Hii ni globu iliyovumbuliwa nchini Uganda inajaribu kukazia matumizi ya lugha ya kiswahili na kuhabarishana kuhusu maswala mbalimbali ya kijamii hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kat na kwingineko. Siasa na mambo ya michezo na kijamii kwa ujumla ndio itakayokuwa mada kuu hapa.Nitakaribisha maoni yenu.
My Blog List
Saturday, July 28, 2012
OLYMPIC IMEANZA RASMI LONDON
Michezo ya Olimpiki imeanza na Tanzania kama kawaida imepeleka timu ya wachezaji sita (6) tu. Ni kiohoja lakini kama kawaida yetu ndo tulivyo yaani hatuna habari na kuwa serious ila tumebakia kila mtu anawaza kupata fedha tu bila kujali zinakujaje. Nasema hivi kwani nionavyo, sidhani kama tutaambulia kitu katika michezo hii; sanasana tunakwenda kutalii.
Ninaguswa kwani nchi yetu ni masikini sana, ina vijana wengi wamejaa vijuweni hawana cha kufanya ila miongoni mwao wangeandaaliwa nadhani leo tungekuwa na angalau timu ya watu kama mia moja hivi na kwa hakika tungekuwa na uhakika wa medali angalau hata moja.
Napendekeza tubadilike, leo naangazia mchezo wa ndondi, je bondia wa Tanzania atafanyaje? Leo anacheza pambano la kwanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)