ndio hapo ni mpaka ukamatwe!

Anonymous said...

HAPO BONGO WAPO VIONGOZI WA JUU SANA NA WA KATI NA WADOGO KABISA AMBAO NGONO KWAO NI KAMA SALA.HASA PALE PESA IPO

emu-three said...

Aliye msafi na ampige mzinzi jiwe..wewe....tunazini kila siku kwa macho..wewe...we acha tu!

as issues said...

greetings i am blogger indonesia

nael said...

memberantas.blogspot.com