My Blog List

Friday, January 07, 2011

MAUAJI YA ARUSHA

Tukio lililotokea Arusha naamini linaweza kuwa ni kielelezo muhimu katika kujenga msingi wa demokrasia katika Tanzania ya kisasa. Kama tuna uelewa wa kileo naamini katika tukio hili basi kuna haja ya mambo yafuatayo kutokea:
i)Ni sawa kabisa kwa viongozi wa Chadema kufikishwa mahakamani lakini mahakama hiyo iwe huru. Na wahukumiwe kama wana hatia.
ii)Yaanzishwe mashtaka katika mahakama kuu juu ya maisha ya watu waliouawa, jeruhiwa, na hata kuvunjiwa haki za binadamu. Mashtaka haya yawe dhidi ya jeshi la polisi na kwa yeyote ambaye alihusika katika kusababisha hasara au hata kushambulia polisi.
iii)Naamini, ikiwa haya yatafanyika, basi IGP, ARUSHA RPC,WAZIRI WA MAMBO YA NDANI lazima wawajibike na tukio hili.
Kama kweli tunataka mabadiliko ya kweli basi kuna haja ya kampeni maalum za kuwalazimisha watendaji wakuu wa Polisi wawajibike. Vyombo vya habari visilale.

5 comments:

Dadang Sutopo said...

join us survey

Anonymous said...

Ukiachia mbali kuwajibika kwa Jeshi la polisi, hata viongozi wa chadema nao wawajibishwe ktk mahakama hiyo, kwani yote haya yangeepukwa kwa kufuata diplomasia

Simon Kitururu said...

Nakubali kabisa ulilosema Mkuu!

emu-three said...

Hii ingefanyika hivyo, basi HAKI INGETAWALA. Lakini nani wa kumfunga paka kengele?
KUMBUKA: Hii haijaanza leo, hayo ni marudio tu!

HI5 said...

I've been really enjoying this! Well done!