My Blog List

Sunday, September 19, 2010

KAMPENI ZA UCHAGUZI TANZANIA

Nilikuwa kimya sana kwa muda mrefu, sasa nitajaribu kuwalisha watu juu ya yanayojiri juu ya Kampeni za uchaguzi mwaka huu 2010. Tayari Moshi tumeshuhudia bonge la kampeni la kitajiri na vimbwanga vya kila aina vya mgombea uraisi ambaye pia ni raisi wa Jamhuri ya Muungano JK. Hiyo ilikuwa ni wiki hii. Sidhani kama kutakuwa bonge lingine la mkutano kama ule kwa habari nilizozipata.
Wacha hayo, sasa hivi stori kuu ambayo ni ya msingi ni hii kuendelea kukamatwa pembe za ndovu kule Hong Kong kutokea Tanzania. Jamani, mimi nataka niulize, hivi, si ndio sisi tulikuwa tunataka turuhusiwe kuziuza pembe tukawekewa uzibe na majirani zetu majuzi tu, sasa kwa jeuri tumeamua tunaziuza kinyemela au ndio nisemeje?

Pili, kuna hili la Mke wa Raisi jamaa hawataki ampigie mumewe kampeni, mimi naona kama vile kuna ka wivu hivi, hivi ina maana mke wa raisi kutumia mali za serikali dhambi? kwani si ndio mama namba moja eti? Sasa kama yeye ndiye namba moja kwanini makelele wajameji? Hebu someni wake wengine wa maraisi wanavyofanyaga alafu tujiulize hivi kwani mama yetu ana shida gani, si tumuache atumbue kanchi haka masikini?

Wadau nawasikilizia kwa haya mawili.

1 comment:

emu-three said...

Hayo ndio mambo ya siasa ya `umimi', kama ni kwa mwenzakoo haifai, haitakiwi!
Kuhusu Pembe, mimi ndio najiuliza kila mara `utajiri wetu' huu ina maana hatutakiwi sisi wenyewe tuufaidi...angalia madini, angalia umiliki, angalaia mishahara ya wabongo na wenzetu wakuja inavyotofautiana, yaaani sie ni wa beii ndogo tu, hatuthaminiwi kabisaaa