My Blog List

Wednesday, September 28, 2011

RAIS MPYA ZAMBIA AKARIBISHWA IKULU




Rais mpya wa Zambia bw Sata amekaribishwa Ikulu na kukabidhiwa rasmi mjengo na Rais wa zamani Banda. Hawa jamaa wamepiga hatua sana kidemokrasia.
Serikali mpya tayari imeanza kazi kwa kudhibiti matumizi mabaya ya mali za umma. Kwa mfano, kumbe chama tawala MMD kilikuwa kinatumia magari ya jeshi kwa kampeni. Magari hayo yamekamatwa yote.

DIKTETA IDD AMIN ALIKUWA KIONGOZI BORA

Hivi una habari kuwa Iddi Amin, yule dicteta wa Uganda alikuwa kiongozi bora kuliko Museveni? Soma hii ucheke.

MAMBO YA THE HAGUE



Hawa ni mawaziri wawili wa Kenya. Mmoja ni mtuhumiwa wa mauaji wakati wa uchaguzi, UHURU KENYATA ambaye anashtakiwa huko The Hague ingawa mambo yanaonekana yana mwelekeo mzuri kwake. Anayembusu ni Beth Mugo, waziri wa Afya wa Kenya. Wote ni Wakikuyu, ukabila bila shaka ndio unaowaunganisha.

WANGARI MAATHAI KUPEWA MAZIKO YA KITAIFA



Naamini huyu ndiye mwanamke ambaye alikuwa makini kwa kile alichokiamini. Lakini kama kawaida yetu wanadamu, kifo kimemfika na sasa serikali imeamua itampa maziko ya kitaifa. Profesa Wangari, aliweka wosia kuwa akifa asizikwe na jeneza la mbao kwani ni kuharibu misitu.
Alikuwa ni mwanamke mwanaharakati haswa wala si hawa wanaharakati wa kijinsia ambao uswahiba wao na mafisadi ndio mtindo. Huyu alisimamia alichokiamini akiboresha mazingira na wanawake wa kawaida vijijini na sio hawa wanawake wasomi ambao kwao kutetea wenzao si jambo la msingi sana.
Kifo cha mama huyu kina maana nyingi sana mojawapo ikiwa ni hii hapa na pia alikuwa anajituma kwa alichokipambania. Hii ilimfanya awe tofauti na wengine na pia kwa kiasi kikubwa wengi waliomjua siku zile, wanadai alikuwa mbele yetu sana kiuelewa.

Friday, September 23, 2011

RAIS BANDA AKUBALI MATOKEO YA UCHAGUZIKISTAARABU



MANENO YA MWISHO YA RAIS BANDA AKIWAAGA WANANCHI BAADA YA KUSHINDWA UCHAGUZI

Haya ni maneno ambayo naamini ni viongozi wachache sana tulionao leo hii ambao wataweza kuyasema na kukubali yaishe kwa amani. Hebu yasome alafu utaniambia.

I HAVE CALLED THIS PRESS CONFERENCE TO SAY A FEW WORDS. THE ELECTION CAMPAIGN OF 2011 IS OVER. THE PEOPLE OF ZAMBIA HAVE SPOKEN AND WE MUST ALL LISTEN. SOME WILL BE HAPPY WITH WHAT THEY HAVE HEARD, OTHERS WILL NOT.

THE TIME NOW IS FOR MATURITY, FOR COMPOSURE AND FOR COMPASSION. TO THE VICTORS, I SAY THIS: YOU HAVE THE RIGHT TO CELEBRATE BUT DO SO WITH A MAGNANIMOUS HEART. ENJOY THE HOUR BUT REMEMBER THAT A TERM OF GOVERNMENT IS FOR YEARS.

REMEMBER THAT THE NEXT ELECTION WILL JUDGE YOU ALSO.
TREAT THOSE WHO YOU HAVE VANQUISHED WITH THE RESPECT AND HUMILITY THAT YOU WOULD EXPECT IN YOUR OWN HOUR OF DEFEAT.

I KNOW THAT ALL ZAMBIANS WILL EXPECT SUCH BEHAVIOUR AND I HOPE IT WILL BE DELIVERED. SPEAKING FOR MYSELF AND MY PARTY, WE WILL ACCEPT THE RESULTS. WE ARE A DEMOCRATIC PARTY AND WE KNOW NO OTHER WAY.

IT IS NOT FOR US TO DENY THE ZAMBIAN PEOPLE. WE NEVER RIGGED, WE NEVER CHEATED, WE NEVER KNOWINGLY ABUSED STATE FUNDS. WE SIMPLY DID WHAT WE THOUGHT WAS BEST FOR ZAMBIA. I HOPE THE NEXT GOVERNMENT WILL ACT LIKEWISE IN YEARS TO COME.

ZAMBIA DESERVES A DECENT DEMOCRATIC PROCESS. INDEED, ZAMBIA MUST BUILD ON HER PAST VICTORIES. OUR INDEPENDENCE WAS HARD WON, OUR DEMOCRACY SECURED WITH BLOOD.

ZAMBIA MUST NOT GO BACKWARDS, WE MUST ALL FACE THE FUTURE AND GO FORWARD AS ONE NATION. NOT TO DO SO WOULD DISHONOUR OUR HISTORY.

TO MY PARTY, TO THE MMD CANDIDATES WHO DID NOT WIN, THE LESSON IS SIMPLE. NEXT TIME WE MUST TRY HARDER.
WE FOUGHT A GOOD CAMPAIGN. IT WAS DISCIPLINED. I STILL BELIEVE WE HAD A GOOD MESSAGE AND WE REACHED EVERY PART OF THE COUNTRY.

WE TRAVELLED TO ALL NINE PROVINCES AND WE SPOKE TO ALL ZAMBIANS. TO THOSE WHO WORKED EVERY HOUR OF THE DAY, I SAY ‘THANK YOU’. YOU HAVE DONE YOUR BEST. BUT, SADLY, SOMETIMES OUR BEST IS NOT GOOD ENOUGH.

DO NOT BE DISHEARTENED. THE MMD WILL BE BACK. WE MUST ALL FACE THE REALITY THAT SOMETIMES IT IS TIME FOR CHANGE. SINCE 1991, THE MMD HAS BEEN IN POWER. I BELIEVE WE HAVE DONE A GOOD JOB ON BEHALF OF ALL ZAMBIANS.

FREDERICK CHILUBA LED US TO A GENUINE MULTI-PARTY STATE AND INTRODUCED THE PRIVATE SECTOR TO OUR KEY INDUSTRIES. ZAMBIA WAS LIBERATED BY AN MMD IDEAL BUT MAYBE WE BECAME COMPLACENT WITH OUR IDEALS. MAYBE WE DID NOT LISTEN, MAYBE WE DID NOT HEAR.

DID WE BECOME GREY AND LACKING IN IDEAS? DID WE LOSE MOMENTUM? OUR DUTY NOW IS TO GO AWAY AND REFLECT ON ANY MISTAKES WE MAY HAVE MADE AND LEARN FROM THEM. IF WE DO NOT, WE DO NOT DESERVE TO CONTEST POWER AGAIN.

THE ZAMBIA WE KNOW TODAY WAS BUILT BY AN MMD GOVERNMENT. WE KNOW OUR PLACE IN HISTORY AND WE KNOW THAT WE CAN COME BACK TO LEAD AGAIN IN THE FUTURE. A NEW LEADERSHIP WILL BE CHOSEN, AND THAT LEADERSHIP WILL BE FROM THE YOUNGER GENERATION.

MY GENERATION… THE GENERATION OF THE INDEPENDENCE STRUGGLE– MUST NOW GIVE WAY TO NEW IDEAS; IDEAS FOR THE 21ST CENTURY. FROM THIS DEFEAT, A NEW, YOUNGER MMD WILL BE RE-BORN. IF I CAN SERVE THAT RE-BUILDING, THEN I WILL.

I MUST THANK MY CABINET FOR DELIVERING ON OUR PROMISES. WE DID A LOT OF GOOD FOR ZAMBIA. MANY OF OUR PROJECTS WILL BLOSSOM INTO BRIGHT FLOWERS. SOME OF YOU WILL BE BACK TO SERVE ZAMBIA AGAIN – I KNOW YOU WILL DO YOUR BEST FOR YOUR PARTY AND FOR YOUR COUNTRY.
TO THE CIVIL SERVANTS AND GOVERNMENT OFFICIALS, IT HAS BEEN A PRIVILEGE TO SERVE WITH YOU. WE HAVE WORKED MANY LONG HOURS TOGETHER. WE DID IT NOT FOR OURSELVES BUT FOR ZAMBIA. SERVE YOUR NEXT MASTERS AS YOU DID ME, AND ZAMBIA WILL BE IN GOOD HANDS.

I MUST THANK MY FAMILY AND MY WIFE. THEY HAVE STOOD BY ME AND I CANNOT ASK FOR MORE LOYALTY THAN THAT WHICH THEY HAVE DISPLAYED. I LOVE YOU ALL DEARLY AND I WILL ALWAYS BE IN YOUR DEBT.

BEING PRESIDENT IS HARD WORK, IT TAKES LONG HOURS OF WORK. AND BECAUSE OF IT, I HAVE NOT ALWAYS BEEN THERE FOR YOU. YET, STILL YOU WERE THERE FOR ME.

WORDS CANNOT EXPRESS THE DEPTH OF MY LOVE FOR YOU ALL. ALL I ASK IS THAT MY FAMILY CONTINUES TO SERVE ZAMBIA AS I HAVE SOUGHT TO DO.

BUT MY GREATEST THANKS MUST GO TO THE ZAMBIAN PEOPLE. WE MAY BE A SMALL COUNTRY ON THE MIDDLE OF AFRICA BUT WE ARE A GREAT NATION. SERVING YOU HAS BEEN A PLEASURE AND AN HONOUR. I WISH I COULD HAVE DONE MORE, I WISH I HAD MORE TIME TO GIVE.

OUR POTENTIAL IS GREAT. OUR RESOURCES ARE IMPRESSIVE.
I URGE YOU ALL NOW TO RALLY BEHIND YOUR NEW PRESIDENT.
YES, WE MAY HAVE DIFFERENT IDEAS BUT WE BOTH WANT THE SAME THING – A BETTER ZAMBIA.

NOW IS NOT THE TIME FOR VIOLENCE AND RETRIBUTION.
NOW IS THE TIME TO UNITE AND BUILD TOMORROW’S ZAMBIA TOGETHER. ONLY BY WORKING TOGETHER CAN WE ACHIEVE A MORE PROSPEROUS ZAMBIA.

IN MY YEARS OF RETIREMENT, I HOPE TO WATCH ZAMBIA GROW. I GENUINELY WANT ZAMBIA TO FLOURISH. WE SHOULD ALL WANT ZAMBIA TO FLOURISH. SO, I CONGRATULATE MICHAEL SATA ON HIS VICTORY.

I HAVE NO ILL FEELING IN MY HEART, THERE IS NO MALICE IN MY WORDS. I WISH HIM WELL IN HIS YEARS AS PRESIDENT.
I PRAY HIS POLICIES WILL BEAR FRUIT.

BUT NOW IT IS TIME FOR ME TO STEP ASIDE. NOW IS THE TIME FOR A NEW LEADER. MY TIME IS DONE. IT IS TIME FOR ME TO SAY ‘GOOD BYE’.

MAY GOD WATCH OVER THE ZAMBIAN PEOPLE AND MAY HE BLESS OUR BEAUTIFUL NATION.

I THANK YOU.

KUMBE TANZANIA INAITAMBUA SERIKALI MPYA LIBYA?



Hapo Juu: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akitambulisha na kusalimiana na mwenyekiti wa NTC, serikali mpya ya Libya. Sasa najiuliza, ile kadhia ya kumwita balozi wa Libya eti kapandisha bendera kumbe ilikuwa danganya toto tu.

HUYU ANAOMBA KURA NA BASTOLA KIUNONI


Sitaki kuweka maelezo sana ila Ismail Aden Rage ni Mbunge wa Tabora Mjini. Hapa anaomba kura katika kampeni huko Igunga. Unaionaje hiyo? Kwa mtindo huu, ushindi lazima tu, sijui sheria za uchaguzi zinasemaje juu ya hili.

Thursday, September 22, 2011

UCHAGUZI ZAMBIA NA VIMBWANGA VYA UCHAKACHUAJI

Uchaguzi umemalizika Zambia, lakini kama kawaida, Afrika, hakuna uchaguzi msafi. Kuna kila dalili za uchakachuaji na amani tayari umeanza kuleta dalili za kuvurugika kwa amani. Bofya hapa, upate habari kamili.
Hivi si inawezekana Afrika tunahitaji democrasia ya kiafrika na si hii ya vyama vingi kupiga kura. Naona watawala wanapenda chama kimoja. Wadau mnaonaje?

PIKIPIKI (BODABODA) INANITISHA KUIENDESHA


HAPA NAJIVINJARI SIJUI NIACHE USAFIRI HUU?
Kwa mtanzania wa kawaida kama mie, usafiri ninaomudu ni bodaboda. Mie naendesha ya kwangu lakini hali ya usalama huko barabarani ni mbaya sana. Kwa miezi nane tu iliyopita tayari wamekufa watu 53 kwa ajali za pikipiki.
Najiuliza sijui niache kuendesha au vipi manake ukiacha hivyo vifo, majeruhi ndio usiseme. Angalia taarifa hii ya polisi Tanzania uniambie nifanyeje, hivi kwani nini hasa chanzo cha ajali hizi nyingi hivi? Binafsi huu ni mwaka wa nne naendesha pikipiki, nimepata ajali mara moja tu, na siku hiyo ilinibidi niache kuendesha kwa wiki hivi manake nilipatwa na kiwewe, Mungu alisaidia sikuumia ingawa nilichubuka magotini tu na mtambo haukudhurika. Mwendesha baskeli mmoja mlevi aliingia barabarani nikiwa kwenye spidi, katika kujaribu kumkwepa ndipo nikamgonga na nikaruka mtaroni. Ni Mungu alisaidia tu.
Kwa takwimu hizi za polisi, nimebaki sina majibu kwa usalama wangu, nifanyeje jamani?

Tuesday, September 20, 2011

UGANDA - WEAKLEAKS HAIKANUSHWI ILA YANAFAFANULIWA




Uganda ni nchi ambayo imekuwa chini ya utawala wa Rais Museveni kwa miongo kadhaa sasa. Rais huyo inasemekana sasa ameanza kuwa dikteta na anamuandaa mwanae kumrithi kama ilivyo kawaida kwa viongozi wa kiafrika. Ndani ya chama chake wako watu ambao wamethubutu kuweka wazi juu ya kupinga baadhi ya mambo ambayo anayafanya.
Yuko bwana mmoja, Kapteni Mike Mukula, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa NRM kutoka ukanda wa Mashariki na aliyewahi kuwa waziri wa Afya, amenukuliwa na Wiki Leakes akisema kuwa hakubaliani na mambo ya Museveni na alipohojiwa hakupinga mambo ambayo aliongea na Balozi wa Marekani. Huyu bwana jasiri kwelikweli, tungekuwa na viongozi wa aina hii wanamzunguka Rais wa Tanzania, mbona ingekuwa raha!

Thursday, September 15, 2011

GAIDI LA UGANDA



Kijana wa Kiafrika ni kwanini anaamua kuwa "gaidi" na kuamua kuteketeza maisha ya wenzake? Soma hii uone huko Uganda mfuasi wa magaidi wa somalia.

Tuesday, September 13, 2011

TUMEANZA NA MELI BADO NDEGE

Ajali haina Kinga - Wahenga walisema. Sijui wenzangu mtasemaje ila hizi ajali mbili zilizotokea moja, Zanzibar ambapo meli imezama na ya pile kule Kenya ambapo bomba la mafuta limepasuka na likaua wakazi wengi masikini ambao waliamua kujenga nyumba juu ya bomba la mafuta linadhihirisha kuwa "Ajali ina kinga bwana".
Hebu ona hili: Meli ina uwezo wa kubeba abiria idadi fulani; lakini kwa tamaa na utamaduni wa kuvunja sheria abiria wanashindiliwa kwenye meli mpaka inaelemewa na kuzama. Kama Sheria ya Sumatra juu ya udhibiti wa usalama vyombo vya majini ingesimamiwa, je ajali ingetokea? Tujiulize.
Jambo lingine, jana wakati wa hitma ya kkuwakumbuka marehemu hawa wa meli, Rais JK alieleza jinsi uokozi ulivyofanyika nikashangaa sana. Eti meli imezama saa 7 usiku, yeye kapewa taarifa saa 9. Alafu vyombo vya uokozi vya jeshi na polisi vilishindwa kuiona meli ilipo hadi saa 11 alfajiri, karibu masaa 5, pale helkopta ilivyofanikiwa. Hivi kweli ni sahihi kutumia helkopta moja kutafuta meli? Kwanini hazikutumika helkopta nyingi?
Inashangaza sana, wakati wa Kampeni za Siasa, Raisi anatumia takriban helkopta nne zilizokodiwa kwa mahela lukuki; lakini inaonekana jeshi halina helkopta au hakuna utaratibu wa helkopta sijui nini.
Naamini haswa, kuwa ajali hii ya meli ingeepukika ama pasingetokea kifo hata kimoja.
Maadam watanzania tumekubali kuishi kwa kutozingatia usalama wa maisha yetu; basi sitashangaa hata tukaanza kushuhudia ajali za ndege, kwani sasa hivi, usafiri wa ndege umekuwa sana, na ninaamini kwa tabia yetu ya kutojali usalama, sitashangaa ajali za ndege zikianza.