My Blog List

Saturday, August 11, 2007

SHIRIKISHO LA AFRICA MASHARIKI-- SI HATUA MUAFAKA

Leo nigusie tena juu ya hii jumuiya yetu ya Africa Mashariki (EAC) ambayo watanzania wengi wameikataa kwa kutoa maoni yao kwa tume ya Profesa Wangwe. Nianze kwa kuwafananisha wote wenye ndoto ya kuundwa ama kuharakisha (Fast Tracking) uundaji wa Shirikisho la Africa Mashariki (EAF) hawana tofauti na wapigania haki wa uhuru watanguliziwa bara la Afrika ambao ndoto yao ya Shirikisho la Afrika mpaka leo ni kiinimacho.

Baadhi ya wanaofuatilia mtizamo wangu ni wazi nimekuwa napinga Shirikisho la Afrika Mashariki ila nikiunganga mkono hatua ya Jumuiya tu kwani naamini Shirikisho la Afrika Mashariki itakuwa ni hatua ya kisiasa isiyokuwa na manufaa yeyote kwa mwanachi wa kawaida.

Mmoja wa watu wanaotaka Shirikisho la Afrika Mashariki liharakishwe ni Yoweri Kaguta Museveni--Rais wa Uganda. Aliweza hata kubadili katiba ya Uganda kwa kuwahonga wabunge Shilingi Millioni Tano za Uganda (chini ya shilingi milioni tano za Tanzania) kila mmoja ili tu wapitishe mabadiliko ya kuondoa "ukomo" wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano cha mtu kuwa rais wa nchi. Lengo inasemekana na wachunguzi wengi wa siasa za Uganda likiwa ni ili aendelee kuwa madarakani hadi pale mchakato mzima wa Shirikisho utakapowadia ambapo ataweza kuwa Rais wa kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki ifikapo 2013.

Museveni anaamini Shirikisho ndio njia pekee iliyobakia kutuletea umoja Afrika Mashariki; anafikiri ni rahisi namna hiyo; mwenyewa kwa miaka ishirini na ushehe sasa ameshindwa kuinganisha Uganda sijui Afrika Mashariki itawezekanaje. Hapa pananipa utata sana manake viongozi (wanasiasa) wetu kuna nyakati wanafanya mambo kikondoo sana. Hebu nivute hisia nikumbushe historia ya bara letu la Afrika, ambapo ndoto za waanzilishi wake za kuunda Shirikisho la Kisiasa mpaka leo zimebakia katika vitabu vya historia tu kwa visababu ambavyo hapa kwetu Afrika Mashariki navyo vipo pia.

Moja, mwaka 1958, Osagyefo Kwame Nkrumah alifanya juhudi sana kuinganisha Afrika kwa kuanzia na Ghana na Guinea, ikafuatiwa na Ghana-Guinea-Mali ambazo zote hazikudumu. Pili, kukaja Shirikisho la Senegambia kati ya mwaka 1981 na 1989. Zote hizi hazikudumu sana wala kuweza kusimama; kwa ujumla mashirikisho ya kisiasa yaliyojaribiwa katika karne iliyopita hayakufanikiwa pia si tu Afrika bali hata sehemu nyingine za ulimwengu na mifano ipo mingi: kwa mfano, Shirikisho la India Magharibi (West Indies Federation) kati ya mwaka 1952 hadi 1962.

Nyingine ikawa ni Shirikisho la Kijamaa la Mataifa ya Kiarabu (Federation of Socialist Arab States) kati ya mwaka 1972 hadi 1977 ambapo msisitizo ulikuwa wa kizalendo yaani Pan Arabinism; alafu likawepo lile shirikisho la Yugoslavia kati ya mwaka 1945 hadi 1992; na mfano wa mwisho kabisa ni lile shirikisho kubwa kubwa kabisa la kisiasa wakati wa vita baridi la Urusi ( Union of Socialist States of Russia) la mwaka 1922 hadi 1991.

Unaweza kuona mashirikisho niliyoyataja hapo juu yalianza na kufa kwa sababu mbalimbali ambazo pia zipo hapa Afrika Mashariki. Lakini pia mtu anaweza kujiuliza mbona yapo mashirikisho ya kisiasa ambayo bado wamo na yanaendelea? kwa mfano, Shirikisho la Nigeria lenye watu takriban millioni mia moja na kumi (110) au lile la Ethiopia lenye wakazi takriban milioni sabini na nane (78). Kama kweli Mashirikisho haya mawili ya kiafrika yana tija hasa kwa wananchi wa kawaida ni kwanini basi nchi zote hizi mbili bado ziko katika kundi la nchi zinazoendelea na si nchi zilizoendelea?

Hii ni sababu inayonifanya mimi kutokuunga mkono wazo la Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki. Nikihakikishiwa ni dawa ya kutuondoa kutoka katika nchi zinazoendelea, au zile masikini sana ulimwenguni (LDCs) basi nitaunga mkono; ila kwa hali ya sasa nafikiri shirikisho halina maslahi makini ukiacha matakwa binafsi ya wachache.

Nimejaribu kutizama pia lile shirikisho ambalo nadhani ni mfano wa mafanikio ulimwenguni, nalo ni ule Muungano wa Mataifa ya Amerika ( United States of America) ambalo kisiasa ni mfano wa kuigwa kimafanikio. Je hiki ni kielelezo cha Shirikisho la Afrika Mashariki kufikiwa? Mimi sioni kama ni kweli kabisa: nikumbushe kihistoria ilihitajika takriban miaka mia moja (100)--1776 hadi 1865 pamoja na vita kali na kubwa ya kiraia ya mwaka 1861 hadi 1865 ndipo Marekani ikakomaa na kuweza hata kustawi kama taifa lenye nguvu kabisa ulimwenguni.

Ni wazi kuundwa kwa Shirikisho sio mchakato wa kuharakishwa kama akina Museveni, Kibaki na Kikwete wanavyotaka. Kuna mambo mengi ya kuzingatia hasa ukiangalia EAC ni jumuiya yenye nchi zenye historia ya kupiganapigana katika kila jambo la kisiasa.

Labda nisisitize kuwa si Marekani tu ambapo mambo hayakuwa rahisi kama vile maraisi wetu wanavyotaka tuharakishe kufikia Shirikisho. Niwapeleke katika jumuiya ya Ulaya--(European Union). Kuanzia juhudi za mwanzo kabisa pale uliposainiwa mkataba wa Roma- 1957, kuanzisha Jumuiya ambayo mpaka leo mchakato wa kuunda Shirikisho la Kisiasa umebaki kiini macho. Mwaka juzi tu wanachi wa Ufaransa na Uholanzi walikataa kuunga mkono Katiba mpya ya Jumuiya ya Ulaya kwenye kura ya maoni, ambapo lilikuwa ni pigo katika kukwamisha mchakato mzima wa kufikia Shirikisho la Kisiasa. Tunaweza kuona ni miaka zaidi ya hamsini sasa Ulaya inashindwa kuunda Shirikisho la Kisiasa.

Mambo yote haya niliyoyataja yananifanya niamini kuwa muungano ya kiuchumi ni hatua muafaka ambayo itatufaidisha kiuchumi baada ya kipindi fulani. Nionavyo, Shirikisho la Kisiasa halitaweza kwa jinsi yeyote kuleta faida yeyote kwa mwananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisha wanasiasa wetu. Wanasiasa wetu waache mawazo eti ile kuwa tu na idadi kubwa ya watu basi utakuwa na soko kubwa ambayo ni kielelezo cha nguvu za kiuchumi. Kwa Jumuiya yetu kweli soko litakuwa kubwa ila ni dhaifu sana kiuchumi; ni soko la wateja wengi ila ni masikini sana na ndio hapa nadhani zifanyike juhudi kuendeleza wananchi kielimu na kiuchumi hasa kiujasiriamali (entreprenuership) ndipo tutegemee soko lenye tija. Kinyume chake, hii "uharakishaji" ni usanii mwingine wa watawala kama walivyowahi kujaribu hapo nyuma na kutofanikiwa.

Mwisho ni vyema tuangalie historia ya mashirikisho ya kisiasa katika sehemu kadhaa za dunia ili tuweze kung'amu tufanye nini katika juhudi zetu za kujumuika kimataifa; lisiwe suala la kuharakisha bila kujiuliza je ni kwa maslahi ya nani? Je watawala wanawaza juu ya mwananchi wa kawaida katika jumuiya? Mimi nashangazwa sana na hili zoezi la kukusanya maoni juu ya Shirikisho kufanyika wakati tayari wameshatia saini kuruhusu "kuharakisha mchakato" mzima wa kuunda Shirikisho. Zoezi zima la kukusanya maoni naamini ilikuwa ni ufujaji wa fedha kwani viongozi wetu walishaamua jambo walilotaka kutuuliza; sasa sijue kwanini wanakusanya maoni kwa kitu walichokwisha kitolea maamuzi. Ama kweli tusipokuwa makini tutaburuzwa bila kutafakari.

Namaliza nikisema: "Shirikisho si hatua muafaka"; ila Jumuiya inahitajika kwa sasa yaani mambo ya sarafu moja, umoja wa forodha ni mambo ya msingi yatakayotusaidia kuendeleza wananchi wetu kwa miongo kadhaa labda na ndipo tufikiri Shirikisho tutakapokomaa vya kutosha.

UMOJA WA AFRIKA--USA NI NDOTO NYINGINE ZA ALINACHA

Mwaka 1963, tarehe 25, mwezi Mei, Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulianzishwa rasmi chini ya hekima za muasisi mkuu Asagyefo Kwame Nkrumah. Lengo lake lilikuwa ni kulifanya bara la Afrika kama nchi moja kubwa ambayo aliamini itakuwa na nguvu ulimwenguni dhidi ya hujuma zozote za mabeberu. Julius Kambarage Nyerere, 'mchonga meno' alimpinga vilivyoo kwa hoja yake ya miungano ya kimkoa (regional blocks).

Leo hii, karibu miongo mitano, bado tuko palepale hatujaweza kuamua tufuate hoja ya Asgyefo au Julius. Mwaka 2002, October 15, ikiwa ni miaka 38 ya OAU, viongozi wetu walikutana Durban, Afrika Kusini na kuunda Umoja wa Afrika (AU) mbadala wa OAU. Ilikuwa ni hatua moja mbele kuongeza nguvu za kisiasa na kiuchumi kama hatua moja kuelekea muungano kamili. Mapema mwezi Julai, viongozi wetu wamekutana Accra-Ghana ili sasa waunde Shirikisho la Afrika. Raisi wa Libya akawa kinara na kuivalia njuga hoja ya Nkrumah kuunda Shirikisho la kisiasa (USA).

Mkutano wa maraisi wa Afrika kule Accra unezua tofauti na hali ya sintofahamu sana baina ya viongozi wetu. Kwa mfano, raisi Muammar Ghadafi alikazia sana kuwa shirikisho liharakishwe; yaani, kuanzishwa kwa wizara ya mambo ya nje na ulinzi ifikapo January 2008. Hali hii haikuwapendeza viongoz wengine wengi: Moja, raisi Umaru Yar'Adua alipinga hali ya kuharakisha na akaungana na Nyerere kwenye hoja ya "Mashirikiano ya Kimkoa"(regional blocks).

Mwishoni mwa mkutano ule, ni wazi ilijionesha wazi kuwa Umoja wa Afrika (AU) tulionao umefeli kabisa. Raisi wa kamisheni ya AU, Alpha Oumar Konare wa Mali alikiri kuwa ni chombo kisichokuwa na nguvu kabisa. Alisema lengo ni kufikia shirikisho ila 'mpango barabara' (road map) ya kufikia hapo ni kuwa tumechanganyikiwa na hatujui tufanye nini.

Je tumuenzi Julius Nyerere au Kwame Nkrumah? Hadi sasa wazo la Nyerere linaungwa mkono na wengi wa viongozi waliokutana kule Ghana.

YAWEZEKANA RAISI KIKWETE NI MWOGA!


Kama sijakosea Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mwoga katika kuwachukulia hatua watendaji kadhaa pale panapotokea tuhuma zenye kustahili mtu kuadhibiwa. Hii kusema bei ya mafuta kushindwa kudhibitiwa na serikali ni udhaifu wa Ewura kunanitia wasiwasi sana, kwani raisi anajaribu kutupa mpira. Ninahisi wauza mafuta ni kundi linaloendesha mambo kimafia mafia hivi na lina uswahiba na baadhi ya vigogo wenye nguvu (untouchables).

Serikali inaogopa kuwagusa na inarusha mpira kwa Ewura iwashughulikie situ ambacho nadhani Ewura hawataweza. Kuna uwezekano serikali yetu imeshanunuliwa na hawa mafia wa mafuta ndio maana wanaogopwa na wanajipangia bei watakavyo. Kama sivyo, basi serikali ijaribu kufanya yale iliyofanyiwa Shirika la ndege la Uingereza wiki hii kwa kupigwa faini dhidi ya kupanga bei ghali kuwanyanyasa wasafiri. Nitaeleza juu ya muono wangu huu wa labda raisi wetu ni mwoga mwishoni mwa waraka wangu wa leo; ila kwanza nigusie hisia zangu kadhaa pale nilipobahatika kumuuliza Raisi Kikwete maswali mawili wakati akihojiwa na shirika la utangazaji la VOA la Marekani hivi majuzi.

Kwa miaka sita sasa nimekuwa mfuatiliaji wa kipindi cha mahojiano cha redio na televisheni "Straight Talk Africa" kinachorushwa na shirika la utangazaji la Sauti ya America (VOA) na kuendeshwa na mtangazaji Shaka Sally. Hivi karibuni pia nimekuwa pia mshiriki na nimepata nafasi kutoa ama kuuliza maswali juu ya mada zilizokuwa zikijadiliwa. Wiki hii, yaani tarehe 1/8/2007, Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ndiye mgeni akihojiwa kutoka Dodoma. Washiriki tulitakiwa tutume maswali mapema kwa barua pepe. Nilifanya hivyo ili nipate nafasi ya kipekee kumuuliza Raisi swali juu ya mustakabali wa nchi yetu. Na kwa bahati nzuri kabisa, maswali mawili ya kwanza yalitoka kwangu; yalihusu wasiwasi wangu juu ya mchango wa sekta ya madini kwa uchumi wetu. Mheshimiwa Raisi alinijibu na nikaridhika hasa swali la kwanza ila sehemu ya pili kidogo kutokana na uhariri uliofanywa na Shaka Sally, sikuridhika na jibu la mheshimiwa Raisi.

Swali langu la kwanza nilitaka mheshimiwa Raisi lilikuwa ni kwa vipi ametimiza ahadi yake ya kuipitia upya mikataba ya madini iliyosainiwa na serikali iliyopita ili sasa ituletee tija? Raisi alijibu vyema kwa maoni yangu na napenda nimshukuru sana kwani alieleza makubaliano kati ya serikali na makampuni mawili: Barrick Gold na Resolute Mines, kuwa sasa yanalipa kwa takriban asilimia 33% ya kodi ikijumuisha pia na mrabaha.Na akasema kuwa kiwango cha dunia au kimataifa ndio hicho kinachotumika katika nchi nyingine. Raisi aliahidi kuwa kuanzia sasa mchango wa makampuni ya madini itakuwa asilimia 33% na si tena yale mambo ya 3%.

Swali langu la pili ambalo mheshimiwa Raisi Kikwete hakuniridhisha kwa majibu na ningependa kama inawezekana atoe ufafanuzi zaidi pindi akipata wasaa niliuliza: Je ni kweli Tanzania hatuna uwezo wa ndani wa kuweza kuzalisha madini hadi hatua ya mwisho na badala yake tunauza nje madini katika hatua ya malighafi?

Raisi alijibu kuwa hatuna nibu la ndani kwa hili na imetubidi tutegemee mitaji ya nje ya kimataifa kama hali halisi inavyodhihiri. Binafsi, nilitegemea ajibu hivyo kwani si mara ya kwanza kusikia viongozi wetu wakisema hivyo. Jibu hili linanisumbua sana na litaendelea kuniuma roho labda mpaka atakapotokea mtu anipe maelezo fulani ambayo sidhani kama huwa yanazingatiwa tunaposema eti nchi ya miaka arobaini na zaidi ya uhuru haina uwezo wa kuuza rasilimali zake katika thamani stahili kupata faida halisi. Je ni kwanini nasema hivi?

Ili nimtendee haki Raisi Kikwete, labda nioneshe swali langu ambalo Shaka Sally alilihariri lilikuwa hivi: Je ni kweli Tanzania hatuna uwezo wa teknolojia au kitaaluma kutengeneza madini ya nchi yetu hadi hatua ya mwisho? Kama ni kweli, ni nini maana ya kuwa na idara ya Geolojia kwa mfano pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam? Ina maana kwa miaka yote ya uwepo wa idara hii imekua ikifanya nini kama imeshindwa kutupatia wataalam katika sekta ya madini?

Manake kwa hoja ya kutegemea mitaji kutoka nje, inamaanisha chuo chetu kimeweza tu kutuzalishia wataalamu wa kusaini mikataba bila kuzingatia maslahi ya nchi, hii ni hatari kwa elimu yetu kwani haikidhi haja ya kuzalisha wasomi wazalendo, kweli tumekwisha. Nimpongeze mheshimiwa Raisi alishang'amua hili alipokuwa ziarani kule nchi za Nordic.

Nikiacha maswali ambayo niliyazua binafsi, niseme tu mahojiano ya Raisi yalikuwa mazuri sana na ya uwazi wa dhati. Kwa mfano, Raisi Kikwete akijibu swali la Juma Iddi, juu ya "Kupaa kwa Uchumi Wetu", Raisi aliweka wazi kuwa kwa sasa tuko kwenye mchakato tu na kusema Uchumi unapaa ni mapema sana. Alitumia kauli: "We are yet to see the trickle down". Hapa Raisi Kikwete aliifunga ile hoja ya majibizano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu na waandishi kadhaa katika gazeti hili la Tanzania Daima.

Raisi aliulizwa na Shaka Sally juu ya Visheni yake kwa Taifa: Alisema lengo lake kuu ni kuona Tanzania inaondoka kutoka kundi la nchi masikini kabisa (Least Developed Countries) hadi kuwa kati ya nchi za pato la kati (Middle Income) mara moja ifikapo 2010. Hapa mkazo ataweka kwenye Kilimo na Miundo Mbinu. Na ndio hapa Raisi Kikwete alipoungana na akina Padri Kitambo, Mwanakijiji na Malera kuwa kusema 'uchumi unapaa si kweli kabisa'. Kwa visheni ya Raisi Kikwete, tutegemee ndege itaanza kuwasha injini zake ifikapo 2010; kwa sasa iko gereji ikishughulikiwa.

Shaka Sally alitaka kujua kuwa tangu Raisi Kikwete awe raisi ni jambo gani au uamuzi gani mkubwa na muhimu anaweza kujivunia kati ya mengi aliyokwishafanya? Alisema ni upanuzi wa elimu ya sekondari ambapo asilimia 96% ya wanafunzi wameandikishwa shuleni. Ila alikiri kiwango cha elimu kinachotolewa hakina viwango madhubuti. Na alikiri ni changamoto iliyobakia kuboresha ubora (quality) akitumia neno 'tall order'. Hapa raisi Kikwete alinikuna kwa kuwa mkweli kwani ni kweli kabisa kunahitajika kazi ya ziada; yaani walimu bora na zana bora.

Jambo lingine Raisi Kikwete aliulizwa: je ni nini kinaichoisumbua sana roho yake tangu awe Raisi katika majukumu yake? Jibu la Raisi lilinipa hisia mchanganyiko; kwani raisi alisema kuwa pale anapomuondoa mtu kutoka kwenye madaraka yake amegundua imekuwa ikiambatana na habari za uzushi zaidi na si ukweli. Kwa maana nyingine majungu ni mengi sana anayofikishiwa Raisi wetu. Na ndio maana amesisitiza katika kikao cha NEC kilichomalizika hivi karibuni kuwa tuhuma zozote dhidi ya watendaji ziambatane na ushahidi.

Hapa napata hisia raisi wetu labda hajui kwa nafasi aliyopo majungu lazima yawepo mengi sana; ila kwa kiongozi ni lazima mtu ujifunze kuamini hisia zako pale unapopata jambo na kulitafakari. Kwenye mambo ya utawala kuna kitu kinaitwa "INTUITION" yaani hali ya kung'amua jambo lisilohitaji kufikiri sana na kiongozi unachukua hatua stahili.

Raisi amenishtua kidogo labda hana karama za kiuongozi za kutosha. Kwani kama ni kweli anaumia roho kwa kugundua baadhi ya mabadiliko ya viongozi aliyofanya hayakustahili kwa ajili ya majungu; basi inamaana kuwa hii kuongezeka kashfa kila kukicha na Raisi anakaa kimya labda pia anaumia roho?

Nitoe mifano michache ambapo kashfa zisizohitaji hata mtu kufikiri na kuchukua hatua dhidi ya wahusika: hivi waliosaini Richmond, Kashfa ya Minara ya BOT au hii ya hivi majuzi mtu kwenda kusaini mkataba na kampuni ya madini huko ughaibuni kinyume na taratibu tulizojiwekea ni mambo ya majungu kweli? Raisi Kikwete acha woga, usiumwe roho; chukua hatua, bila maamuzi magumu hasa kutoka kwako nchi hii haitajengwa wala kwenda mbele.

Visheni yako haitafikiwa hata kidogo ukiumia roho kwa kupima majungu, wajibisha watu kwa ujasiri. Angalia hisia za wananchi juu ya kashfa mbalimbali alafu chukua maamuzi kuwaadhibu waliokuzunguka ambao wanakosa kila kukicha wakijua hawafanywi kitu. Woga wako utalifikisha Taifa hili katika siasa za kiushirika vikundi (patronage au cronyism) kama utajaribu kupima uzito wa majungu yanayoambatana na kashfa kadhaa. Si ulishasema huna ubia na mtu; sasa ukiumia roho dhidi ya maamuzi yako hii itapalilia "ubia".

Mwisho, nitoe hongera kwa mheshimiwa Raisi kwa mahojiano yale na VOA; Mungu Ibariki Tanzania iwe na viongozi majasiri wasio waoga na wenye kutenda badala ya kutoa sababu kwa kila jambo lililo ndani ya uwezo wao.

DRC-UGANDA VITANI?

Kuna mgogoro wa mpaka kati ya Uganda na Congo-DRC.Kiini ni kisiwa kimoja ndani ya ziwa Albert ambapo pia kinahusishwa na uwepo wa mafuta. Mgogoro huu unakuwa na kuna mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi mbili hizi.
Kuna habari za wanajeshi wa Kongo kuwavamia wa Uganda mpakani.

Saturday, August 04, 2007

LIGI YA UINGEREZA YAANZA

Msimu mpya wa ligi ya Uingereza unaanza na kwa wale wapenda soka, mambo mtindo mmoja. Kesho mechi ya kufungua pazia itapigwa kati ya Chelsea na Man United. Utabiri unaonesha huu ni mwaka wa Chelsea au Liverpool kwa nionavyo japo Arsenal nina shaka wataonesha maajabu. Huko Uganda, chama cha soka kinafanya mabo kibiashara ambapo ligi ya Uganda itaoneshwa runingani.
Sasa ligi inaanza na utabiri unaonesha ni mwaka wa timu zilezile za msimu uliopita.
Huko Hispania kuna uvumi kuwa Barcelona kumwongeza Henry haitafua dafu kiushambuliaji kabisa.

Ukiacha soka kuna mambo ya personality yamenikuna kidogo. Alafu kuna hii hali ya Zimbabwe inakuwa mbaya kila kukicha na inaonekana Robert Mugabe kaamua kukomalia urais.

Wednesday, July 25, 2007

SHIRIKISHO LA AFRIKA MASHARIKI NI UTAPELI WA WATAWALA

Kamusi ya Kiingereza na Kiswahili inafafanua neno "MYTH" kama uwongo, jambo lililobuniwa na pia likimaanisha ngano. Mimi napenda nitumie neno 'ngano' kujenga mada yangu.

Kwa wale waumini wa dini mbalimbali neno 'Ngano" halitakuwa jipya kwani misaafu ya dini zote imejaa ngano za kila aina ambazo zinasaidia hasa wahubiri kufikisha ujumbe pale wanapohitajika kuhakikisha kuwa kondoo wa bwana hawapotei njia. Ninatizama Shirikisho la Afrika Mashariki ambalo hivi majuzi watanzania takriban 75% wameamua kulikataa hasa ule mpango wa wanasiasa wetu wa kuharakisha kufikia shirikisho itakapofika mwaka 2013. Binafsi siamini kuwa ni busara kuwa na shirikisho ila tu naunga mkono wazo la Jumuiya kama ilivyo sasa hivi ikiimarika kila kukicha kama taasisi itakayosaidia sekta ya uchumi kukua na urahisaji wa biashara miongoni mwa nchi zetu.

Shirikisho la Afrika Mashariki sio la lazima wala jibu toshelezi katika kupambana na umaskini. Kama lilivyokuwa tukio la uhuru katika miaka ya 1960 ambapo tunashuhudia nchi zetu zikiendelea kuwa katika kundi la nchi masikini zaidi ulimwenguni. Hali ya uchumi ni mbaya na nafikiri tutegemee pia ndivyo itakavyokuwa katika muungano wa kisiasa; kwani kwa mawazo ya uongozi tulionao hadi leo hii, kifikra si watu wa kutufikisha katika maendeleo. Bado mawazo yetu wengi tunafikiri kuwa kiongozi basi ni kujilimbikizia mali binafsi na familia pamoja na rafiki zetu.

Kwa kipindi chote cha ukusanyaji maoni ya wananchi juu ya kuharakishwa na pia kujua kama wazo la shirikisho ni muafaka, nimejaribu kutafakari maoni ya watu wengi na nikajiuliza swali: Hivi ni kwanini wanasiasa wetu wanatudanganya sana wanapotetea shirikisho au hata jumuiya kama ni jibu la umasikini,eti wigo wa soko utaongezeka na maisha bora yataibuka?Ndio hapa ngano ya Shirikisho inapoanzia; ni kweli, Shirikisho litakuwa na soko takriban la watu zaidi ya milioni mia moja. Hili ni soko la pili kwa ukubwa nadhani hapa Afrika ukiacha lile ya shirikisho la Nigeria lenye watu zaidi ya milioni mia moja arobaini na ushehe.

Pamoja ukubwa wa soko la Nigeria, bado watu wengi-wateja wa soko-ni masikini wa kutupwa sawa na hapa kwetu. Kimahesabu, "sifuri ukijumlisha sifuri ni sawasawa na sifuri". Unategemea masikini anunue nini kama tunatetea hoja ya wigo wa soko? Bila hatua madhubuti kwa kila nchi kuwezesha wananchi wake kuwa na nguvu za kushiriki kwenye soko ni bure kabisa. Hatuhitaji shirikisho manake hao wanaongoza nchi zao ambao wameshindwa kuwawezesha wananchi wengi kutoka kwenye umasikini, ndio haohao watakaotuongoza katika shirikisho. Je wana lipi jipya kukabiliana na dola kubwa la shirikisho ukiachilia mbali kushindwa kwao kwenye serikali zao ndogo?

Nadhani tunahitaji tu jumuiya kama ilivyo sasa ili ichochee kuondoa umasikini na wala si shirikisho. Naamini kuwa si sahihi kuwa ukubwa wa eneo au wingi wa watu ni kigezo cha kuwa na nguvu za kiuchumi. Turejee vitaifa vidogo vidogo kama Uingereza, Ufaransa, Japan na tujiulize je wana ukubwa wa hata Tanzania? Au yapo mataifa yenye hadhi ya kuitwa bara kama vile: Antarctica na Australia pamoja na ukubwa wao bado si mataifa namba moja kwa utajiri au maisha bora ulimwenguni. Nasema hii ni ngano ya wanasiasa kutafuta ofisi za kuendeleza maisha yao labda.

Nikitizama upande wa faida ya uwekezaji kutoka nje (FDI) ambazo tayari zinajionesha katika kila nchi kwa sasa ni wazi kuna faida bila kutegemea shirikisho. Tuangalie mashirika mbalimbali ya kikanda kama vile ASEAN la bara Asia, COMESA na hata SADC utaona ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa uchumi na biashara bila mfumo wa shirikiso katika nchi husika. Hivi Botswana au Mauritius chumi zao zinastawi sana kwa ajili ya Shirikisho au utawala bora? Ni wazi tuna tatizo la utawala na usimamizi wa rasilimali zetu na kama ni hivyo hata lije Shirikisho ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Inaonekana hatujui tatizo letu Afrika Mashariki sio kuongeza soko; tujitizame kwanza, la sivyo tutahamisha matatizo ya utawala mbovu kutoka vijinchi vyetu hadi kwenye Shirikisho.

Naamini hata kama Shirikisho litaundwa, bado serikali za ndani za nchi zetu zitabakia na hatamu ya kuvutia uwekezaji ili kutoharibu hali ya uchumi wa nchi zetu. Kwa mantiki hii tuturajie serikali hizi kuendelea kutoa misamaha ya kodi na hata ruzuku kuvutia wawekezaji ili kuzuia kuachwa nyuma. Sasa hapa Shirikisho ni kama mzigo tu wa kuongeza gharama za kiuendeshaji. Ninapowaza jinsi viongozi wetu wanavyopenda minjonjo ya ukubwa napata taabu sana kuelewa ni nini hasa lengo la kupigia mbiu Shirikisho. Naona kama vile ni kwa matakwa yao binafsi na wanatudanganya wananchi ndio maana naliona wazo la Shirikisho kama "ngano".

Jambo la msingi ni kuwa hata katika jumuiya nyamafu kama ya sasa ya EAC, haitawezekana kuleta maendeleo ya kiuchumi na kufuta umasikini katika jamii ambayo asilimia hamsini ya wananchi bado wanaathiriwa na malaria; nusu ya watoto wana kwashakoo na theluthi moja ya wanawake wanakufa kwa gonjwa la kuepukika kama ukimwi. Sioni ni kwa vipi shirikisho la kisiasa litaweza kuondoa madhila haya. Hatari iliyopo ni kutuongezea gharama za kuendesha shirikisho hasa za viongozi --mamwinyi--waliopania kujipandikiza ili kutawala eneo hili kama himaya yao na watoto na marafiki zao.

Kabla sijamaliza mada yangu, hebu tujiulize juu ya faida za Shirikisho la Afrika Mashariki kama zipo? Je Shirikisho hili linalotakiwa na watawala wetu litampa faida mwananchi wa kawaida? Na je katika "anga za kimataifa" tutakuwa na sauti kubwa ya kisiasa katika kada na duru za kisiasa za ulimwengu huu wa utandawazi? Je shirikisho litaweza kutukwamua dhidi ya "utegemezi wa wafadhili au wahisani?" Jibu naliona ni hapana: kwa taarifa tu ni kwamba yale mashirika makuu ya kiuchumi ulimwenguni kama Benki ya Dunia (World Bank), Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) na hata Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) yanatoa mgawanyo wa nguvu za maamuzi kwa nchi au mataifa kupiga kura katika kufanya maamuzi mbalimbali kwa kuzingatia GDP.

Tukilitizama Shirikisho kama litaundwa ni kwamba litakuwa na GDP ya kama dola 30 bilioni sawa na asilimia 8% ya nchi ya Afrika Kusini. Kimsingi na kiutaratibu haitaweza hata kutimiza sharti la kutoa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB). Tutaendelea kushikilia kiti kimoja katika Benki ya Dunia pamoja na nchi nyingine ishirini na mbili (22) za Afrika kwa kupokezana. Dunia ya leo bila kuwa na nguvu ya maamuzi ni kwa vipi tutajikwamua hali kandamizi kadhaa ambazo mataifa yenye nguvu yananyanyasa mataifa makubwa? Ni kutokana na muono wangu huu napatwa na hisia labda viongozi wetu hasa wanavyopigia debe hii ngano iharakishwe basi ni uzushi tu na usanii na si kwa maslahi ya uchumi bali ni maslahi binafsi labda.

Nawaona wanasiasa wetu katika mtizamo wa mnyama kondoo; hasa pale anapokuwa anapelekwa machinjioni na wala hajui kifo chake. Wanasiasa wetu hawatizami mbali katika utendaji wao mara nyingi. Nchi zetu tusipokuwa makini nahisi tumetekwa nyara na sera za kizamani za kiuchumi ambazo hazikidhi haja ya jamii kwa ujumla bali kwa matakwa binafsi zaidi. Wenye kuona mbali wamebaki tumechanganyikiwa ni kwa vipi bado barabara zetu ni mbovu, hakuna huduma bora hospitalini na bado kuna wanakijiji wanalala nyumba za majani na udongo miaka zaidi ya arobaini ya uhuru.

Je tiba ya haya ni shirikisho? Mimi siamini kabisa, ndio maana sitaki Shirikisho naona hii ni ngano ya wanasiasa katika kutudanganya kama watoto kwa maslahi yao zaidi; ni 'utapeli wa watawala' ila tu Jumuiya tuliyonayo hadi sasa ni hatua muafaka.

NANI ATAMRITHI MUSEVENI?

Kama kuna mtu pekee ambaye anaweza kumruthi rais Museveni siku za usoni ni mheshimiwa Amama Mbabazi. Museveni aliwahi kusema huyu ndie pekee 'presidential material' na sasa yeye mwenyewe kathibitisha. Lakini inasemekana Museveni kukaa madarakani muda mrefu kunamfanya sasa kununua umaarufu kwa kutumia pesa kuwarubuni wapinzani warejee NRM.Hata aliyekuwa katibu mkuu wa EAC, Amanya Mushega ambaye wametofautiana kwa muda mrefu sasa anatafuta njia za kurejeana japo inasemekana ni vigumu. Lakini pia rafiki na swahiba wa Museveni naye kaanza kumtenga bosi wake.

Kufuatia kuibuliwa kwa kashfa ya ngono ya yule askofu mkosoaji sana kule Zimbabwe, Pius
Ncube, inasemekana huu ni mtindo wa "Big Brother". Chama tawala Uganda kimependekeza kuanzishwa kwa mafunzo ya kijeshi kwa kila mwananchi kwa lazima; je ndio mwanzo wa vita Uganda?
Nchini Uganda kumetokea walokole ambao wanajitajirisha kwa jina la Yesu. Je umasikini ni kujitakia?

Mwisho kweli Uganda bado nchi ya kijeshi, makada wa chama tawala walikutana majuzi; ona mambo yaliyojiri na vituko vya waziri mmoja msomi.

Saturday, July 21, 2007

Kweli haya ni mambo makubwa, yaani Robert Mugabe anatumia mbinu chafu za akina Museveni kumchafua Askofu Ncube ambaye anampinga sana.

MU 7 HANA LENGO LA URAIS WA EAC

Rais Museveni ameamua kukanusha eti ana maslahi katika jumuiya ya Afrika Mashariki, yaani anataka kuwa Rais wa kwanza kama inavyosemkana licha ya hivi majuzi kufanya ziara kwa gari katika nchi zote tatu.
Pili kuhusu jumuiya ni vyema tukamfahamu spika wa sasa wa bunge la jumuiya.

Monday, July 16, 2007

HATUHITAJI SHIRIKISHO ILA JUMUIYA INATOSHA--EAC

Ripoti ya maoni ya wananhi wa Tanzania imetoka na ni wazi wananchi wengi wana woga mkubwa na hawataki shirikisho.Binafsi sitaki shirikisho ila tu napenda tuwe na jumuiya kwani nadhani Shirikisho ni maslahi ya wanasiasa tu na kwa mwananhi wa kawaida si tija.

Lakini pia, kama mtanzania, mimi ni mmojawapo wa wale wasioridhishwa bado kama kweli tunahitaji kuwa na shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) .Ukiusoma mkataba wa kuanzishwa kwa EAC unaeleza kinagaubaga mtiririko mzima unaopaswa kufuatwa na nchi wanachama ili kufikia shirikisho.

Yanayotokea kwa kipindi hiki, kidogo yananishangaza hasa "uharakishwaji wa kupata shirikisho" fast traking.Kwenye mkataba wa jumuiya-mataifa shirika-Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi-yanawajibika hatua kwa hatua, taratibu; yaani kwanza, muungano wa mapato(custom union), pili, soko la pamoja(common market), tatu, sarafu moja(monetary union) na mwisho Shirikisho la Kisiasa(Federation).

Lengo la mchakato huo ni ili kupata ushirikiano makini wa kiuchumi ambapo watu wenngi masikini wataweza kuishi na kumudu maisha ya kiwango cha juu katika eneo hili. Inapowezekana kunyanyua kiwango cha maisha cha raia wengi masikini basi shirikisho linakuwa linawezekana. Shirikisho lingetakiwa lifikiriwe katika kipindi kifupi hadi 2013 kuweza kuzibadili taasisi mbalimbali za kitaifa katika mataifa shirika ziwe chini ya mtandao mmoja wa shirikisho.
Sioni itawezekanaje katika kipindi kifupi hadi 2013 kuweza kuzibadili taasisi mbalimbali za kitaifa katika mataifa shirika ziwe chini ya mtandao mmoja wa shirikisho. Hebu nitoe mifano michache:

Moja, Nchi ya Kenya iko tayari kwa shirikisho kwani ni njia mojawapo ya kuimarisha zaidi nguvu yake ya kiuchumi na kibiashara. Uchumi wa Kenya inasemekana ni karibu asilimia 50% ya uchumi wa Uganda na Tanzania kwa pamoja. Pili, ukienda Uganda na Tanzania hapa pia kuna kiini macho. Taarifa za kiuhumi zinaonesha kiwango kidogo cha biashara kati ya nchi hizi mbili. Kwa mfano, Uganda Bureau of Statistis-2004 zinaonesha mwaka 2003 Uganda iliuza bidhaa za thamani ya dola 78 millioni kwa Kenya, alafu ikauza dola 5.8 milioni kwa Tanzania.
La kushangaza kabisa ni kwamba mwaka huohuo Uganda iliuza bidhaa za thamani ya dola 13.7 milioni kwenda Sudan ambayo sio nchi mwanahama wa EAC.

Ninachokiona hapa kuna hatari inakuja hapo baadaye: Uganda inafanya biashara zaidi na Sudan kuliko Tanzania. Tukumbuke mwaka 2003, Sudan ya Kusini bado ilikuwa itani; sasa hii hali imebadilika kabisa hali ni shwari, na mpaka 2011 upo uwezekano wa Kusini mwa Sudan kuwa taifa huru.

Na kwa hali iliyo sasa biashara kati ya Uganda na Sudan itakuwa sana na wala Uganda haitahitaji nchi kama Tanzania kibiashara kabisa. Haya yote yameshaanza kutokea sasa. Kwa ushahidi tu, mtu aende kushuhudia ni malori mangapi yanapita usiku na mhana yakiwa na shehena ya bidhaa kutoka Uganda na Kenya katika barabara ya Yei hadi Juba.

Uchumi mzuri unapimwa na biashara, na kama ni hivyo je shirikisho la nini?Jumuiya inatosha kwani vikwazo vyote ya biashara vitaondolewa. Shirikisho ni mzigo kwa wanasiasa kutafuna kile kinachozalishwa na faida ya jumuiya kwa kuwakirimu wanasiasa na misafara yao ya kifahari.Nawaunga mkono wananchi kukataa shirikisho ila nasisitiza Jumuiya ni muafaka.

Saturday, July 14, 2007

LEO NI "BASTILE DAY"

Nchini Ufaransa leo ni siku ya kukumbukwa na kutafakari: "BASTILE DAY"

Wednesday, July 11, 2007

KAMPENI ZA MUSEVENI EAC ZAANZA?

Katika kile kinachoelezewa na baadhi kama kampeni ya Rais Museveni kuzunguka kwa gari nchi za Afrika Mashariki ni kampeni za kutawala eneo hili, basi jana Museveni alidhuru kaburi la Mwalimu Nyerere, nadhani kupata baraka za mzee.

Museveni kapita miji ya Busia, Kisii, Migori, Isbania, Mwanza hadi Butiama katika juhudi za kujitambulisha kama mfalme mpya wa kaya ajaye.Inasemekana hata mkewe aliwahi kusafiri kwa basi kutoka Kampala hadi Nairobi.Kuna hisia jamaa amepania uraisi wa Shirikisho la EAC na mkewe atamrithi kule Uganda. Ziara yake haikuweza kumalizika kwani kutoka Musoma ilimbidi apande ndege ya serikali ya Tanzania kurejea kwao kwani barabara hazifai.

Haya yakitokea, kwenye chama chake NRM, kuna makundi ya kisirisiri kama yale ya mitandao ya CCM.


Ama kweli duniani kuna mambo, kumbe bado usodoma na ugomora upo makanisani?

Mwisho nimalize na tahariri ya kuitetea NGO : HAKI ELIMU kwani waheshimiwa wetu na akili zao mgando hawaitaki kabisa. Napenda sana kazi yake.

Saturday, July 07, 2007

UJAMBAZI SASA UGANDA

Tanzania ni nchi ya usiri sana hasa juu ya masuala ya ujambazi lakini Uganda ni wazi kwani mtu unaweza kuwajua hata kwa sura majambazi gazetini.

Wednesday, July 04, 2007

UNITED STATES OF AFRICA-KIINI MACHO

Bara la Afrika kuwa nchi moja itabaki kuwa kiini macho milele.Mkutano uliomalizika karibuni viongozi wetu hawakuwa tayari kukubali wazo hili linalopigiwa chapuo na Ghadafi. Wengine wanatuambia kuwa ni wazi waafrika tumepotea njia hadi tutakapokubali kuwa na namna yetu ya kufanya mambo dhidi ya wazungu.

Hivi kuna sababu na haja ya kuharakisha jumuiya ya Afrika Mashariki?Pia ni vizuri tujue ile ripoti ya kiuchumi ya nchi za Mashariki ya Afrika inasemaje.
Habari ya kuvuti huko Uganda ni hii ya kubadilishwa kazi yule mlinzi au msaidizi wa Rais Museveni baada ya kumuumiza rais na sasa kuna mlinzi mpya.Hiyo ni burudani tosha ila kuna hii hadithi juu ya yale mapinduzi ya mwaka 1971 yaliyofanywa na Idd Amin.

Monday, July 02, 2007

MUSEVENI MTOTO MAFUNZO ZAID YA KIJESHI MAREKANI

Museveni anazidi kumuongezea ujuzi wa kijeshi mwanaye, je anamuandaa kumrithi?

Thursday, June 28, 2007

AMINA CHIFUPA KAUAWA--KIFO HIKI KICHUNGUZWE


Juzi usiku saa tatu na dakika kumi napokea sms kutoka kwa mtu fulani wa karibu aliyepo Dar es salaam ikiwa na maandishi ya herufi kubwa: AMINA CHIFUPA KATUTOKA, AMINI USIAMINI. Mara nasikia pia tangazo redio free afrika juu ya hili. Basi naamua kumuuliza huyu bwana ninini maoni yake?

Anajibu: WAMEMUONDOA KISAIKOLOJIA. TANZANIA HAIHITAJI MAJASIRI!NCHI HII NI BORA KUWA KIMYA TU! KAA NA FAMILIA YAKO KAMA UKIONA WATU WANA ISHU CHAFU ACHANA NAO! HAIKUHUSU. LEO NDIO MAADHIMISHO YA AGAINST DRUGS NA SHUJAA AMEONDOKA! IPO SIKU WATU WATACHOKA NA HAPATAKALIKA! IMENIUMA KUPITILIZA.Ni maneno mazito ambayo hata mimi yaliniingia hasa lakini naamini ni lazima wapiga filimbi(whistle blowers) waendelee kuwepo. Hisia zangu ni nyingi hasa kulihusu bunge letu. Nitaeleza kwa mujibu wa mambo yaliyojitokeza baada ya msiba huu.

Amina ni mtu anaelezewa na walomfahamu kama mtu aliekuwa na upeo ambao ulihitajika nchi hii.Ila wengine kuona anafariki katika hali isiyoelezeka kwa mtu mwenye akili timamu wanathubutu hata kukilaani chama cha mapinduzi japo mie nadhani tuna tatizo la utamaduni wa kutokubali kuelezwa ukweli.Wengine wamemfananisha na Princes Diana hata pia wengine wakafikia kusema siku ya madawa ya kulevya iitwe jina lake kitu ambacho sidhani kitasaidia kwa nchi kwani ni zaidi ya hapo ndio tutaweza kumuenzi: yaani kuwa mashujaa kupambana na umafia bila kuogopa ufa hadi bila kujali kufa kama Amina ndipo tutaikomboa nchi yetu dhidi ya umafioso wa baadhi ya watu.

Kwa ufupi nafikiri mhariri wa gazeti la serikali hakukosea,AminaChifupa alikuwa ni taa iliyopotea.Huko Dodoma wabunge wetu walionekana kwenye runinga wenye simanzi ila sina hakika kama ilijkuwa ni kweli ama ni unafiki tu. Nasema hivi kwani mimi naamini chombo kama bunge kingeweza kutoa msaada mkubwa sana wa ushauri nasaha wa kitaalam kumuokoa dada hyu dhidi ya hali ngumu aliyokuwa akikabiliana nayo.

Sijui kama kuna akina mama wabunge walijipenyeza hadi kuona Mbunge huyo alikuwa akiendeleaje hadi alipozidiwa.Wananchi wengi nikiwa mmojawapo naamini kabisa ile kauli ya Amina dhidi ya uuzaji wa dawa za kulevya ndio chanzo cha hii sukari tunayoambiwa imemwondoa, kwani imemsababishia mahangaiko na fedheha (depression) mengi ya ndani hasa pale ilipopelekea hata ndoa yake kuingia matatizo.Spika wa bunge na katibu wa bunge nadhani wana deni kutueleza: je walichukua hatua gani kumsaidia mbunge huyu hasa baada ya matatizo yake ya ndoa?

Sipendi sana kusikia hizi kauli za oh ni Mungu kaamua basi hatuwezi kufanya kitu, tufike mahali nchi hii tujifunze kuhoji matukio sio kuleta habari ya Mungu kwani ni dhihirisho nchi hii watu hatupendi kufikiri labda.Ukiweka suala la Mungu tayari unazuia uwezekano wa mtu kuchunguza, napenda sana serikali ianzishe uchunguzi mara moja.

Mwenye akili za kizamani atadai hii ni maisha binafsi, ila naamini katika dunia ya leo taasisi kubwa kama bunge inaendeshwa kisasa. Ni wajibu wa watendaji wakuu wa bunge kujua hali na matatizo mbalimbali ya kisaikolojia ya watu waliochini yao na jinsi ya kuwasaidia. Haitoshi tu kupigiwa simu na kulitangazia bunge fulani ni mgonjwa.Ilipashwa spika na katibu wajue maendeleo ya mbunge Amina kila kukicha, huu ndio wajibu wa kiongozi au mtendaji wa taasisi yeyote ya kileo ukizingatia tuko katika serikali iliyokuja na kauli mbiu: Ari Mpya na Nguvu Mpya na Kasi Mpya.Hapa taasisi ya bunge ninashawishika kuilamu kwa kuuliza: Je spika na katibu mlimsaidiaje mbunge Amina?Je bunge letu lina idara ya kutoa ushauri nasaha?

Labda nikumbushe kuwa Amina ni kielelezo cha mbunge ambaye anathubutu kusema jambo ambalo viongozi wetu wengi hawako tayari kusema kwa woga na pia labda maslahi wanayopata huko.Unafiki utailetea balaa nchi hii siku za usoni, kwani nakumbuka miaka miwili iliyopita aliuawa kule nchini Uganda Makamu wa Rais wa Sudan, John Garang, kwa ajali ya ndege ambayo inaaminika ilipangwa. Lakini waandishi jasiri waliposema ukweli kuwa kulikuwepo namna Raisi Museveni aliwakamata na kusema wanahatarisha amani.

La ajabu wiki iliyopita, mke wa Garang mwenyewe kadai mumewe aliuawa na anataka uchunguzi haraka. Mama huyu alitumiwa na Rais Museveni wakati wa kampeni za uraisi kumpigia debe Museveni na kudai Museveni ni mtu safi ambaye anasaidia hata nchi jirani kama ilivyokuwa kwa mumewe.Unafiki ni hatari ila leo anasema anaamini mumewe aliuawa.Tufike mahali tuseme ukweli ndio tutajua na kuzuia mafioso ya watu fulani ambao wanafanya wapiga filimbi kama Amina wafunge midomo yao.

Kwangu inauma na ninaamini ni pigo hasa kwa akina mama wa Tanzania kwani hata wale jasiri kama Anne Kilango watafunga midomo yao sasa. Nashangazwa pia na vyombo vya habari havina vipindi vya mijadala kuhusu kifo kama hiki; navisihi vituo vya redio na Televisheni vipite mitaani kuonesha hisia halisi za watu wengi sio kutuwekea mahojiano na watu kama waziri mkuu, sijui meya wa Kinondoni na watu wengine kwenye serikali unadhani watasema nini kama si tu kutuambia Mungu kamtwa kwa sababu anampenda. Vyombo vya habari kwa mwendo huu wa kutokuwa na utamaduni wa kuhoji, nchi hii itaendelea kuwa juu ya watu mafioso.

Natia shaka uwezekano wa kuwekewa sumu hata kusababisha sukari mwilini kushindwa hata kudhibitiwa kidaktari. Kwanini uchunguzi usifanyike?Mbona serikali ya Uganda majuzi ilimpoteza pia kiongozi kijana na katibu mkuu wa wizara ya ulinzi ambaye alikuwa tishio kwa vigogo wengi na pia mtu wa karibu wa Museveni. Baada ya kupinga uwezekano wa kifo kuwa sumu sasa serikali ya Uganda imeamua kufanya uchunguzi. Kenya ulifanyika uchunguzi wa kifo cha Ouko ila sisi watu wanaondoka tunabaki kusema oh!Mungu kampenda kuliko sisi, Bwana ametwaa! Ujinga gani huu jamani? Inatia uchungu tusivyopenda kuchunguza. Tangu Kolimba, Mwaikambo na wengine ambao hawasemwi sana.
Tumekwisha watanzania, naomba nifunge hoja kwa kuomba maelezo ya taasisi ya Bunge na pia kifo hiki kichunguzwe. Mungu amlaze pema peponi, Amina.

Saturday, June 23, 2007

MACHUNGU YA LRA

Kama unataka kujua ubaya wa vita kule Uganda kaskazini basi msome huyu mama alivyoathiriwa na waasi wa LRA.
Museveni kaanza kubadilika, anathubutu sasa kuwakamata mawaziri wala rushwa ambao waliaminika kama wasioshikika(untouchable), je unajua kwanini?Wiki iliyopita jumuiya ya Afrika Mashariki imezipokea Rwanda na Burundi, je kuna manufaa?

Wednesday, June 20, 2007

RIO FERDINAND -KAMPALA

Rio Ferdinand wa Man United alikuwa Kampala wiki iliyopita kuona maendeleo ya kituo cha michezo ya vijana anachofadhili yeye na baba yake.Nimecheka kumsoma baba wa Ferdinand haiba yake.Uganda nayo yachemsha kuna hatari isifuzu kwenda Ghana.
Tunakumbushwa pia ni nini changamoto za jumuiya ya Afrika Mashariki?Pia je ni kweli juhudi zote za kuunda jumuiya ya Afrika Mashariki zitaondoa umasikini?
Pia serikali ya Sudan imeanza uchumguzi dhidi ya mauaji ya John Garang.

MALKIA WA UINGEREZA HATANG'ATWA NA MBU UGANDA NG'O!

Ama kweli tuna kazi Afrika, yaani Malkia wa Uingereza-Elizabeti atazuru Uganda na serikali imeanza juhudi kusafisha kwa kupulizia dawa maeneo ya karibu na atakapolala ili asijeambukizwa Malaria. Kumbe tunaweza zuia Malaria Afrika?
Vita dhidi ya Rushwa Uganda inaongozwa na mwanamama matata kwelikweli.Pendekezo ni kwamba waheshimiwa wetu wanapohusishwa na rushwa basi wajiuzulu.Soma pia mapendekezo ya nnini Uganda ifanye ili iepuke dhahama baada ya kugundua mafuta.

Friday, June 15, 2007

MAMBO?

Leo nimeona niwaoneshe hasa wabongo kwanini wanapenda sana tamthiliya za TV ambazo ni za muda mrefu?Alafu je ni sawa kwa mtu mwenye akili kubaki kimya au kuunga mkono uchaguzi wa Nigeria hivi majuzi?Pia hivi kweli Iddi Amin alikuwa hatari isemavyo?

Saturday, June 09, 2007

kumbuku

http://www.monitor.co.ug/score/score06092.php(Uganda prep)
http://www.monitor.co.ug/health/health06073.php(Madhara ya AC)
http://www.monitor.co.ug/oped/oped06092.php(Iddi Amin)
http://www.monitor.co.ug/oped/oped06092.php(Musevei speech)

Wednesday, June 06, 2007

Uganda Yashinda Nigeria

Mafuta yaligunduliwa Uganda, je nchi kuwa na mafuta ndio laana?Je kukuwa kwa China ni baraka Afrika?Leo nakumbushia pia juu ya Mayombo tena, huyu mtu alikuwa na mengi ya kueleza yasiyojulikana.Nigeria yashindwa.

Saturday, June 02, 2007

Soka

Kwanza nikumbushe tu kuwa watawala wetu wanafunga midomo a wananchi tusizungumze. Nilionehsha makala moja wiki mbili zilizopita lakini Ndesanjo akaniambia nimekosea viungo vyake.Nataka niseme sikukosea nadhani jamaa walifunga kiungo kisifanye kazi lakini alieandika yuko hapa kaandika ni kwanini nilitaka msome mjue uhuru wa habari unavyoogopwa.
Leo ni kandanda hapa Afrika Mashariki, Kampala Uganda inaavaana na Nigeria mechi ambayo ni lazima waganda washinde kocha maarufu Ugannda anasema hivyo. Na huko Mwanza Taifa Stars ni lazima washinde la sivyo ni kusahau safari ya Ghana. Sina matumaini sana kwani kiwango cha timu yetu ukilinganisha na Senegali tutegemee maajabu ili kushinda.
Kwanza nikumbushe tu kuwa watawala wetu wanafunga midomo a wananchi tusizungumze. Nilionehsha makala moja wiki mbili zilizopita lakini Ndesanjo akaniambia nimekosea viungo vyake.Nataka niseme sikukosea nadhani jamaa walifunga kiungo kisifanye kazi lakini alieandika yuko hapa kaandika ni kwanini nilitaka msome mjue uhuru wa habari unavyoogopwa.
Leo ni kandanda hapa Afrika Mashariki, Kampala Uganda inaavaana na Nigeria mechi ambayo ni lazima waganda washinde kocha maarufu Ugannda anasema hivyo. Na huko Mwanza Taifa Stars ni lazima washinde la sivyo ni kusahau safari ya Ghana. Sina matumaini sana kwani kiwango cha timu yetu ukilinganisha na Senegali tutegemee maajabu ili kushinda.

Wednesday, May 30, 2007

RUSHWA UGANDA

Inasemekana eti Serikali ya MU7 iliingia madarakani 1986 ikiwa na mawazo ya kimapinduzi ambayo sasa yanadaiwa yamepotea njia.Huko Uganda kashfa kubwa ya rushwa imesababisha mawaziri vigogo kuwwekwa ndani, ni kisa kinachofanana na kile cha mheshimiwa Dito kupewa dhamana kwa kesi ya mauaji.Kisa hiki ni mfano hai wa siasa za kulindana zinapofika ukingoni.

Monday, May 21, 2007

MAUAJI YA SUMU KWA WANASIASA

Sasa waganda wameanza kuuana kwa sumu, siasa si mchezo.Kama ulishasikia mwanasiasa anayeogopeka ndiye huyu Uganda.
Uganda ni nchi iliyojaa vifo visivyoelezeka.
Wale wajasiriamali
Leo kwa wale wanasikiliza BBC Swahili, basi kila mara utamsikia msemaji wa jeshi la Uganda,ni muwajibikaji na msomi wa kileo jeshini ambaye hakusita kuandika makala juu ya kifo cha yule askari aliyefariki majuzi bila woga au mficho, ndie huyu Meja Kulayige. Mwisho kuna kashfa kubwa ya fedha Uganda tena.

Saturday, May 12, 2007

Harusi za gharama muhimu?

Wale wanaooa je mnataka harusi ya gharama?

JANET MUSEVENI KATIKA KASHFA YA GLOBAL FUND

Nchi ya Uganda imeshuhudia kashfa kubwa ya wizi na matumizi mabaya ya fedha za wafadhili hasa zile za fuko maalum(Global Fund). Iliundwa tume kuchunguza na matokeo yake ni kwamba hata mke wa Rais anahusika.Ni kashfa kubwa kwani inawahusu askari jeshi wa vyeo vya juu ambao ni vigumu kwa Museveni kuwagusa.
Upande wa michezo, timu ya taifa ya soka hapa tayari inaanza maandalizi dhidi ya Nigeria.Tanzania kwa sasa maneno mengi juu uteuzi wa timu hapa chama cha soka kimejipanga vizuri sana.Kwenye mambo ya kisiasa zaidi hebu soma juu ya ule msemo wa kiingereza usemao: Like Father like.....

Saturday, May 05, 2007

WIKI HII UGANDA

Ni vyema tuanze na juu ya nini chanzo cha kifo cha Brigedia maarufu na kijana aliyefariki Uganda siku za karibuni manake inadaiwa labda ni sumu.
Tuachane na kifo na tuendelee na siasa juu ya utawla bora.
Na mwisho eti mtoto wa Iddi Amin kaanzisha wavuti kuweka kumbukumbu za baba yake. Ila kama watu wanafikiri JK wa bongo ni rais wa karibu na watu Museveni ndio usiseme kwani ana kawaida ya kutembelea vyombo vya habari yaani redio za FM na kufanya malumbano ya simu na wtu kdhaa.

NOBLE MAYOMBO-ASKARI SHUJAA UGANDA

NEWS




Uganda mwanzoni mwa wiki hii ilimpoteza askari, mpiganaji na msomi mahiri kabisa.Noble Mayombo ni wazi alikuwa ni kati ya vijana wanaoaminiwa sana na Rais Museveni.Jamaa kafariki baada ya kuugua ghafla na inasemekana huenda kategewa sumu.Pia ni kwamba alikuwa kati ya maafisa wanaoeneza utawala wa ubabe wa Museveni na sumu yake katika ukanda mzima wa maziwa makuu.
Ni wazi alikuwa na maadui wengi saana na alikuwa na msimamo thabiti dhidi ya wapinzani akiamini mateso(torture) kama njia muafaka dhidi ya wahalifu na wapinzani kama Kiiza Besigye.Licha ya uaskari alikuwa pia ni katibu mkuu wa wizara ya ulinzi.Mengi yatasemwa lakini kashaondoka ila lazima tumkumbuke, kwani jamaa wengine wanadai hivi mashujaa tunawakumbukaje?
Jamaa kaagwa kiana yaani mwili wake kuwekwa Bungeni, mie nauliza hivi shujaa kama huyu mbona hajulikani njee ya Uganda?Mie kama msikilizaji wa redio za Uganda niliwahi kumsikia akifanya malumbano na pia nukuhu kadhaa zinamwonesha kama mtu mwenye kujidai sana; na kweli nadhani alikuwa mahiri japo nafikiri alikuwa akitetea tu utawala.
Jamaa kama kawaida mtu akifa, mkewe kamsifia kweli!
Andrew Mwenda ni mwandishi maarufu wa habari Uganda anamwelezeaje huyu bwana?Pia kifo hiki kinatukumbusha ni nini maana ya maisha.
Mwisho yuko Mhindi anatukumbusha juu ya umuhimu wa wahindi katika uchumi wa afrika.

Saturday, April 28, 2007

Thursday, April 26, 2007

UTAWALA WA KIBOKO UGANDA

Makamu wa Rais wa Uganda bado anaandamwa na kashfa ya uzinzi. Uganda imeanzisha kikosi maalum: KIBOKO SQUAD kutokana na kuongezeka kwa fujo na maandamano kila kukicha dhidi ya maamuzi dhalimu ya serikali.Watu wanachapwa viboko wakijaribu kuandamana.
Uganda pia wiki iliyopita yule bondia maarufu wa nchi hilyo alirefjea nchini humo.

Baada ya uchaguzi kule Nigeria Raila Odinga wa Kenya anaeleza woga wake juu ya nguvu kubwa alizzonazo Rais wanchi na athari zake za uchaguzi ujao.

SAYARI NYINGINE KAMA DUNIA

Wanasayansi wamegundua sayari mpya inayoaminika ina maisha ya viumbe hai kama dunia. Huko Uganda pia yuko jamaa mmoja mchungaji mwenye kipaji kwelikweli, mjue Sempa.
Nigeria imempata Rais mpya kwa uchaguzi uliolalamikiwa sana, je nini kitarajiwe?

Raisi Museveni wa Uganda kasababisha sakata kubwa la uuzaji wa msitu wa asili kwa Wahindi.Hebu tuujue undani wa tatizo hili la MABIRA FOREST kwa dhati.Wengine wamependekeza kuwe na MAPINDUZI YA SUKARI.Iko pia barua ya wazi kwa rais Museveni kutoka kwa mwananchi wa kawaida.Yapo maoni ya Mhindi juu ya dhahama hili na anajaribu kufananisha na hali ya wakat wa Iddi Amin.Mwingine katupa kanuni ya kubalansi mazingira na uchumi bila athari.

Tuesday, April 10, 2007

UZINZI HALALI UGANDA?-MAHAKAMA

Museveni hatimaye kaanza kuzungumzia mipango ya kuondoka.
Mahakama ya Uganda imefafanua juu ya sheria ya ukahaba au uzinzi kwa mwanamke na mwanaume, hata hivyo bado akina mama wengi wa Kampala wanataka talaka waachane na mabwana zao.Amanya Mushega, katibu mkuu wa EAC wa zamani anazungumzia juu ya utawala bora. Hotuba yake inatoa historia ya siasa za Uganda.
Ule msitu wa Mabira ni kielelezo cha rushwa nchini Uganda kwa miongo mingi anasema Andrew Mwenda.

Saturday, April 07, 2007

MZUKA WA IDD AMIN BADO

Watu wanamjua Iddi Amin kama mtu mnyama kuwahi kutokea Afrika. Lakini ni lazima tumtizame huyu bwana kwa undani hasa kuwa hata waliomfuatia ni wanyama pia, je unajua kwanini? Tunaambiwa eti serikali ya Museveni ni tishio kwa wapinzani kama alivyokuwa Idi Amin.
Amanya Mushega alikuwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki, yeye anapinga kuuzwa kwa msitu wa Mabira. Tunakumbushwa jinsi vyama vya siasa visivyo na nidhamu. Na je nini chanzo cha matatizo ya Afrika, Museveni alishasema ila leo hii anavunja aliyowahi kunena.

HERI YA PASAKA

Ni Pasaka hivyo hatuna budi kujua sikukuu hii husheherekewa vipi na jamii mbalimbali duniani?
Huko Uganda bado kasheshe la uuzaji wa msitu wa Mabira linaendelea.Limesababisha mfalme wa kabila la Baganda Ronald Mutebi kuja juu na kukataa uuzaji huo ndani ya Mahakama ya Kikatiba ya Uganda.Hii inasababishwa pia na tishio la hali ya hewa kuchafuka duniani. Wanasiasa ni watu wa ajabu kwelikweli, Museveni aliwahi kusema atalinda mazingira lakini leo hii anayabomoa kwa kuuza msitu huu.
Ujumbe wa pasaka eti Mbeki.

Tuesday, March 27, 2007

MAKAMU WA RAIS UGANDA NA HAWARA!

Ms NAKKU, Prof. BUKENYA AND THE MAFI
Zile harakati za kutia nyongo harakati za Makamu wa Rais wa Uganda ili asimrithi Museveni zinaendelea, hapa kajitokeza Mwanamama mmoja na kudai eti yeye mke wa pili wa Profesa Bukenya.
Haya yote ni kule kuonesha kuwa viongozi wetu na jamii kwa ujumla kuna tatizo la kimaadili. Zaidi ya maadili pia eti kuna maadui wa Bukenya wanataka kumuangusha. Yeye anadai eti ni mafia ndani ya serikali, je ni kweli?
Tunalojiuliza ni hivi kweli atapona na kashfa hii huyu bwana?Na je kuna uwezekano wa Mganda kuwa Raisi?

SIASA ZIMBABWE SAWA NA UGANDA?

Hali ya kisiasa ya Zimbabwe inalinganishwa na Uganda kwa kiasi fulani.Je Waingereza wajinyonge atakavyo Mugabe? Wiki hii Bunge ndani ya harakati za Jenet Museveni,(mke wa rais) lilizima juhudi za kumjadili na kumlaani Mugabe.
Museveni naye inasemekana anao mawaziri ambao hawatakaa waachishwe nyadhifa zao.Tunakumbushwa pia umuhimu wa nidhamu katika siasa.
Mwisho hebu tujisomee kwanini demokrasia imeichafua Afrika kwa sana? Andrew Mwenda, ni mwandishi maarufu na makini ana mengi ya kutuambia. Ndio maana Museveni anadaiwa kuwa kibaraka wa Bush huko Somalia.

Monday, March 26, 2007

NINA WASIWASI KAMA TUTAKWENDA GHANA.

Nilisema juzi kuwa tutafungwa na kweli tulifungwa. Sina hakika kama tutafuzu kwani ninahakika kibarua ni kigumu kwa hali ya mchezo ilivyokuwa juzi ni kwamba sisi tuko kwenye ligi ya kiwango kingine kabisa na wapinzani wetu Senegali au Burkinafaso.
Leo nataka nieleze hisia zangu kwa jinsi nilivyotizama mechi ile. Kwanza kabisa sina matatizo na kocha Marcio Maximo japo nashangazwa ni kwanini aliamua wachazaji wetu wacheze kwa kutafuta ushindi na si kujihami ugenini siku ile kitu ambacho kiliwachosha sana na tukafungwa.Magoli yote yalisababishwa na mapungufu ya walinzi wetu. Tangu mwamuzi Mourad kuanzisha mechi, ndani ya dakika tatu za mwanzo tayari Senegali walipata kona ambayo nadhani mlinsa lango wetu angetakiwa azuie mpira ule usitoke lakini kwasababu azijuazo yeye aliuacha mpira utoke huku akijua ingekuwa kona. Wachezaji wetu lazime waelewe kona ni goli kwa wazoefu kama Senegali nadhani.
Nawapongeza Taifa Stars kwa dakika thelathini za mwanzo ila baada ya hapo pumzi ziliwaisha kabisa. Vijana wakawa wazito kuziba nafasi hasa sehemu ya kiungo na mzigo ukabaki kwa ngome kuelemewa na ndiyo maana hata makosa yalikuwa ni lazima kwa wachezaji wa nyuma kwani walikuwa wakiucheza mpira muda mwingi.Ndipo dakika ya 87 jamaa wakapata kona; sijui kama wenzetu wanajufunza kulinda lango wakati wa kona. Goli la kwanza lilitokea hapa kwa kichwa cha Mamadou Niang. Sitaki kuhoji kwanini mchezaji yule aachwe kupiga kichwa huru ila nadhani kama nguzo ya goli ya upand wa kushoto kungekuwa na mtu basi angeokoa mpira ule kirahisi.
Sielewi nahodha, Mecky Mexime, aliyetakiwa kuwa pale alikuwa wapi kwani hata kona nyingine iliyofuata katika dakika ya 44 pia nguzo ya kushoto ilikuwa tupu. Kwa ujumla kipindi cha kwanza tulijitahidi sana kwani angalau Abdi Kassim aliweza angalau kupiga shutu moja zuri langoni mwa Senegali na pia Mwaikimba na Said Maulidi(SMG) walikuwa wakipasiana vizuri japo Smg alikuwa na tatizo la uzubaifu wa kurejea pazi za mbadilishano(return). Mapungufu mawili yalikuwa ni: moja, mipira ya kurusha tulishindwa kuitumia kabisa. Sielewi kwanini hatukuwa tunarusha mipira mirefu langoni mwa adui. Pili, kiungo chetu kilichezwa na wachezaji wadogo kiumbo ambao wasingeweza kumudu maumbo makubwa na kimo kirefu cha viungo wa Senegali kama tulivyoona.
Mara kadhaa niliona Nizar Khalfan akijaribu kukokota mpira kama vile anacheza chandimu mchangani. Ni lazima Maximo afundishe wachezaji wetu watumbue eneo la katikati ndilo linaloamua mechi. Wenzetu wanajipanga kwa eneo lenye ukubwa fulani hivyo kupenya si rahisi kwani wanaziba matundu yote katikati huku wakisaidiwa na uwezo wao mkubwa wa kuteleza na kuzuia kwa nguvu wakitumia ulizaji vibuyu(tackling) wa nguvu za ajabu.Ni vigumu kiungo chetu kingetamba siku ile. Ningependekeza Maximo aanzishe mfumo wa kutumia kiungo wa mbele ya walinzi(defensive shield) kule Brazil wanamuita "Burukutu" na awe ni mtu mwenye nguvu na mapafu haswa. Nasema hivi kwani siku ile niliona viungo wote wanacheza kama walinzi na hakuna aliyekuwa akichezesha kuunganisha washambuliaji.
Hapa napenda nipingane kabisa na Zamoyoni Mogella alipokuwa akichambua medhi ile runingani alipotupilia mbali kuwa umbo si hoja.Umbo ni kigezo hasa kwa wachezaji wa kiungo cha kati katika mpira wa kileo kwani hawa ni watu wanatakiwa kuwa na nguvu nyingi na uwezo mkubwa wa kuzunguka eneo kubwa la kati hadi mbele(zones).Nimshauri kabisa Maximo, kuwa kuna haja ya kusaka wachezaji warefu wenye nguvu wa eneo la katikati kama kweli tunataka kwenda Ghana.Hawa wapo sio lazima watoke Simba au Yanga.Wapo mikoani na wana uwezo wa kufundishika kiufundi.Nikumbushe kuwa mchezaji wa zamani wa Ushirika ya Moshi na Yanga, Willy Martin alitokea namna hii, mwanzoni akiwa mtu goigoi tu kimpira lakini Dan Koroso alimpika na akaja kuwa mahiri ajabu.
Sasa niendelee na kipindi cha pili cha mechi ile ya jumamosi: kilianza kwa mabao ya haraka haraka. Goli la pili la Diomasy Kamara ni magoli wanayofungwa wadosi katika ligi za ulaya kama Charlton, Wartford na hata West Ham siku hizi. Mara nyingi yanakuwa makosa ya mabeki wasioelewa vizuri. Nilifikiri mabeki wetu walikuwa bado hawajajua nini kinatokea kiwanjani, ilinishangaza sana. Ni makosa ambayo mpira wa kimataifa hutakiwi kuyafayanya kabisa.
Dakika mbili baadaye, Niang alifunga japo alinawa lakini refa hakuona ila mabeki wetu walionekana kumuacha Niang acheze wakinyanyua mikono kwa refa kama walivyozoea hapa Bongo. Ushamba wa mpira wa ridhaa ulijionesha wazi kwani filimbi haijalia wewe unatakiwa ucheze mpira.Ni mambo ya kujifunza haya kwa wachezaji wetu hasa wanapokuwa ugenini kwani wakumbuke mara nyingine huenda refa kalishwa mlungula dhidi ya wageni.
Goli la nne katika dakika ya 61 lilisababishwa na uzembe wa Nsajigwa ambaye hakuruhusiwa kupanda mbele siku hiyo kwani aliwekewa winga teleza ambaye hakumpa mwanya wa kupanda na plani nzima ya Taifa Stars ikaingia mtimanyongo.Nsajigwa alijaribu kumpiga chenga msenegali na akakosea na ndipo krosi ikatumwa na Niang akaunganisha kwa kichwa cha nguvu baada ya kumzidi kipa Ivo aliyetoka vizuri na kuchelewa. Ila hapa pia lazima niwalaumu walinzi wetu jpale kipa alipotoka hakuna mtu alibakia nyuma yake kulinda lango.
Kuanzia hapa nilitaraji goli la tano lakini Mungu akaweka mkono kwani Wasenegali walikuwa wanatutega tuende mbele watushtukize jambo ambalo halikufanikiwa.Nilimwonea huruma Maximo wakati Costa anapiga chenga alafu akanyang'anywa manake Maximo alishika kichwa akijua tumekwisha. Kwa ujumla Senegali walitumia 3-5-2 na sisi sikuona 4-4-2 ila muda mwingi ilikuwa5-3-2 kitu ambacho ingekuwa vigumu kupata bao na pia kufungwa japo pia tulifungwa. Hii nadhani ilisababisha viungo wetu wazidiwe na viungo wengi wa Senegali. Na hivyo mpira kuchezwa na mabeki kwa muda mrefu hali iliyosababisha wafanye makosa mengi. Kimsingi nafasi ya Ghana bado ipo ila Maximo afanye kazi kwenye ufundi(technique) hasa kiungo na pia ningependa tuone wanaitwa vijana kadhaa wapya wenye mbio kali katika wingi zote mbili. Pia ninataka Maximo atafute mchezaji wa mguu wa kushoto kucheza beki ya kushoto kwani siamini Mecky anafaa nafasi ile; hana spidi na hajui kulinda ipasavyo.

Saturday, March 24, 2007

TAIFA STARS NADHANI TUTAFUNGWA LEO

Nianze na huu mchuano wa leo kati ya Taifa Stars na Senegali. Maoni yangu ni kwamba haddi wakati naandika makala hii nadhani Senegali wana nafasi ya kushinda: uzoefu, vipaji vilivyoiva,mbinu bora na ufundi mwingi pamoja na uenyeji.Hizi ndizo sifa zinazonifanya niamini watatufunga angalau mabao matatu bila majibu.
Timu yetu itategemea ngome na golikipa angalau tupate sare. Ni wazi kwenye kiungo patatuangusha kama hatutakuwa makini na ufungaji sitaki kusema chochote kwani sioni kama kuna mtu atakayeweza kufunga japo kidogo labda Saidi Maulid na mkongwe
Nigusie pia habari za siasa wiki hii Komredi Mugabe anaanza kudondoka ni wazi siku zake zinahesabika; pia huko Uganda wanasiasa wameamua kuuza msitu maarufu na muhimu wa Mabira japo yuko mfalme wa Buganda kaamua kuipa serikali ardhi ili isiuze.
Uganda bado inabakia ni nchi yenye waasi wengi, hebu wajue.

Saturday, March 17, 2007

AFYA ZETU TWAZIJALI?

Kabla ya kuangalia afya hebu tuone Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anasemaje juu ya muungano huu?Na ni jinsi gani majeshi ya Uganda yana umuhimu huiko Somalia?
Leo tuangalie afya, hasa juu ya mambo ambayo wengine twafikiri ni urembo kumbe liipo jambo hasa kwa wanawake ambao hawatakiwi kuvaa mini skirt.Pia je kutoa mimba sawa?Pia ni jinsi gani kusevu pesa kunawezekana?
Siasa je unajua ile report ya tatizo la PRA?Maajabu ya maadili kwenda likizo, hata Mufti Mkuu mdanganyifu?Ni vizuri pia tujue wanasiasa maarufu wana historia gani?
Mwisho juu ya wazazi wetu, je kuna haja ya kuwajali?

Saturday, March 10, 2007

MAJAJI WAMALIZA MGOMO

Baada ya ile sinema ya Iddi Amin kushinda Oscar, hali ya kisiasa nchini Uganda inaonesha wazi sinema nyingine tayari imeanza kutengenezwa. Kwanza soma ni vipi mwanaye Iddi Amin alivyomfahamu baba yake?Imeshangaza sana hata majaji wanaweza kugoma.Unaambiwa mgomo umekuwa na athari zake kwelikweli. Waganda inabidi waje tena MOSHI kwa majadiliano upya.
Ni vizuri tujue kasheshe lililosababisha majaji kugoma Uganda na ni jinsi gani demokrasia imechafuliwa?
Mwisho ni hii simu mpya ya I Pod.

Wednesday, March 07, 2007

HATA MAJAJI WANAGOMA UGANDA?

Uganda inaongozwa kwa miujiza ya Mungu kwa mujibu wa Museveni. Athari zake ni kama ifuatavyo: moja, majaji wamegoma kwani wamechoka kuingiliwa na serikali na pia hata mawakili(wanasheria) nao wamejiunga na mgomo wa kuidhalilisha taasisi ya mahakama.Museveni ndiye atakayekuwa rais wa kwanza wa jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini haya ya kutuma askari kuingilia maamuzi ya majaji tuyararajie?
Tunaambiwa hakuna utumwa wa hali ya juu kama ule wa kuwa na Rais mmoja kwa muda mrefu. Uganda kama Tanzania inafanya kila juhudi kukandamiza haki ya kupata habari.
Jambo moja linachekesha Museveni ameisifia sana ile sinema ya Iddi Amin iliyoshinda Oscar majuzi, je unajua kwanini?Yanayotokea uganda yanatakiwa kuepushwa ni aibu.Uganda na nchi nyingine Afrika zimebakia hakuna maelewana kati ya serikali na wapinzani.
Tuje mambo ya Makerere, na pia tuone ni jinsi gani wanawake wamefanikiwa kisiasa? Pia nini kinakwamisha mazungumzo ya LRA Uganda?

Wednesday, February 21, 2007

LEO SIASA ZA UGANDA

Uganda ina siasa mbili: ya nchi na ya Jadi ambayo sasa kuna waka moto huko Lubiri.
Kuna fununu Makamu wa Rais wa Uganda atang'olewa madarakani.Je inawezekana?na je ni nani huyu Profesa Bukenya? Yeye mwenyewe kaamua kuwa ngangari na anasema haendi kokote, je hili tishio kwa Museveni na ndio maana anamng'oa kwani kwa Uganda, kuna imani kuwa mtu wa kabila la BUGANDA hawezi kuwa rais kamwe kwani hiki ni cheo cha watu wa anakotokea Museveni tu: Mashariki.
Kuna maoni juu ya filamu ya Iddi Amin; na pia unajua uwongo wa picha hiyo?

Saturday, February 17, 2007

UASI NI RUKSA--KANALI BESYIGYE

Kanali Besigye bado anaendeleza tambo zake za kumng'oa Museveni. Hapa anafikia hatua ya kuhalalisha uasi kama njia halali ya kujipatia madaraka. Alafu mjue shujaa wa Uganda.

WANASIASA NI FEDHULI KULIKO NYANI

Tabia za mwanasiasa yeyote hazina ukweli wala uaminifu, inasemekana wanasiasa ni wadhalimu kuliko hata nyani.
Bado mammbo ya Rwanda nayaona kama kizungumkuti. Ninapata hisia labda akina Kagame wanamsingizia tu mke wa Habyarimana. Sina imani kuwa kuna chuki za magharibi dhidi ya Rwanda.
Museveni ni bingwa wa siasa kwa kuweza kuchanganya siasa na utawala wa kifalme kufanya kazi bila matatizo.Lakini pia zipo gharama za kuzuia matatizo yaliyotarajiwa mfano haya.
Huwa napenda KANDANDA pia;eti meneja wa Chelsea anadai watatwaa ubingwa, je inawezekana?
Kwa wale makapera kama mie: je kuna ulazima wa kuoa?

Wednesday, February 14, 2007

ETI LEO NI SIKUKUU YA VALENTINE?

Wakati nikiwa masomoni Uganda nilijifunza juu ya Demokrasia na mhadhiri wangu kaandika juu alichotufunza gazetini kuhusu siasa za Uganda hasa juu ya majadiliano yasiyokwisha. Hapa anajibiwa na mwandishi eti kakosea. Mjadala unaendelea juu ya siasa haswa. Jua siri ya serikali ya Rwanda kuhusu matumizi bora ya magari ya serikali.Huko Uganda kuna mgogoro bungeni juu ya kuyaruhusu majeshi ya nchi hiyo yaende ama la nchini Somalia. Wapinzani wamegomea bunge kwani hawataki majeshi yande Somalia kitendo kinachoonekana ni kuiunga mkono serikali bila kujijua; je ni kwanini?
Hili ni la muhimu sana juu ya kufungiwa hivi majuzi kwa kituo kipya cha televisheni-NTV-kwani ni juhudi za udhibiti wa vyombo vya habari Afrika Mashariki kama zile za kudhibiti wanaharakati kama HAKI ELIMU nchini Tanzania.Lakini pia tunakumbushwa ipo mijpaka ya kusema na kuandika hasa kwa vyombo vya habari-THE FOURTH STATE.

WIZI WA MITIHANI UGANDA

Wakati nchini Tanzania tuna wabunge na mawaziri wenye tuhuma nzito za kudanganya juu ya masomo au shahada zao huko nchini Uganda wabunge hawako tayari kufanya hayo ama kuruhusu watu kuiba mitihani. Wanachukua hatua inapobidi.
Soma juu ya jinsi siasa ulivyo mchezo wa kufanyiziana: kuanzia Afrika mpaka India na hata Ulaya. Ni mchezo mchafu sana ninavyoamini. Pia niliwahi kuandika juu ya Profesa Mamdani akitusihi Wabongo tuachane na mikopo ya kusoma chuo kikuu, leo kaja na makala nyingine juuu ya hili. Na mwisho kafunga mjadala wa elimu chuo kikuu.
Pia ni vipi ilivyo muhimu kusaidia Wasomalia: unajua PAN Africanism?

Saturday, February 10, 2007

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE--2006

Eti waafrika ni watu wasiweza kuendelea hata wafanye nini, je ni kweli?
Kuhusu elimu huu ndio msimu wa wale wa shule kufurahia mavuno yao.Matokeo ya mwaka huu ni haya hapa.
Pia je unajua kuonesha uwazi wa sehemu zako ni makosa hadharani?
Wakati Wabunge wa Uganda wanabishana juu ya kupeleka askari huko somalia inasemekana ni faida kwa Uganda.\\Pia ni kwawaida kwa walarushwa kulindana, kama uliwahi kusikia kashfa kubwa ya waziri wa Uganda sasa kaula, kapewa tenda na rafikie Museveni.

Thursday, February 01, 2007

JINSI MAJESHI YA BONGO YALIVYOWATIA KIZUIZINI WAGANDA TZ.

Ninapenda sana mambo ya uhusiano yanavyochambuliwa na wengine hebu soma hili.Je unajua mambo ambayo watanzania wengi hatuyajui wakati wa vita ya Iddi Amin?
Unamjua bingwa wa uandishi habari aliyekufa?
Unapaswa kujua pia yuko Rais wa nchi moja ya Afrika(Guinea) bado yuko kwenye zile zama za kung'ang'ania madaraka.Pia soma juu ya jinsi vyama tawala, au vyama dola kama CCM vinavyofanya katiba ya nchi kama mali yao.
Hili ni la muhimu sana kujua juu ya Uganda manake baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana wapinzani walilalamika mahakamani na majaji wa mahakama kuu wakatoa uamuzi kuwa Museveni alikuwa mshindi halali.Jua ni kwanini majaji walitoa uamuzi huo,
Pia ni vyema usome uamuzi wao ulisemaeje?
Soma pia ni jinsi gani bara letu Afrika lilivyo na wabunge ghali sana juu ya uwezo wa nchi.Pia huko Uganda eti ubinafsishaji umegeuka kuwa kama ugaidi.
Pia tunakumbushwa ni kwanini hatuna sababu ya kukumbuka siku ya uhuryu wa nchi zetu?Alafu mwisho kabisa:SOMA JUU YA BLOOD DIAMOND, sinema ambayo inaelezea juu ya umafia ulivyokithiri Afrika.

Wednesday, January 03, 2007

FUNGUA MWAKA 2007

Mwaka 2006 umemalizika na makala kadhaa ambazo zimegusia ni jinsi gani ulimwengu wetu ulivyo na changamoto. Kifo cha Saddam pia kimegusa hisia za wengi na hasa jinsi udikteta mpya ulivyozaliwa na kinyongo hiki cha dikteta. Hata waliokuwa wanamtetea inasemekana serikali ya sasa inawatisha sana.
Mwaka mpya ni wakati wa kugusia juu ya taasisi za kiserikali zinavyopaswa kufanya kazi hasa Afrika Mashariki. Pia tujifunze zaidi nini mchango wa China katika uchumi wa Afrika?
Pia ni vizuri tujifunze juu ya changamoto za SACCOS.

Friday, December 22, 2006

MASLAHI YA NCHI NI ZAIDI YA SIASA NA HISIA ZA WATU

Unaposikia tofauti kati ya siasa na maslahi ya nchi mfano mzuri uko hapa kwenye maziwa makuu.
Pia kuna hili la kalenda ya uendeshaji wa ligi ya soka.
Pia huko Kenya rais Kibaki atakuwa Mombasa kama kawa.

Thursday, December 21, 2006

HAKUNA HAJA YA MIKOPO ELIMU YA JUU-PROF: MAAMDANI

Wakati wabongo tunalia na JK kuhusu mikopo ya elimu ya juu, yule profesa maaarufu, Maamdani kachapisha kitabu akisema eti serikali isilipie ila wote tulipie elimu

Tuesday, December 19, 2006

JK NA JINAMIZI LA CCM NDANI YA MWAKA MMOJA IKULU

JK sasa anaanza kuona ukweli halisi wa bongo kuwa tatizo liko kwenye CCM. Hili ni jinamizi ambalo JK ana kazi ngumu kuliondoa manake ncchi imeoza na itagharimu Taifa sana kuweza kuondoa hayo ambayo JK kakemea jana.

SALAM ZA CHRISTMAS

Tunasherehekia Krismas soma jinsi makasisi wa dini mbalimbali(mapadiri na wachungaji na mashehe pia) walivyobadilika siku hizi na tunakkumbushwa je Yesu wa wakristu angezaliwa leo ingekuwaje Afrika?Alafu nataka uone ni jinsi gani wabunge wa Afrika hasa Uganda walivyo na ulafi na mapenzi na MABENZI na si wananchi, yaani wanatishia serikali pale inapotaka kuwakata usawa.
Mwisho, ona jinsi Jaji Kiongozi Uganda hisia zake juu ya utawala bora.Alafu mkuu wa Jeshi la polisi Uganda naye anaamua kumjibu na kumkosoa ikibidi Jaji Kiongozi, patamu hapa.
Alafu wajue watu kumi waliotingisha Uganda mwaka huu.

Friday, December 15, 2006

MKE WA MUSEVENI KATIKA UGOMVI KUMTETEA MUMEWE

Mke wa rais Museveni ambaye ni mbunge jana inasemekana karushiana maneno makali na mwanamama mmoja wa shoka wa chama cha upinzani katika kile kinachoonekana kutetea rekodi mbovu ya mumewe ndani ya bunge.
Alafu unajua kwanini maprofesa wa Makerere wamegoma? Soma haya.

Wednesday, December 13, 2006

UDIKTETA-SIRI YA KUISHI MUDA MREFU

Eti madikteta hawafi mapema, tunahimizwa tuwe majitu korofi na dhalimu ili tuishi muda mrefu.

Thursday, December 07, 2006

JK AIGE KUTOKA KWA CALDERON WA MEXICO

Kama kweli Tanzania inapenda maendeleo tunahitaji kiongozi kama huyu aliyechaguliwa huko Mexico majuzi. JK angekuwa namna hii na akatekeleza basi tunaweza kufanikisha "Maisha bora kwa kila Mtanzania".
Vinginevyo JK anatania tu.

UHURU BONGO--BONGE LA PATI SAWA AU DHIHAKA?

Kama mtanzania sina budi kujumuika na watanzania wenzangu kuadhimisha siku hii ya miaka 45 ya uhuru wa Tanzania bara(Tanganyika).Huu ni wajibu wa mzalendo yeyote kutathmini je uhuru wetu umeleta tija kwa watanzania wote au kwa kukundi fulani ndani ya jamii tu?Sisherehekei manake kwa hali ilivyo si muafaka kwa hili bali ni wakati wa kujiuliza kwa nini tunaendelea kuharibu uchumi wetu namna hii?Sherehe tuwaachie wanaoona matunda ya uhuru kama akina JK na Ngoyai: hawa kwao hakuna tatizo la umeme, maji wala usafiri au barabara mbovu. Kwao wanazo njia mbadala kutatua haya.
Nimefuatilia sherehe za uhuru leo kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam(RTD) kwani wakati ndio sherehe inaanza hawa jamaa wa Tanesco wakakata umeme alafu ikaw ndio mwisho wa kuangalia Runinga yangu.Matanzgazo ya RTD hayasikiki vizuri nashangaa kwanini RTD wasiweke mtambo wa FM manake hizi FM radio nyingi ni muziki kwa kwenda mbele utadhani siku ya leo ni sawa na zingine. Ni Radio Free Afrika ya Mwanza na Sauti ya Injili ya Moshi angalau leo wamekuwa na vipindi kuwahoji watu ambao walihusika na uhuru wetu wakati ule na wametoa mawazo murua kweli. Nakwambia tukio hili hapa Moshi si la muhimu kama siku ya jumapili au sikukuu ya Idd El Fitri kwani siku hizo umeme ni bwerere.Hasira imenishika kwani baada ya sherehe kumalizika hawa jamaa wanawasha umeme, nakwambia Tanesco hapa Moshi hawajui uhuru kabisa. Hayo tuyaache, ila JK hotuba yake ilikuwa nzuri nampongeza sana. Ila aliangalia tu mafanikio nchi iliyojipatia tu tangu 1961, ameacha kuzungumzia matatizo kama haya ya Umeme.

Nami naona nieleze kwa ufupi japo ninafikiri nini siku hii:

Mtizamo wangu unatia wasiwasi sana kama kweli tumefikia mafanikio ya dhati kulingana na kipindi cha miaka 45. Naanza na sekta ya barabara tumefeli kabisa. Bado hatujaweza kuunganisha nchi yetu kwani tunalazimika kupitia Kenya kusafiri kutoka Arusha kwenda Mwanza, Bukoba au hata Kampala.

Pili bado tunakumbwa na njaa kila mwaka ilihali tuna ardhi, mito kibao kuwezesha kilimo cha umwagiliaji. Ukija kwenye maji ndio usiseme kabisa. Hakuna maji kunywa ya kutosha hata katika miji kama Dar es salaam, Arusha na hata Mwanza.
Huwezi kuamini nchi yenye umri wa miaka 45, haina umeme wa kuaminika na kutosha angalau mautmizi ya majumbani achilia mbali viwandani. Viongozi, yaani wanasiasa hawana utashi wowote kwa maendeleo ya jumla ya nchi. Maslahi binafsi yamewekwa mbele kuliko uzalendo: kwa mfano, nchi inagenishwa kwa kubadilishana/bei poa kati ya watu fulani ndani ya tabaka tawala(elites) na si kwa maslahi ya mtu.
Ukija kwa watunga sheria(Wabunge) ndio basi tena. Bunge limekuwa jamvi la kila mtu siku hizi hata wendawazimu au kwa maana nyingine mbumbumbu kielimu nionavyo kutokana na matendo yao.Elimu si tija kwa mtu kuwa mbunge au diwani. Nidio maana bunge letu ni taasisi ya kubariki mambo yasiyo na maslahi kwa Taifa ila Chama(CCM) na yale ya binafsi. Chama tawala kimelimeza bunge na kutupeleka kuzimu kiuchumi. Tumefika mahali mtu akiheshimu taaluma katika kusimamia au kuamua mambo ya kiuchumi na mengine ya msingi kama hayo anaonekana mwehu na si mwenzetu. Hii ndio miaka 45 ya uhuru tunayosherehekea. Hili ni lazima tulitafakari la sivyo uhuru unakuwa hauna maana.
Kwa robo mwaka sasa nchi iko gizani, hakuna umeme na viongozi na wahusika wetu hawajali kabisa. Ufisadi na kulindana ndio umetufikisha hapa tulipo na viongozi wahujumu hawaguswi bali wanahamishwa kutoka idara au wizara moja hadi nyingine kuendeleza uharibifu. Vipaumbele vyetu ni vile visivyo; viongozi wetu wamebakia kusafiri kutembeza bakuli kwa wafadhili na kuhimiza uwekezaji katika nchi isiyokuwa na umeme wa kuaminika bila aibu. Kiongozi mkuu anadiriki kusema tatizo la umeme limerithiwa kutoka serikali iliyopita bila kung'amua alikuweko ndani ya serikali hiyo.
Kisiasa, nchi imebaki hoi kabisa; vyama vya upinzani viko hoi kabisa na havionekani kuchukua hatua madhubuti kutia changamoto kwa CCM inavyoboronga. Haya yakiendelea, CCM chini ya Makamba imebakia kuwarubuni wapinzani makini kurejea CCM kama ndio kipaumbele. CCM haitaki changamoto, kwake kuwa mpinzani ni uadui, si uzalendo kwa nchi. Kweli hapa hatutaelewa wapi tunakosea kama tutaendelea hivi na ndio maana bado tuko nyuma maeneo mengi. Demokrasia yetu ni kama vile "maonesho kwa wafadhili"(show-off) na sio demokrasia ya dhati.
Viongozi wetu kama vile Lowasa na Makamba wanaongoza kwa sera kongwe za kihafidhina. Hili ni tatizo la viongozi ndani ya chama tawala, serikalini na hata vyama vya upinzani. Tunahitaji kizazi kipya cha uongozi nadhani ili tuendelee. Hata hivyo, kama Taifa tumefanikiwa kubaki na umoja wa kitaifa kitu muhimu kwa nchi yeyote.
Amani tuliyonayo ni lazima tuikuze kwa kuziunda upya taasisi za kidemokrasia katika utawala ili muongo ujao tupige hatua kwa haraka na si kama miaka hii 45 iliyopita. Katiba ni lazima iangaliwe upya ili miundo ya mihimili mitatu ya dola ifanye kazi inavyopaswa kwa uhuru na si kama sasa kwa kulinda maslahi ya chama tawala. Hii imefanya kwa mfano bunge letu kubaki kama muhuri wa udhalimu "rubber stamp" wa serikali mara kwa mara.
Mwisho, ingawa wenzetu wa magharibi iliwachukua muda mrefu kufikia mafanikio ya demokrasia, sisi isiwe kisingizio, kwani dunia ya leo mambo yamerahisishwa ni lazima tuendelee haraka. Nitoe rai: Tuna wasomi wengi wa kila aina Tanzania ila wote wamefungwa jela ya nafsi zao(conscience) na wamekuwa bendera fuata upepo(sycophants) mbele ya wanasiasa wa chama tawala. Ujasiri unahitajika kwa wasomi wa nchi hii la sivyo kama nchi tutaendelea kusherehekea uhuru wa wachache kama tunavyofanya leo hii. Kwani mantiki ya nchi huru sidhani ina maana kwa watanzania wengi wa kama kule vijijini pembezoni mwa nchi hii. Na kwa akina JK, Ngoyai na Makamba: kumbukeni turuhusu changamoto ndani ya chama na hata serikalini kwani ikiwa tutafanya hivyo hatutaona mikataba ya kijinga kama hii ya IPTL, Richmond, Usiri wa biashara ya mihadarati na mengine mengi ambayo hayasemwi kwa kuogopa kumkosoa bwana mkubwa.

Wednesday, December 06, 2006

KAGAME-MUNGU MTU- ASHTAKIWE TU

Naiangalia hali ya Rwanda kama ni tatizo ambalo waafrika hatuwezi kulitatua kwani kihistoria ni vigumu. Sina imani sana na mahakama ya Arusha kwani naiona kama mahakama iliyoundwa na washindi wa vita(RPF) ili kuwahukumu washindwa.
Ndipo hapa ninapokuwa ninamuunga mkono huyu jaji wa kifaransa kutaka pia Kagame ashtakiwe. Sidhani kuna suluhisho la kiafrika, ila naunga mkono juu ya nia ya mficho ya Ufaransa katika sakata hili. Pia nionavyo tutarajie Rwanda yenye matatizo sana hapo baadaye kwani Kagame inasemekana ni kiongozi Mungu mtu.Tatizo letu waafrika ni kutokupenda kusema ukweli na kama tutaendelea na uwongo huu wa Kagame hakuna maridhiano Rwanda.
Lakini pia ni lazima tujue pande zote mbili zilihusikaje katika kile kinachoitwa ukombozi wa Rwanda?Kwa mfano, picha halisi ya ushiriki wa Kagame na Habyarimana unaweza kuisoma na kupata hali halisi hasa hii makala ambayo mwandishi anao uelewa sana wa mambo ya Rwanda.

Tuesday, December 05, 2006

BESIGYE ALIVYOMNYANG'ANYA MUSEVENI MKE

Pamoja na kufuatilia habari za wanasiasa kadhaa ni vyema pia wakati mwingine tujue habari zao binafsi. Leo nataka nieleze habari za kiumbea ambazo niliwahi kuzisikia juu ya Museveni, Kiiza Besyige na huyu mwanamke wa chuma(iron lady) Bi Winnie Byanyima.
Inasemekana ugomvi kati ya Museveni na Besigye pia unachangiwa na kuibiana mabibi. Eti Bi. Byanyima awali alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Museveni wakati wa vita ya msituni. Wakati huo Besigye akiwa kama daktari wa Museveni. Leo hii Bi. Byanyima ni mke wa Besyigye japo nakumbuka niliwahi kumsikia akihojiwa na redio moja Kampala na akadai kuwa eti Besigye ni mshirika wake tu(companion).
Wambeya wanadai eti siku waasi wa Museveni(NRA)wanaiteka na kuitwa Kampala, waliingia Kampala huku gari alilokuwemo Museveni likiendeshwa na Bibie huyu.
Hayo yote tisa, kumi leo hii Dr. Besigye kaamua kuyaanika yote yaliyojiri kule msituni na ni jinsi gani walikutana na bibie huyu.
Kama kawaida, Uganda ni nchi iliyojaa visa vya kisiasa vya kiume kweli si kama Tanzania, soma huyu mpinzani madhila aliyokwishapitia.

RAIS NA GAVANA UGANDA--WAWAKAMUA WALIPAKODI KWA BIASHARA BINAFSI

Mimi ni kati ya wasioamini adhabu ya kifo hata kama mtu kafanya nini. Ila nimeshangazwa sana na nchini Uganda hata katiba inaruhusu kama ilivyo pia kwetu Tanzania. Lingine ni hili la Rais Museveni na gavana wa benki kuu wameamua kutumia pesa za wali pakodi kumsaidia mfanyabiashara mmoja asifilisike.Ila inasemekana huyo mfanyabishara ni jamaa tu anasimamia shughuli za mzee.
Kama kawaida yangu napenda sana kujua inakuwaje watu wengine wanafanikiwa kimaisha wangali wadogo?

Monday, November 27, 2006

MJUE GENERAL SALEH WA UGANDA

Leo nataka watu musome juu ya jamaa ambaye anajulikana kama shujaa hapa Uganda na ambaye ndie aliyesababisha kuanguka kwa serikali ya Obote.

Wednesday, November 22, 2006

MGAO WA UMEME UGANDA NI MIAKA MITATU SASA JE BONGO?

Huku tukiwa tunalaumu wanasiasa wetu juu ya labda hujuma au rushwa juu ya matatizo ya umeme nchini Tanzania kwa sasa, huko Uganda mgao wa umeme umekuweko kwa miaka mitatu sasa na ahadi kama hizi za hapa Bongo ni kawaida.
Mgao umeendelea hata pale serikali ya Uganda ilipobinafsisha shirika la Umeme kwa jamaa wale wa Afrika kusini kama tulivyofanya sisi.
Pia msome jinsi Museveni na Besyige walivyofanana.

Saturday, November 18, 2006

NIMEKOSA MKUTANO

Wanaglobu nilijaribu kuingia ukumbini mambo yakashindikana na hivyo nikakosa kikao, inasikitisha sana.
Bassi leo nikasoma haya:Soma zaidi juu ya historia ya mtu mweusi, je kalaaniwa na Mungu? Pia hebu tujue zaidi ni kwa vipi chama tawala nchini Uganda kinavyoruhusu demokrasia?
Alafu huyyu jamaa namzimia kweli kashinda tuzo ya UN.

Friday, November 17, 2006

JOJI KICHAKA ANASAIDIWA NA BABA YAKE

Baba yake Joji Kichaka karudi kumkomboa mwanaye.pIA soma jinsi mpanga mikakati wa Bush alivyochemsha.