Hii ni globu iliyovumbuliwa nchini Uganda inajaribu kukazia matumizi ya lugha ya kiswahili na kuhabarishana kuhusu maswala mbalimbali ya kijamii hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kat na kwingineko. Siasa na mambo ya michezo na kijamii kwa ujumla ndio itakayokuwa mada kuu hapa.Nitakaribisha maoni yenu.
My Blog List
Wednesday, October 10, 2012
MIAKA 50 UHURU WA UGANDA
Uganda imetimiza miaka 50 kwa kufanya maadhimisho ingawa siyo ya mmbwembwe kibao na gharama kama Tanzania ilivyofanya.Museveni ndiye aliyekuwa mwenyeji wa maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Makamu wa Raisi wa Tanzania Dr. Bilali alihudhuria.
Rais Museveni alitangaza jana mambo 10 yatakayoifanya Uganda kuwa Taifa la maendeleo ya hali ya juu kiuchumi miaka mingine 50 ijayo.Pamoja na mambo hayo 10, ni wazi Museveni sasa anaondoka madarakani atake asitake na haijulikani kama mtoto wake ndiye atakayerithi au la.
Thursday, August 16, 2012
KIPROTICH ALIKUWA NA DHAMIRA YA KUTWAA MEDALI OLIMPIKI
Dhamira ya kutwaa medali kwa mwanariadha wa Uganda Stephen Kiprotich yalikuwepo tangu alipoondooka nyumbani kwao Kijijini huko Kapchorwa. Alimuaga mke wake na kumtamkia kkuwa lazima arudi na medali. Dhamira yake inashuhudiwa na mke wake hapa.
UGANDA INAVYOMTHAMINI MSHINDI WA DHAHABU OLYMPIC
Stephen Kiprotich ndiye mshindi wa mbio za nyika (marathon) katika michezo ya Olimpiki ya London iliyokwisha jumapili iliyopita.
Rais Yoweri Museveni amewaongoza waganda kumpokea kijana huyu ambaye anatoka katika familia masikini ya kiafrika kule Kaskazini mwa Uganda eneo la Kapchorwa. Rais Museveni ameweza kuwaalika wazazi wa kijana huyu Ikulu hapo jana na waganda wamechanga fedha nyingi sana kumzawadia kijana huyu.
Kijana huyu ana mke na walikuwa wanaishi kijijini kabisa maisha ya kienyeji kabisa; na ndiye amekuwa akiibeba familia yake wazazi na ndugu zake.Siku ya jumatatu wiki hii kijana huyu aliwasili Kampala na amekuwa akilakiwa kila mahali alipokwenda, hii imejumuisha kukagua gwaride maalum uwanja wa ndege; na kutembelea Ikulu.
Kuonesha jinsi gani Waganda wanamjali mwanamichezo shujaa huyu, gazeti la serikali "New Vision" limeandaa utaratibu wa kumchangia kiasi cha dola za Marekani 500 Milioni kama zawadi kupitia wasomaji wake. Hadi naandika ilikuwa tayari kuna dola 375milioni.
Mimi binafsi Kiprotich amenifurahisha sana na ninadhani ni funzo kwa watanzania vijana kibao ambao wamejazana mitaani eti hawana kazi.
Saturday, July 28, 2012
OLYMPIC IMEANZA RASMI LONDON
Michezo ya Olimpiki imeanza na Tanzania kama kawaida imepeleka timu ya wachezaji sita (6) tu. Ni kiohoja lakini kama kawaida yetu ndo tulivyo yaani hatuna habari na kuwa serious ila tumebakia kila mtu anawaza kupata fedha tu bila kujali zinakujaje. Nasema hivi kwani nionavyo, sidhani kama tutaambulia kitu katika michezo hii; sanasana tunakwenda kutalii.
Ninaguswa kwani nchi yetu ni masikini sana, ina vijana wengi wamejaa vijuweni hawana cha kufanya ila miongoni mwao wangeandaaliwa nadhani leo tungekuwa na angalau timu ya watu kama mia moja hivi na kwa hakika tungekuwa na uhakika wa medali angalau hata moja.
Napendekeza tubadilike, leo naangazia mchezo wa ndondi, je bondia wa Tanzania atafanyaje? Leo anacheza pambano la kwanza.
Saturday, January 14, 2012
AJALI YAUA MBUNGE
Imekuwa desturi sasa kila kunapokaribia kipindi cha bunge, lazima afe mbunge. Hii nyingine tena.
Subscribe to:
Posts (Atom)