My Blog List

Thursday, March 26, 2009

JINSI TANZANIA INAVYOMOMONYOLEWA NA MAFISADI

Huwa nasikia kelele kuwa mafisadi wamezidi nchini ila kwa haya ninayoyasoma katika vyombo vya habari basi hali ni mbaya sana. Kwa mfano eti serikali ya JK kumbe inashikwa na familia tisa (9) tu; huwezi amini lakini habari ndio hiyo. La kushangaza zaidi eti hata raisi Kikwete na serikali kujisifu kuwa uchumi ni mzuri kwa sasa kupitia Mkutano wa IMF hivi majuzi kumbe ulikuwa uzushi mtupu.

La kushangaza zaidi, ni kule kuendelea kumkumbatia na kumwacha katibu mkuu wa baraza la mitihani necta kubakia katika madaraka yake huku kazi na utendaji mzima ukiwa umepotea njia. Hebu shangaa eti hata vyeti vinaandikwa kwa makosa na hakuna mtu anayeguswa, hivi huyu mama ana egemeo gani pale? Mwisho kabisa inayonivunja mbavu na ninaisubiri itokee ni hili la kuwa kumbe uchaguzi ujao Mafisadi watatupa raisi.

1 comment:

Anonymous said...

YAH KWA KWELI INASIKITISHA KUONA BARAZA LA MITIHANI KITOVU CHA KUTOA QUALITY KTK ELIMU NCHINI KIMETAWALIWA NA UKABILA NA RUSHWA.

KIBAYA ZAIDI NI PALE TUNAPOWAONA WAFANYABIASHARA WAKUBWA WATANZANIA NDIO WANAOIANGAMIZA NCHINI YETU KWA UFISADI MATOKEO YAKE WAKITUMIA VYOMBO VYAO VYA HABARI KUINGAMIZA NCHI YETU