My Blog List

Saturday, February 26, 2011

SABABU ZA MUSEVENI KUSHINDA UCHAGUZI TENA

Yoweri Kaguta Museveni ameshinda urais wiki iliyopita na hii inathibitisha ataitawala Uganda kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kufanya awe ametawala kwa miaka 30. Katiba ya Uganda ambayo ilibadilishwa na kuondoa ukomo wa utawala kwa kura nyingi za wabunge wa chama tawala ndio inayoruhusu hali hii.
Hata hivyo wananchi nao wanaonekana wanampenda huyu mzee kwani amewatoa mbali sana. Lakini pia ameweza kuwa mwanasiasa anayezungumza mambo yenye mashiko kwa wananchi wa kawaida tofauti na mpinzani wake Kizza Besigye. Hii ndio nguzo yake kuu. Ukisoma makala ifuatayo utaona ni kwanini hasa huyu mzee inakuwa vigumu wananchi wamwache?
Pia wengine wameona kuwa kitendo cha kutojiunga wapinzani kwa pamoja kimewaua ingawa pia hii ingekuwa ni kuua umaarufu wa chama cha FDC.

No comments: