My Blog List

Tuesday, March 23, 2010

MNYIKA ANAGOMBEA UBUNGE

Mara nyingi nawaona watu hasa vijana wakionesha dhamira hasa ya kuwa viongozi wa umma. Leo nimekutana na kijana mwenzangu, wa Chama cha Chadema, anatangaza rasmi kugombea ubunge.
Kwa mazingira ya Tanzania, sina hakika kweli kama dhamira yake itafanikiwa iwapo atachaguliwa. Bado mindset/mawazo mtizamo ya watanzania vijana kwa wazee haitamruhusu mtu wa haiba yake kuweza kufanikisha azma yake kirahisi. Kizazi kipya cha vijana wa Tanzania ya leo kimeamua kurithi mtizamo wa wazazi wao: yaani kufanya mambo kwa kufuata hisia zaidi kuliko kwa kufanya uchambuzi wa kina katika kila jambo. Kwa maana nyingine, kama mtu unafikiri sana katika kila jambo unalofanya kama ninavyomfahamu Bwana Mnyika, sidhani kama kweli Bw. Mnyika ataweza Bunge la Tanzania. Watanzania wa leo ni wavivu sana kutumia ubongo, mara nyingi tunatumia mioyo katika kufikiri. Ni jambo la hatari sana na ndio maana watu kama Mnyika wanaonekana na baadhi ya watu kama vile ni vichaa.

Si kwamba ninamchukia ama sipendi Mnyika awe mbunge, ila nataka ajue tu kuwa itakuwa vigumu sana kufikia malengo yake ya kuleta mabadiliko katika Taifa hili changa la Tanzania. Ninamtakia harakati njema.

3 comments:

Anonymous said...

Hakika uliloliongea ni kweli. Ila imefika muda vijana tibadilike, tusiwe wavivu wa kufikiri. Na kwasababu hiyo vijana tunaweza. tumpe nafasi kijana mwenzetu na tumuunge mkono katika harakati za kuleta mabadiliko nchi hii. Pamoja tunaweza tukitumia akili vizuri. Mnyika anaweza. Hatuhitaji mtu mwingine kuona kwaniaba yetu.

Anonymous said...

Mrisho Mpoto anauliza je wewe umepiga kura? sasa niambieni je utawezeshaje kuwafanya vijana kupiga kura na kuhakikisha vijana wanakuwa wengi bungeni ni lazima ujue kama waliokuzunguka wanakubaliana na wewe na wote wamejiandikisha na watampigia kura kijana
Swalilapili tunaijua wazi CCM kama ni wezi wakura je utazilinda vipi kura zako na watu wako?

Anonymous said...

Mnyika namkubali atapita tu leo, na anafaa sana