My Blog List

Wednesday, November 14, 2007

RAIS KIKWETE ADHIHIRISHA JINSI BUNGE LISIVYOJALI MASLAHI YA NCHI

Sijui niuite ni ukinyonga au niseme nini ila kama kuna siku rais Kikwete kanichekesha ni pale niliposikia kuwa ameunda tume ya kuchunguza na kupitia mikataba ya madini. Mshangao ulinipata baada ya kusikia eti na mheshimiwa Zito Kabwe nae ni miongoni mwa wajumbe wa tume. Kwangu hii ilikuwa ni faraja kusikia hili la kumjumuisha mpinzani ndani ya shughuli kama hii. Zaidi kumjumuisha Zito Kabwe lilinichekesha sana.

Zitto Kabwe ndie mwaanzilishi na mpiga filimbi mkuu aliyethubutu kujitoa mhanga na hatimaye kupewa adhabu ya kutohudhuria kikao cha Bunge kinachoendelea sasa ili kutaka tume ya Bunge iundwe kuchunguza haya rais anayoyaundia tume. Kama mtu unafikiri na si kimgandomgando, unapata hisia kuwa raisi Jakaya Kikwete amelipiga bunge mwereka kimawazo. Ni katika msingi huu Bunge letu hasa vinara wake: Waziri Mkuu na Spika pamoja na wabunge wote waliounga mkono Zitto apewe adhabu wanafanywa ni wajinga ajabu.

1 comment:

Anonymous said...

dah! sijui nianzie wapi ila kusema ukweli blog yako inaboa...! hebu zungumzia vitu positive. huna haja ya kutushika masikio eti uamuzi wa Kikwete ni u-kinyonga. hivi ni lini mtu atafanya jema waandishi mkalisifia?? kama asingeliunda hiyo tume mngemsifia?? jamani waandishi kueni kifikira. msifikiri kila mtu anafurahia mnavyoponda kila kitu viongozi wenu wanavyofanya... kusimamishwa kwa Zitto bungeni kulitokana na taratibu za kibunge, na hazi mnyimi fursa ya kushiriki katika kuondolea taifa kero... Bravo Rais Kikwete, Watanzania tuko nyuma yako kukusapoti kwa kila hali